Uteuzi: Rais Samia ateua Mshauri wa Sheria na Mshauri wa Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira

Uteuzi: Rais Samia ateua Mshauri wa Sheria na Mshauri wa Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira

sema Dr munyungi yupo vizuri sana kwenye maswala ya climate change negotiations maana ndio alikua focal point kwa TZ
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

1. Amemteua Jaji George Masaju kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Sheria (Advisor to the President – Legal Affairs). Jaji Masaju ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma. Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Aprili, 2023; na

2. Dkt. Richard Stanslaus Muyungi kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira (Advisor to the President – Climate Change and Environment). Kabla ya uteuzi huu Dkt. Muyungi alikuwa Meneja wa Mazingira, katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Aprili, 2023.View attachment 2595400
Je Rais anapokea ushauri?

Mambo hayaendi kwa sababu ya ushauri usio na viwango au anayeshauriwa hashauriki?
 
Umeongea kienyeji sana. Climate change au mabadiliko ya tabianchi ni mada Muhimu sana kwa sasa! Lazima Mkuu wa nchi apate ushauri maridhawa!
Tatizo naliona kwa huyo mteuliwa!
tatizo gani unaliona kwa mteuliwa?unamfahamu
 
Sitaki kuwa mtabiri sana but I think upo sahihi. Sasa hadi tufike huko kwenye sera ni lazima tuwe na mtu wa ku-coordinate hayo yote!
Kuhusu NEMC hiyo ni taasisi iliyopoteza muelekeo kama Wizara yenyewe.
Highly incompetent kwenye masuala ya mazingira. Sasa hilo la Climate Change ndo kabisa hawawezi kufanya chochote chenye positive implications!
kweli na huyo DR MUYUNGI ndio aliyekua coordinator na lead negotiator wa karibu COP UNFCC nyingi za climate change na kuwa chairman wa LDC'S kwa hiyo jamaa amewekwa kwenye nafasi anayostahili
 
Umeongea kienyeji sana. Climate change au mabadiliko ya tabianchi ni mada Muhimu sana kwa sasa! Lazima Mkuu wa nchi apate ushauri maridhawa!
Tatizo naliona kwa huyo mteuliwa!
Ana nini huyo mteuliwa wa mazingira wakati amefanyia kazi sekta hiyo kwa zaidi ya miaka thelathini?
 
Am afraid to say... But NEMC is very incompetent. That said, the agency is broadly incapable of conducting its core duties!
thibitiisha hili otherwise ni wivu tu labda ulifanya interview ya kazi hukuchaguliwa
 
Kumbe ni yule jamaa alibanwa na lisu kidogo alie kuhusu escrow

Sio kwamba Masaju hajui lakini Lissu sheria na siasa nyingi sana, Masaju yeye inaonekana sio mtu wa siamba sana.
 
Nilidhani atamteua mtu wa kumshauri namna ya kumrejesha fedha zilizoibwa kwenye ripoti ya CAG.
 
Huyu Masaju kama sijakosea alikuwa ndio Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali awamu ya 4 na baada ya Werema kutoka akashika usukani yeye.

Kiufupi hiki cheo cha Mshauri wa Rais mambo ya sheria hakina tofauti kubwa kimajukumu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali maana huyo ndiye mshauri wa serikali na Rais kwa mambo yote ya Kisheria. Kwa lugha nyingine tunaweza kusema Mama ameona Feleshi hatoshelezi
Nadhani Jaji Feleshi yuko na kazi nyingi sana kwa sasa, itakuwa kateuliwa kwa kazi maalumu hasa ya katiba mpya.
 
Ukute kuna dili linataka kupigwa kama la escrow sasa Feleshi anaonekana siyo kiungo mchezeshaji mzuri wa UFISADI FC.
Hahaha..kama kweli mama ni mpigaji basi atakuwa anajuta sana kumteua Jaji Feleshi kuwa AG, huenda alikuwa hamfahamu vizuri, maana hapo watanyooka tu.
 
Back
Top Bottom