UTEUZI: Rais Samia afanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri, Manispaa, Miji na Wilaya 184
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Huu uteuzi haujawakomoa mataga na sukuma gang?

Nyie mibavicha hebu leteni majibu
 
Natafuta jina la MWAKIBIBI aliyekuwa Temeke kapangwa wapi
Na yule walipandishana na Meya wa Dar then next day wakawa wameshika maungo eti wamepeana samahani
Anaitwa MWAKABIBI mkuu alipata kuwa boss wangu nikiwa Temeke kabla ya kuhamia Simiyu.
 
Wanawavunja moyo watumishi wakongwe wa local authorities kama wakuu wa idara kwny halmashauri, weo,das nk

Tumepotea njia kwny hili.post ya uDed itokane na maturity, seniority na kuaminiwa kwny local authorities sio favour ya siasa bwana.

Tuna veteran staff kibao wapo bench kwny halmashauri lakin hawaonwi eti.
Mimi siafiki,hao wakuu wa vitengo halmashauri ndiyo wapigaji wakuu.so ukiwakabidhi shamba si ndiyo utaambulia mabua.Wateuliwe watu competent waadirifu kutoka popote.Hakuna anayesomea u-DED.tena hata wakati mwingine wangekuwa wanatoa hata ma CEO wa mashirika makaubwa yanayofanya vizuri.Hamashauri ndiyo injini ya maendeleo ya nchi.Huko ndiyo kila kitu kwa habari ya maendeleo ya nchi.
 
Mnaowafahamu hawa wateule, je Ukada wa CCM kma alivyokuwa Magufuli umeendelezwa na Samia? Professionalism imezingatiwa? Au ni mwendo wa kichama, makada?

Lakini kwa Samia nowadays ataweka rekodi ya uchama ......
Kuna ndugu wa Nape
 
Kiukweli mamlaka ya Uteuzi imeniudhi Sana akiwemo Waziri wa Tamisemi.Inakera Sana mnawatoa watu wanaochapa Kazi na mnawaacha wahuni na wezi.

Mathalani DED wa Sumbawanga MC alikuwa analalamikiwa Sana kwa kutumia nafasi yake kufanya biashara ambapo anauzia Manispaaa anayoiongoza blocks kwenye miradi ya Serikali,mambo ya ubabe na dharau lakini ameachwa.Ukute alikuwa anawahonga watoa taarifa.

Kana kwamba haitoshi Wenye mamlaka wameenda kumtoa DED wa Njombe B.Mwenda ambae sijawahi sikia kashfa yeyote kwake na amwkuwa akifanya vizuri kwenye sekta za maendeleo na kukusanya mapato mengi Sana kwa Mji wa Njombe.

Hata kama mnataka kupachika watoto wenu si bora mngeangalia waliokuwa na kashfa? Mfano wale walionunua magari ya mil.400 si TU kwamba wameachwa ila kwa jeuri walinunua magari Mengine ya kifahari kuonyesha jeuri.

Kwa staili hii it seems ukiwa mtu mzuri,mpenda haki na maendeleo hufai kwenye Serikali hii,Hawa wanataka uwe fisadi Ili uwe unahonga wenye mamlaka.Nimejifunza kitu hapa ukipata nafasi piga pesa sepa .
 
Nimeitetea serikali yangu kwa muda mrefu, nimehangaikia chama, nimesemwa kwa sababu ya kuitetea serikali yangu, ni msomi mzuri, Ila sijabahatika teuzi Hadi leo, Ila nashangaa Kuna watu wawili wamechaguliwa halmashauri mbili tofauti. Dah, Angalia majina Dollar, na Lutengano. Naomba nafasi moja ikikupendeza mh. Rais uniteue nikaitumikie halmashauri
Wewe tafuta watu wa usalama mikoani hao ndio wanapeleka majina na kufanya vetting,Rais ni kutia saini tuu.
 
Back
Top Bottom