Uteketezaji huu wa vifaranga ni unyama uliopitiliza

Hata mimi niliiona hiyo. Ni unyama wa hali ya juu sana. Kitendo hiki hakipaswi kurudiwa.
 
Mwekwzajo wa Tanzania anakufa tunamuangalia tikiachia vifaranga kutoka Kenya...tumeacha kuchoma vya Kenya kulinda viwanda vyetu sasa tunachoma vyetu
 
Bora wangevipakia kwenye reli ya MaguSamia waniletee nikuze nile nyama
Your browser is not able to display this video.
 
Hii zilipendwa

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Ata ili pia mkalitazame!!
 
"However, some certified pasture-raised egg farms are taking steps to eliminate the practice entirely"
the irony wanasema kumlisha kuku-dume ni ghali zaidi ili umle nyama na bado atakua na uzito mdogo & will take longer to mature, now. who bares the cost? kuna kampuni nilisoma waliacha kufanya culling lkn added cost wakaongeza kwenye mayai wanayouza kwa wateja wao. hivyo ni kama hamna namna hii kitu lazima iwe addressed properly in one way or another.
 
Roho imeniuma sana kuona kiumbe hai kinachoma moto!

Kwani hakuna njia nyingine isiyokua ya mateso zaidi ya kuwachoma moto? Kwanini japo wasinge wagawa bure?
 
Ukimsikiliza JK utaona kuna sehemu kwenye hotuba yake wakati akihutubia mkutano wa NEC ulioisha 2022 aliyotoa tahadhari nzuri kwa rais Samia (pamoja na tafasri zingine, ila mi naona hii ndiyo sahihi kwa sasa), moja wapo nadhani ni ku personalize mambo ambayo ni ya kitaasisi. Issue ya vifaranga vilivyochomwa enzi za Dkt Magufuli ilikuwa mambo ya biashara na sababu yawezekana kabisa ilikuwa kama hii ya hawa vifaranga waliochomwa chini ya utawala wa rais Samia. Ila yeye eti kila siku eti tulifikia hatua mbaya ya kuchomeana vifaranga. Nadhani rais Samia, Mama yetu amejionea mwenyewe live bila chenga kilichotokea tena kwa vifaranga vilivyokosa soko
 
Havijaingizwa, vimezalishiwa Moshi. Vimekosa soko baada ya vifaranga kutoka nje kuruhusiwa kuingia na hivyo vya ndani kukosa soko.
 
Ishu ya hao vifaranga ilinitia simanzi sana nikawaza

Kwanini wasigawe bure kwa atakaye?

Kwanini wasipeleke msituni wakavitelekeze ndege na wanyama wajipatie riziki?

Kwanini wasivitose majini samaki na viumbe maji wakajipatie chakula?

Lakini leo tena nimeshangaa eti kuna mradi mkubwa (kuku) wa serikali hukohuko moshi tena

Yaani hata Baruan alisononeka yule kunguru anavyolia pale wakati vinachomwa ni kama vile anataka nyama wakati nyama yenyewe inateketezwa yeye ananyimwa

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…