Uturuki imewapiga Wakurdi zaidi mara 1000 ndani siku nne kuretaliate shambulio la kigaidi lilifofanyika. Cha ajabu hatusikii wanaharakati mkilaani

Mfalme au watawala wa Palestina walikuwa kina nani. Mji mkuu wa Palestina ulikuwa upi.
Palestine mji mkuu ama makao makuu toka enzi hizo ilikua ni Jerusalem.
Palestina ilikua Jimbo katika majimbo ya himaya zilizopita,hawakubahatika kujitawala wenyewe.
Palestina ilikuwa kama mkoa wa Ottoman empire. Haina historia, haina milki, haina watawala waliopita, sasa taifa gani halijulikani limetoka wapi.
Kaka wewe una uelewa bana embu acha kuchekesha.
Kama Songea ilikua ina historia yake na viongozi wake kina Songea mbano kwanini Palestina isiwe na historia!?
Je huo mkoa hakuna kiongozi anayeongoza mkoa ambaye ndiye muwakilishi wa himaya katika huo mkoa!?
Palestina ilikua jimbo sio tu kipindi cha Ottoman hata kipindi cha Byzantine pia.
Na ilikua ina kiongozi wa jimbo muwakilishi wa dola husika.
Je hapo unasemaje kuwa haina historia!??
Au neno PALESTINA LILIZUKAJE ZUKAJE!?
Usije ukaniletea historia za biblia.
Niletee walau hata historia ya 1800 hadi 1910 ya historia na watawala wa Israel!??
Angalizo usiniletee historia za biblia.
Haijawahi kuwepo kama ambavyo Palestina haijawahi kuwepo. Sasa kesi zao ni moja, kwanini Wapalestina wawe wapigania haki alafu Wakurdi wawe magaidi?
Mkuu wewe mtu mzima bana usilete utoto sasa.
Kama Palestina haikuwepo BRITISH PALESTINE MANDATE ILITOKEA WAPI!??
Naomba unijibu hilo swali.
Halafu wakurdi ni kabila ambalo asili yake uajemi.
Makabila yote yamekubali kuwa chini ya mataifa mengine,kwanini wakurdi wakatae!??
Palestina imebeba makabila tofauti na ilikua jimbo katika himaya tofauti hadi inafikia kutawaliwa na Uingereza.
Aya unafananishaje na kabila moja la kurdi!??

Palestina ilikuwepo kama haikukuwepo ilikuaje ikatokea mandatory government ya Muingereza hapo!?
Na kuna hadi sarafu za Kipalestina na passport za kusafiria za Palestina na Jerusalem ukiwa kama mji mkuu.
Bro hata historia sidhani kama umesoma.
Huko Iraq wameingia kama walowezi sio asili yao.
Panapowahusu wakurdi ni Iran na Uturuki embu fuatilia historia kipindi Iran inaitwa ANATOLIA KAMA ANATOLIA hadi kuja kwa turkmeni/waturuki hapo na kuingiliana nao.
Wakurdi hawakuwahi kuwa na mipaka kama wamaasai.
Hivyo wakianza kudai kujitenga lazima tuwaone wakorofi.
Mbona wenzao wamekubali kuwa chini ya mataifa mengine kama makabila!???
Huko Iraq wanavamiwa kwasababu hawakuchi kuanzisha matatizo.
Hao hawachelewi kudai kuiongoza Iraq ilhali teyari wana semi-autonomy state.
Hakuna pahala wakakaa kwa amani ni lazima walete fujo.

Sidhani kama kuna hoja hapa zaidi ya kuzungushana tu mkuu.
 
Ndio maana husikii Free Free Kurdistan wakati Kurdish ndio vizazi vya Original Hitites.
 
Ardhi ya nani ambayo Israel ameikalia? Hizo nadharia zenu mlizotengenezewa mkamezeshwa bado mnaziishi?
Palestinians.... hiyo westbank ni Israel?hata tu mipaka ya sasa ya Israel je westbank ni eneo lao? Ila kuna walowezi laki 5 wa Israel. Sasa hiyo ni halali?
 
Palestinians.... hiyo westbank ni Israel?hata tu mipaka ya sasa ya Israel je westbank ni eneo lao? Ila kuna walowezi laki 5 wa Israel. Sasa hiyo ni halali?
Hiyo ni ardhi na hiyo ni mipaka yao ya asili tangu wayback, wakati Palstine waki dominate pal kwa msaada wa Ottoman empire waliwaondoa Wayahudi wengi kutoka maeneo yao.

Ingawa Wayahudi kwenda Ulaya ilikuwepo tangu kipindi kile cha utawala wa Rumi, pia Utawala wa Ottoman uliendelea kuwa sababu ya Wayahudi kukimbilia Ulaya kwa jinsi walivyokuwa wakiwa mistreat sababu ya tofauti ya dini
 
Maelezo marefu yasiyo na mantiki,kwa hiyo unataka kusema wakurdi ni wa kutoka sayari ya Mars hawatakiwi kokote.Umejikita kutetea wakurdi wapigwe tu kwa kuwa eti hawapendwi,mara wanatega mabomu bila sababu,unataka kusema wao hawana masilahi yoyote wana matatizo ya akili ? Tupate elimu zaidi
 
Maelezo yana mantiki vizuri ila akili yako ina ukakasi kwenye kuelewa.
Wakurdi ni kabila miongoni mwa makabila ya Uajemi.
Makabila yenzao yamekubali kuwa chini ya bendera moja,wao ndio kina nani hadi waanzishe fujo kutaka ardhi kila nchi wanayoishi!?
Huko Iraq wao ndio vyanzo vya suicide bombings,Syria pia wanaleta machafuko huku wakiyasambaza na Uturuki.
Unaonekana MTOTO WA TAARIFA wewe.
 
Hiyo ni ardhi na hiyo ni mipaka yao ya asili
Acha ujinga, kama unatoa hii story kwenye bible basi ujue Israel na babu yao Abraham walitokea Syria huko na walikuta Jerusalem ina wakazi tayari na ilishakua na mfalme rejea mwanzo 14 kwahiyo hapo sio asili yao.

Kingine
 
Acha ujinga, kama unatoa hii story kwenye bible basi ujue Israel na babu yao Abraham walitokea Syria huko na walikuta Jerusalem ina wakazi tayari na ilishakua na mfalme rejea mwanzo 14 kwahiyo hapo sio asili yao.

Kingine
Bora ya mjinga, ona ulivyo mpumbavu na brainwashed, Ottoman empire ni story ya bible? Wayahudi kuamia Ulaya ni story ya bible pekee?
Ibrahim yupi aliyetokea Syria? Hata kama alikuta watu pale ndiyo umeambiwa hao watu walikuwa ni Wapalestina? Mnaleta story za kuungaunga wakati ni wavivu wa kusoma na kuelewa, na hata mkiwa mnasikiliza badala ya ku reason ni ninyi mnakua mnajiandaa kubisha...nyamafu
 
Kama Wakurdi hawana haki ya kumiliki ardhi, kwanini Wapalestina wawe na haki hiyo.
Na Kwanini Jews wawe na haki ya kumiliki ardhi kama Palestinians hawana haki ya kumilimiardhi ambao wameitumiak kwa miaka yote tangu maisha yatokee duniani. Kumbuka Ibrahimu aliwakuta wafilisti na aliishi miongoni mwao kwa amani.
 
Tuliza mshono na wenge wewe. Mbona kama vile unaondolewa b-ikra.
 
Hata kama alikuta watu pale ndiyo umeambiwa hao watu walikuwa ni Wapalestina?
Punguza utoto, we si umedai ardhi ile ni ya wayahudi ndio nakwambia sasa walishakuta watu wanaishi mfano Gilgashites, Hivites, Rephaites n.k sasa kwanini huwa mnasema ardhi ni ya wayahudi?

Hata kwenye Bible, mwanzo 14 inaonyesha Abraham anatoa sadaka lwa mfalme wa Jerusalem. Ila utakuta jitu kama wewe unatoka povu kuwa Jerusalem ni ya waisrael.
 
Ibrahim yupi aliyetokea Syria?
Huyu Abraham wa Biblia si alitokea Uru ya wakaldayo sasa kivipi mtu wa Syria huko awe mmiliki wa Israel? Ina tofauti gani na wakoloni waliokuja Afrika alafu baadae waseme wao ndio wamiliki
 
Punguza makamasi usoni hayo, wewe unavyodai ardhi ni ya Wapalestina na ndiyo wanaodai ardhi yao na kuwataka Wayahudi waondoke?, hao wengine unao waleta hapo wametoka wapi?
 
Kwa hiyo ukorofi ni tiketi ya kuuawa?
 
Huyu Abraham wa Biblia si alitokea Uru ya wakaldayo sasa kivipi mtu wa Syria huko awe mmiliki wa Israel? Ina tofauti gani na wakoloni waliokuja Afrika alafu baadae waseme wao ndio wamiliki
Unarukaruka tu kama vi pop-corn na story zako za kuungaunga, Ibrahim gani aliyetokea Syria?
Tangu lini Mesopotamia ilikuwa Syria?
 
Punguza makamasi usoni hayo, wewe unavyodai ardhi ni ya Wapalestina na ndiyo wanaodai ardhi yao na kuwataka Wayahudi waondoke?, hao wengine unao waleta hapo wametoka wapi?
Sababu Palestine limetokana na jina Philistine ambao ni descendants wa hapo kuanzia caphtorites n.k so kwa vyovyote itakavyokua ardhi haiwezi kuwa ya Israel it's either palestine or ancient canaanites
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…