Palestine mji mkuu ama makao makuu toka enzi hizo ilikua ni Jerusalem.Mfalme au watawala wa Palestina walikuwa kina nani. Mji mkuu wa Palestina ulikuwa upi.
Palestina ilikua Jimbo katika majimbo ya himaya zilizopita,hawakubahatika kujitawala wenyewe.
Kaka wewe una uelewa bana embu acha kuchekesha.Palestina ilikuwa kama mkoa wa Ottoman empire. Haina historia, haina milki, haina watawala waliopita, sasa taifa gani halijulikani limetoka wapi.
Kama Songea ilikua ina historia yake na viongozi wake kina Songea mbano kwanini Palestina isiwe na historia!?
Je huo mkoa hakuna kiongozi anayeongoza mkoa ambaye ndiye muwakilishi wa himaya katika huo mkoa!?
Palestina ilikua jimbo sio tu kipindi cha Ottoman hata kipindi cha Byzantine pia.
Na ilikua ina kiongozi wa jimbo muwakilishi wa dola husika.
Je hapo unasemaje kuwa haina historia!??
Au neno PALESTINA LILIZUKAJE ZUKAJE!?
Usije ukaniletea historia za biblia.Meanwhile Wayahudi wana historia ya watawala, ushahidi wa kihistoria wa tangu enzi na enzi. Tangu watawala wa dola la Kirumi wapo hata hiyo Ottoman haijakuwepo. Kabla hata tawala za Kiislamu wala dini yenyewe ya Kiislamu kuwepo Middle East tiyari Wayahudi wana rekodi ardhi hiyo.
Niletee walau hata historia ya 1800 hadi 1910 ya historia na watawala wa Israel!??
Angalizo usiniletee historia za biblia.
Mkuu wewe mtu mzima bana usilete utoto sasa.Haijawahi kuwepo kama ambavyo Palestina haijawahi kuwepo. Sasa kesi zao ni moja, kwanini Wapalestina wawe wapigania haki alafu Wakurdi wawe magaidi?
Kama Palestina haikuwepo BRITISH PALESTINE MANDATE ILITOKEA WAPI!??
Naomba unijibu hilo swali.
Halafu wakurdi ni kabila ambalo asili yake uajemi.
Makabila yote yamekubali kuwa chini ya mataifa mengine,kwanini wakurdi wakatae!??
Palestina imebeba makabila tofauti na ilikua jimbo katika himaya tofauti hadi inafikia kutawaliwa na Uingereza.
Aya unafananishaje na kabila moja la kurdi!??
Palestina ilikuwepo kama haikukuwepo ilikuaje ikatokea mandatory government ya Muingereza hapo!?Kama ambavyo Palestina ulikuwa mkoa tu ndani ya Ottoman empire. Ndio maana hakuna Mfalme wa Palestina wala royal family wala Repuplic wala mji mkuu wala historia ya taifa.
Wakurdi wana claims zaidi ya ndani ya Iran. Wamasai hawana historia kama taifa, hawajawahi kuwa na mji mkuu ingawa wana machifu wao, hawajawahi kuwa na mpaka sasa wakianza kudai nchi yao tutawashangaa kama Wakurdi na Wapalestina.
Na kuna hadi sarafu za Kipalestina na passport za kusafiria za Palestina na Jerusalem ukiwa kama mji mkuu.
Bro hata historia sidhani kama umesoma.
Huko Iraq wameingia kama walowezi sio asili yao.Hata hivyo Wakurdi wananyanyaswa kila nchi walipo, hivyo basi wapewe ardhi ya asili yao kama nchi ili ambapo kote hawatakiwi warudi kwao. Huwezi goma kuwashirikisha kitaifa alafu unagoma wasijitenge. Biafra ingekuwa taifa sababu ya kutengwa, South Sudan imetokana na hiyo sababu.
Sasa remnants wa Persia hawawataki, na hawatakiwi kwingineko wanabaguliwa. Ni sawa kulazimisha Austria na Hungary kurudia kuwa nchi moja kisa "mbona zamani zilikubali kuwa Austro-Hungary".
Hawajataka kujitenga karne hii, wameanza tangu karne iliyopita. Walianza wanataka watambuliwe, ikashindikana wakataka basi wakae peke yao. Kila jamii zinazowazunguka zinawaona makafiri.
Wakurdi unaosema panapowahusu ni Iran tu ndio haohao wana jimbo la Kurdistan ndani ya Iraq, wana special representative bungeni. Na wanatengwa wamevamiwa na Repuplican Forces ya Iraq enzi za Saddam Hussein. Unasemaje wanahusika na Iran pekee.
Panapowahusu wakurdi ni Iran na Uturuki embu fuatilia historia kipindi Iran inaitwa ANATOLIA KAMA ANATOLIA hadi kuja kwa turkmeni/waturuki hapo na kuingiliana nao.
Wakurdi hawakuwahi kuwa na mipaka kama wamaasai.
Hivyo wakianza kudai kujitenga lazima tuwaone wakorofi.
Mbona wenzao wamekubali kuwa chini ya mataifa mengine kama makabila!???
Huko Iraq wanavamiwa kwasababu hawakuchi kuanzisha matatizo.
Hao hawachelewi kudai kuiongoza Iraq ilhali teyari wana semi-autonomy state.
Hakuna pahala wakakaa kwa amani ni lazima walete fujo.
Sidhani kama kuna hoja hapa zaidi ya kuzungushana tu mkuu.