Utafiti Wangu: Watoto wengi hupenda zaidi ndugu upande wa mama kuliko upande wa baba

Utafiti Wangu: Watoto wengi hupenda zaidi ndugu upande wa mama kuliko upande wa baba

Unalosema ni kweli japo kuna exceptions, niko karibu na ndugu wa baba hasa watoto wa mashangazi, Ila nisipokuwa makini wanangu watakuwa karibu upande wa mama yao as yeye na nduguze wapo so close.

Nilichoamua kufanya, watoto watakwenda kwa babu na bibi (kusalimia)kila ikibidi, watoto wa kaka/dada zangu watakuja au wa kwangu wataenda kila inapobidi. Then na-limit trip za wao huko ukweni[emoji39] how about that Infantry Soldier
Wote ni ndugu zao huna haja ya kubania upande mmoja.
 
Napatana sana na watoto wa ba mkubwa wangu sana yaani unaweza hisi tumezaliwa pamoja kuliko ndugu upande wa mama ni ile hy ya jujuu sana
 
Napatana sana na watoto wa ba mkubwa wangu sana yaani unaweza hisi tumezaliwa pamoja kuliko ndugu upande wa mama ni ile hy ya jujuu sana
Una raha jamani...mimi watoto wa ba mkubwa hata siwafahamu...tunaweza kupishana tu barabarani. Watoto wa baba mdogo wapo watano ila ninaoweza kuwatambua hata nikikutana nao kariakoo ni wawili hao watatu pengine tushapigana vikumbo sana humu mtaani
 
Upande wa mama una nguvu sana,
Najazia tu.....

Nyumba ni mama, wageni wanakuja nyumbani au hawaji sababu ya mama.

Sasa wamama wengi ni wabinafsi, wanapenda zaidi wa kwao. Na wanapasiana watoto ktk kutembeleana. So unakuta watoto wenu wanazunguka kwa ndg zake tu - kwa mamdogo, kwa mamkubwa, kwa mjomba, kwa bibi (ukweni) ndo mzunguko huo.

Walioko kwenye ndoa kongwe wanaelewa zaidi

Hii
 
Yawezekana 50% uko sahihi. Mm naona kwa kiasi kikubwa inategemea ndugu wa upande up mko karibu zaid kwamfano mm nko dom na upande wa baba ndo weng tuko nao karibu
Lakini pia ikiwa uko karibu na ndugu wa pande zote nadhan wa upande wa mama utakuwa nao karibu sana coz wanawake huwa wanashow love sana wenye dada zao watakubali co kama brothers, wamama una bond nzur kwa ndugu zao ila wababa tuko nao kimaslahi sana kwakuwa wanatutaftia pesa
 
Baba na Mama wana jukumu la kuhakikisha watoto wanafahamu familia zao. Kama Mama atakuwa comfortable zaidi kupeleka watoto kusalimia kwao, vile vile, Baba anatakiwa asimamie watoto wafahamu upande wake pia. Sasa we we kama unamuachia mzazi mwenzako apange likizo kwenda kwao halafu hushiriki , mfano , familia nzima iende kijijini kwenu (kama mnatoka kijiji kimoja), mzazi (aidha mama au baba) atajisikia comfortable zaidi kufikia kwao halafu kuenda kusalimia upande wa pili wa familia. Kama mkisafiri wote angalau mnaweza mkafanya 50/50.

Kingine, nilichogundua kwenye familia nyingi, kuna wababa wanakumbatia sana upande wao. Hata wakioa na kuzaa watoto wao, wako radhi kuweka watoto wa kaka na dada zao kwanza kabla ya watoto wao. Kuna makabila mengi, hasa ukikuta baba ni first born,wako radhi hela ikosekane home lakini watoto wa dada na kaka wapate hela walizoomba kwa ba mkubwa.
 
Baba na Mama wana jukumu la kuhakikisha watoto wanafahamu familia zao. Kama Mama atakuwa comfortable zaidi kupeleka watoto kusalimia kwao, vile vile, Baba anatakiwa asimamie watoto wafahamu upande wake pia.
Upo sahihi kabisa mkuu...
 
Back
Top Bottom