Usitafute utajiri, utajiri ni matokeo. Tafuta kibali cha Mungu

Dawa ya chuma ulete na wale wanaojibadilisha ni nini?
 
Walemavu wapo ili utukufu wa Mungu ujirihidhirishe.
Kwamba Mungu anatumia walemavu kujidhihirisha utukufu wake?

Yani watu wana teseka ili yeye ajidhihirishe utukufu wake?

Kwani ni lazima atumie mateso na kuwatesa watu kudhihirisha utukufu wake?

Huyo Mungu mwenye kutumia walemavu, wagonjwa na mateso kudhihirisha utukufu wake ni KATILI sana na hana upendo wowote ule kwa viumbe wake.

Mungu muweza wa yote, Anashindwaje kudhihirisha utukufu wake kwa watu pasipo mateso?

Huyo Mungu yupo kweli?
 
Sawa na baba ana uwezo lakni anashindwa kuwatimizia watoto wake mahitaji yao mpaka aombwe
Yani baba hata akishindwa unaweza kusingizia kuwa ni kwasababu ya ubinadamu tu.

Inawezekna vipi kwa Mungu huyo mwenye sifa kama hizo akasubiri mpaka kuombwa?

Imagine wewe unataabika na unadhiki hujala tangu jana na huelewi mambo yanaendaje,
Then Mungu mwenye uwezo wote ujuzi wote na upendo wote awe anaangalia tu mpaka umuombe?

Waamini walio wengi huwa hawajumuishi maana halisi ya uwezo wote na upendo wote
 
Mkuu ni ngumu kukupa chakula cha kiroho na ukaelewa kwa maana humuamini mtoa hcho cha kiroho hvyo itakuwia ugumu sana katika kuelewa nin maana ya hcho #KIBALI.

Pili kuhusu kuomba na kupewa baraka na mahitaji yako kwa muumba wako ni lazma umuombe kwa maana unapo muomba ndo unadumisha utukufu wake kwa kumnyenyekea, ndivyo apendavyo kwa maana yey n mkuu na ndo muhimili juu ya vilivyo hai na vilivyokufa.

Ni mfano mdogo tu, hv ulishawah kwenda dukani kwa mangi na noti ya elfu kumi ukakaa kmya tu bla kuzngumza chochote na mangi akajua na kukupa mahitaji yako??

Na kwanin mung akupe mahitaj yako bila kuonesha nia ya uhitaji?? Hapo ndpo linapokuja suala la kuomba kibali

Ila itakuwia ugum kuelewa kwa maaana uamin katika mungu na tayar umeandaa majib yako, ambyo n kinyume cha uzi na mada tajwa hapo juu.

Mungu Yupo na miujiza yake ipo wazi, muda bado unao. Usije ukajua umuhimu wake wakat upo nje ya mda.

#Amiin[emoji1621][emoji1621]
 
Hapo huwa sielewi,

Mungu mwenye uwezo wote ujuzi wote na upendo wote halafu tukitaka kitu mpaka tumuombe tena?
Ulimwengu wa roho unaongozwa na matamko
 
Umetoa mfano wa mangi ambae hana ujuzi wote.

Mungu mwenye ujuzi wote anafahamu kabisa shida na magumu unayopitia.

Sasa kama anajua hali yako na anakuacha upitie katika magumu kiasi cha kupoteza maisha kwa njaa, huyo Mungu sie wa haki na hana upendo wote kama asemavyo.

Hivyo hiyo ni test tu katika kuonesha contradiction katika dhana ya uwepo wa Mungu huyo.
Matokeo ya test hiyo yanaonesha kuwa huyo Mungu hayupo in real dimension.
 
Umezaliwa huna hata nguo
Unahangaika na maisha miaka yote uliyo hai, unapata ulichofanikiwa halafu unaondoka mtupu tena kama ulivyokuja

Maisha Raha Sana
Roho za umimi hizi. Tafuta mali vizazi vyako vije viishi vizuri. Hapa ndipo wanapotushindia wazungu
 
Sifa za Mungu unazijua?

Kwamba ni Mungu muweza wa yote,

Kwamba ni Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele,

Kwamba Mungu ni mwema sana,

Kwamba Mungu ni mwenye upendo,

Kwamba Mungu ni mwenye huruma sana,

Kwa Mungu ni Mkamilifu.

Si ndivyo mnavyo amini au sio?

Sasa tuanze [emoji116]

Mungu mwenye kujua yote, Alishindwaje na Anashindwaje kufahamu mahitaji yako unayo yahitaji mpaka umuombe?

Je anafahamu yote huyo Mungu, Kama tu anashindwa kujua mahitaji yako hadi umkumbushe kwa kumuomba?

Tuendelee [emoji116]

Mungu muweza wa yote, Alishindwaje na Anashindwaje kutoa mahitaji kwa binadamu wote pasipo kukumbushwa na kuombwa?

Je anaweza yote kweli huyo Mungu?

Twende kazi[emoji116]

Mungu mwenye upendo, Alishindwaje na Anashindwaje kutoa baraka zake kwa watu Wote duniani wakafanikiwa maishani wanapo muomba?

Maskini wanaomba kila kukicha, ila Umaskini hauwaishi, wagonjwa wenye magonjwa sugu kama kansa wanamuomba sana wapone ila Hawaponi,

watoto wachanga wanazaliwa na ulemavu kama unjiti, vichwa vikubwa, uchizi na kasoro nyingine nyingi za kimwili lakini Mungu mwenye upendo hajaweza kuwaponya angali wawapo tumboni mwa mama zao.

Huyo Mungu ana upendo kweli?

Huyo Mungu mwenye sifa zote tajwa hapo juu yupo kweli?

Kwa mtu mwenye Akili timamu utagundua kwamba Mungu huyo Hayupo.
 
Wewe una elimu ya rohoni, ila usije kujaribu kufanya uzinzi, hicho kibali kinaondoka
 
Ulimwengu wa roho unaongozwa na matamko
Elezea na fafanua kinaga ubaga

Ulimwengu wa roho ni nini?

Ulimwengu wa roho upo wapi?

Ulimwengu wa roho ulitoka wapi?

Otherwise, ulimwengu wa roho ni Fiction stories,Fairytales, Hekaya, dhana za kufikirika, imaginations just an illusion.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…