UTEUZI: Maharage Chande aondolewa TTCL, ateuliwa kuwa Postamasta, Ulanga arudishwa TTCL

UTEUZI: Maharage Chande aondolewa TTCL, ateuliwa kuwa Postamasta, Ulanga arudishwa TTCL

Huyu maharage atakuwa kampigia Mheshimiwa kujitetea siyo bure.

Sasa posta masta nani ataposti barua tena?

Au kazi ya kupokea barua za kuomba kazi, nazo ipo nini ile , mmmh karongwa
Posta juzi wamezindua jengo kali arusha kule, posta si barua tu
 
Sababu gn mtu huyu anahamishwa hamishwa kama mkimbizi? Kama kazi imemshinda si aondolewe? Kwann tunalea ujinga chini ya kivuli cha kuhamisha, kutengua na kuteua? There's obviously a very serious paralytic problem in this government, one doesn't need to be a nuclear physicist to realize the obvious...
 
Kwamba shida/tatizo ni huyo Maharage? Acheni hizo bwana, sote tunajua tatizo lilipo...tunalifumbia macho tu.
So tatizo lipo wapi?
Katiba?
Taasisi ya Urais ikiwemo washauri wake ni kwamba they are incompetent? au kuna kando aliye juu ya Rais kwamba akipitisha kimemo kwa "mama" imeisha hiyo haina kupingwa??!

Inatia ukakasi na kuacha vingi viulizo make sio kwa panga tengua hizi.
Wazee wa CCM mnatatuharibia Nchi mpaka lini?
 
Huyu PostaMasta ambaye ametenguliwa alikuwa vizuri sana aisee halafu bado kijana mdogo mchapakazi sana sijui mama ameonaje aisee
 
Mpaka pale kiharage kinapofyekwa! Kwa msichana... ... ndio mambo hukaa sawa kwa binti Ili aolewe.... Ki-kurya

Kukiacha kiharage.... ni kosa la kiitifaki!.... Hata kiutamaduni wetu sisi wakurya!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

Amemteua Bw. John Ulanga kuwa Balozi. Bw. Ulanga ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Amevunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na amemteua Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Gideon Kingu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Amemteua Bw. Maharage Chande kuwa Postamasta, Shirika la Posta Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Bw. Chande aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Bw. Chande anachukua nafasi ya Bw. Macrice Daniel Mbodo ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Aidha, Mhandisi Peter Ulanga ataendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Kwaiyo Peter ulanga na John ulanga ni ndugu wote wamekua teuzi si ndio
 
Huu ni ubaguzi wa dini kabisaaaaa, wagalatia wengiiii, tunataka usawa,
Sasa ngoja upande ule uzidi kidogo tu japo mmoja uone hayo maneno na mipasho
Muwe mnavumilia kama wenzenu
Hapa naona ni kina john, peter ulanga, jacob
Basi rohooo kwatuuuuuu
 
Hali hii ya teua leo kesho vunja na rekebisha na kesho kutwa badilisha ni dalili tosha za CONFUSION ndani ya utawala. Tuwashauri wakae pembeni tuu, nchi ni muhimu kuliko matumbo yao.
Hii hali haijawahi kutokea katika historia ya nchi hii
IMG-20230925-WA0020.jpg
 
Back
Top Bottom