Uteuzi: Rais Samia ateua Mshauri wa Sheria na Mshauri wa Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira

Uteuzi: Rais Samia ateua Mshauri wa Sheria na Mshauri wa Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira

Anashauri kuhusu tabia nchi na mazingira Rais wapi na ili afanye nini ?, Kwanini ushauri wake asiupeleke huko kwa wadau ili wautungie sheria na mikakati ? Au kama vipi Rais anapenda sana hii Topic aingie Youtube na kusoma makala mengi tu Online... (At least gharama itakuwa ni bundle na sio package atakayopewa huyu mdau)
Kwani Environment Experts wa NEMC kazi yao ni nini?
 
wawe wanaangalia na kesi alizoshikilia akiwa jaji, zimeendaje, ndicho cha muhimu. most of his cases were poorly handled na huwezi amini kama ndio alikuwa AG.
Kama Mfalme wa Msoga ameamua kuwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali yake awe Mshauri wa Mama Maridhiano,sisi Watanganyika ni nani ata tupinge!
 
Huyu Masaju kama sijakosea alikuwa ndio Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali awamu ya 4 na baada ya Werema kutoka akashika usukani yeye.

Kiufupi hiki cheo cha Mshauri wa Rais mambo ya sheria hakina tofauti kubwa kimajukumu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali maana huyo ndiye mshauri wa serikali na Rais kwa mambo yote ya Kisheria. Kwa lugha nyingine tunaweza kusema Mama ameona Feleshi hatoshelezi
Ukute kuna dili linataka kupigwa kama la escrow sasa Feleshi anaonekana siyo kiungo mchezeshaji mzuri wa UFISADI FC.
 
Umeongea kienyeji sana. Climate change au mabadiliko ya tabianchi ni mada Muhimu sana kwa sasa! Lazima Mkuu wa nchi apate ushauri maridhawa!
Tatizo naliona kwa huyo mteuliwa!
Kwani NEMC kazi yao ni nini?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

1. Amemteua Jaji George Masaju kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Sheria (Advisor to the President – Legal Affairs). Jaji Masaju ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma. Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Aprili, 2023; na

2. Dkt. Richard Stanslaus Muyungi kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira (Advisor to the President – Climate Change and Environment). Kabla ya uteuzi huu Dkt. Muyungi alikuwa Meneja wa Mazingira, katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Aprili, 2023.View attachment 2595400
Kazi ya mwanasheria mkuu ni nini?huyu mtawala yeye kila siku ni kuteua...nchini imepigwa matrilioni ya pesa halafu yeye yupo tu...daaah 2025 sio mbali kura zitaongea
 
Ukimsikiliza Masaju akijibu hoja bungeni ni dhaifu na uwezo mdogo enzi hizo kwani hamna wengine? Hakuna vojana shupavu wenye mawazo mapya?
Ndio maana nikasasema utafikiri samia alikuwa anaish nje ya nchi halafu akarudi halafu hajui watu .samia anayouwezo mdogo mno ila huyu mwanasheria bora binti yangu mwenye cerificicate ya sheria
 
Hapa naona Mama anataka a true,genuine and independent legal adviser, apart from AG na Waziri, kwenye mikataba etc nchi imekuwa inapigwa kila siku na tukipelekwa ICSD au other arbitration forums tunapigwa mchana,mpaka tunashindwa kupeleka ndege zetu kwenye competitive routes.
 
Umeongea kienyeji sana. Climate change au mabadiliko ya tabianchi ni mada Muhimu sana kwa sasa! Lazima Mkuu wa nchi apate ushauri maridhawa!
Tatizo naliona kwa huyo mteuliwa!
Mkuu wa nchi kuna taasisi gani ambayo haimpi ushauri kila kitu kipo under her earshot...., Ningeelewa kuwa na vitengo vya kushughulikia hili jambo mahsusi au kuwaongezea wigo/uwezo watu wa mazingira au Taasisi za Uchunguzi wa Kimazingira...., Anyway sijui huenda hii ni cheaper option (huenda jamaa anajitolea na kazi yake haiji na a Blank Check)
 
Hakuna kujitolea hapo. Atalipwa maposho na usafiri kwa status yake.
Muhimu ni kuwa naiona nchi ikielekea kuwa na sera rasmi kwenye hilo jambo!
 
Hakuna kujitolea hapo. Atalipwa maposho na usafiri kwa status yake.
Muhimu ni kuwa naiona nchi ikielekea kuwa na sera rasmi kwenye hilo jambo!
Sera rasmi sio kuwa na mtu bali taasisi na kwenye ma-vyuo watu kushauriwa kwenye research zao kufanya uchunguzi katika jambo hili hakuna shortcut..., By the way nini kazi ya NEMC (https://www.nemc.or.tz/pages/background) na taasisi kama hizo ?

Au Rais hana namba zao au NEMC hawana contact ya Rais au wakienda kumshauri hawasikilizi....
 
Sera rasmi sio kuwa na mtu bali taasisi na kwenye ma-vyuo watu kushauriwa kwenye research zao kufanya uchunguzi katika jambo hili hakuna shortcut..., By the way nini kazi ya NEMC (https://www.nemc.or.tz/pages/background) na taasisi kama hizo ?
Sitaki kuwa mtabiri sana but I think upo sahihi. Sasa hadi tufike huko kwenye sera ni lazima tuwe na mtu wa ku-coordinate hayo yote!
Kuhusu NEMC hiyo ni taasisi iliyopoteza muelekeo kama Wizara yenyewe.
Highly incompetent kwenye masuala ya mazingira. Sasa hilo la Climate Change ndo kabisa hawawezi kufanya chochote chenye positive implications!
 
Am afraid to say... But NEMC is very incompetent. That said, the agency is broadly incapable of conducting its core duties!
Okay...

But to is the cure rectify their incompetence to appoint an individual to advice and individual about what to do ?, Kama vipi kwanini kwenye zile servant quarters pale ikulu waziweke kachumba kamoja ka NEMC ili washauriane vizuri na Mheshimiwa (akiwa kwenye lunch break)
 
Hivi na mm wataniteua lini jamaaniii??
Unataka ufanye nini ? Kama hicho unachotaka kukifanya kwanini usikifanye mpaka siku uteuliwe..., Kama issue ni kwenda na wewe ulambe asali basi hautufai (utakuwa kupe wa kodi zetu) kama walivyo hao waliopo sasa; kwahio wewe au wao yoyote aliyepo pale outcome itakuwa kama hii iliyopo sasa
 
Okay...

But to is the cure rectify their incompetence to appoint an individual to advice and individual about what to do ?, Kama vipi kwanini kwenye zile servant quarters pale ikulu waziweke kachumba kamoja ka NEMC ili washauriane vizuri na Mheshimiwa (akiwa kwenye lunch break)
Nadhani kuwa na individual at the advisory capacity sijambo baya. You can't just wake up and establish a fully fledged entity. Lazima uwe na pa kuanzia!
Ndugu yangu... Hao NEMC unaowasema ni jina tu... Vinginevyo kusingekuwa na huu uchafuzi wa mazingira uliokithiri kwa sasa Tanzania
 
Unataka ufanye nini ? Kama hicho unachotaka kukifanya kwanini usikifanye mpaka siku uteuliwe..., Kama issue ni kwenda na wewe ulambe asali basi hautufai (utakuwa kupe wa kodi zetu) kama walivyo hao waliopo sasa; kwahio wewe au wao yoyote aliyepo pale outcome itakuwa kama hii iliyopo sasa
Kama wanavyotamani wengine!
Anataka sifa, hela na ukwasi
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

1. Amemteua Jaji George Masaju kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Sheria (Advisor to the President – Legal Affairs). Jaji Masaju ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma. Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Aprili, 2023; na

2. Dkt. Richard Stanslaus Muyungi kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira (Advisor to the President – Climate Change and Environment). Kabla ya uteuzi huu Dkt. Muyungi alikuwa Meneja wa Mazingira, katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Aprili, 2023.View attachment 2595400
Dr muyungi kutoka kuwa mkurugenzi wa mazingira ofisi ya makamu wa raisi hadi kuwa meneja mazingira TANESCO sijui ilikuaje
 
Back
Top Bottom