Mkuu ni ngumu kukupa chakula cha kiroho na ukaelewa kwa maana humuamini mtoa hcho cha kiroho hvyo itakuwia ugumu sana katika kuelewa nin maana ya hcho #KIBALI.
Pili kuhusu kuomba na kupewa baraka na mahitaji yako kwa muumba wako ni lazma umuombe kwa maana unapo muomba ndo unadumisha utukufu wake kwa kumnyenyekea, ndivyo apendavyo kwa maana yey n mkuu na ndo muhimili juu ya vilivyo hai na vilivyokufa.
Ni mfano mdogo tu, hv ulishawah kwenda dukani kwa mangi na noti ya elfu kumi ukakaa kmya tu bla kuzngumza chochote na mangi akajua na kukupa mahitaji yako??
Na kwanin mung akupe mahitaj yako bila kuonesha nia ya uhitaji?? Hapo ndpo linapokuja suala la kuomba kibali
Ila itakuwia ugum kuelewa kwa maaana uamin katika mungu na tayar umeandaa majib yako, ambyo n kinyume cha uzi na mada tajwa hapo juu.
Mungu Yupo na miujiza yake ipo wazi, muda bado unao. Usije ukajua umuhimu wake wakat upo nje ya mda.
#Amiin[emoji1621][emoji1621]
Sifa za Mungu unazijua?
Kwamba ni Mungu muweza wa yote,
Kwamba ni Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele,
Kwamba Mungu ni mwema sana,
Kwamba Mungu ni mwenye upendo,
Kwamba Mungu ni mwenye huruma sana,
Kwa Mungu ni Mkamilifu.
Si ndivyo mnavyo amini au sio?
Sasa tuanze [emoji116]
Mungu mwenye kujua yote, Alishindwaje na Anashindwaje kufahamu mahitaji yako unayo yahitaji mpaka umuombe?
Je anafahamu yote huyo Mungu, Kama tu anashindwa kujua mahitaji yako hadi umkumbushe kwa kumuomba?
Tuendelee [emoji116]
Mungu muweza wa yote, Alishindwaje na Anashindwaje kutoa mahitaji kwa binadamu wote pasipo kukumbushwa na kuombwa?
Je anaweza yote kweli huyo Mungu?
Twende kazi[emoji116]
Mungu mwenye upendo, Alishindwaje na Anashindwaje kutoa baraka zake kwa watu Wote duniani wakafanikiwa maishani wanapo muomba?
Maskini wanaomba kila kukicha, ila Umaskini hauwaishi, wagonjwa wenye magonjwa sugu kama kansa wanamuomba sana wapone ila Hawaponi,
watoto wachanga wanazaliwa na ulemavu kama unjiti, vichwa vikubwa, uchizi na kasoro nyingine nyingi za kimwili lakini Mungu mwenye upendo hajaweza kuwaponya angali wawapo tumboni mwa mama zao.
Huyo Mungu ana upendo kweli?
Huyo Mungu mwenye sifa zote tajwa hapo juu yupo kweli?
Kwa mtu mwenye Akili timamu utagundua kwamba Mungu huyo Hayupo.