Mkuu huko kote tumepitia sisi ambao tumesoma hizo shule.
Nimesoma na watoto wa majaji, ma rpc, wakurugenzi wa taasisi, n.k.
Nawajua lamba lamba waliokuwa wana phd za kujikomba kwa hawa watu lakini leo hii maisha yao ni magumu licha ya kuwa na vyeti mpaka chuo.
Kwanza hata hao wazazi usifikiri ni rahisi rahisi tu kwamba anamogia connection rafiki wa mtoto wake, wazazi wengi wana miaka 50+ huko wameishi na wana experience za maisha, Mzazi atampambania mtoto wake sio rafiki yake ambae wakitumia jicho la tatu wanaona kabisa huyu anataka kumtumia mtoto wetu.
Pia mkimaliza hizo shule kila mtu anaenda na njia yake, wachache sana wana stick.
Ukisema umpeleke mtoto wako shule hizo kwa kusema kwamba alambe lambe watoto wa matajiri watampumulia kisogoni aisee, Hawa watoto wa vigogo baadhi nawajua ni wanyanyasaji sana, kuna mmoja alikuwa ana simu nzuri enzi hizo, kuna jamaa alikuwa anajikomba komba ili awe anapewa hio simu, aligeuka kuwa mtumwa kuanzia kumfulia nguo, kumnyoshea nguo, n.k