Unaona kaka sasa unavyokua unayabananga mambo!??
Palestina ilikuwepo toka enzi.
Mfalme au watawala wa Palestina walikuwa kina nani. Mji mkuu wa Palestina ulikuwa upi.
Na ndio maana hata katika historia ya Muingereza miongoni mwa maeneo aliyoyatawala ni Palestina.
Palestina ilikuwa kama mkoa wa Ottoman empire. Haina historia, haina milki, haina watawala waliopita, sasa taifa gani halijulikani limetoka wapi.
Meanwhile Wayahudi wana historia ya watawala, ushahidi wa kihistoria wa tangu enzi na enzi. Tangu watawala wa dola la Kirumi wapo hata hiyo Ottoman haijakuwepo. Kabla hata tawala za Kiislamu wala dini yenyewe ya Kiislamu kuwepo Middle East tiyari Wayahudi wana rekodi ardhi hiyo.
JE UNAWEZA KUNIAMBIA KURDISTAN ILIWAHI KUWEPO KABLA!???
Haijawahi kuwepo kama ambavyo Palestina haijawahi kuwepo. Sasa kesi zao ni moja, kwanini Wapalestina wawe wapigania haki alafu Wakurdi wawe magaidi?
Kurdi ni kabila kama unavyoona Fursi.
Kurdi ilikua kabila ndani ya Anatolia au Persia.
NARUDIA TENA,KURDI ILIKUA KABILA NDANI YA ANATOLIA/PERSIA/IRAN.
Kama ambavyo Palestina ulikuwa mkoa tu ndani ya Ottoman empire. Ndio maana hakuna Mfalme wa Palestina wala royal family wala Repuplic wala mji mkuu wala historia ya taifa.
KURDI walitakiwa wawe chini ya IRAN HADI SASA KWASABABU KURDI ILIKUA NI MIONGONI MWA MAKABILA YA KIAJEMI.
Ni sawa useme wamaasai waanze kupambania taifa lao.
Wakurdi wana claims zaidi ya ndani ya Iran. Wamasai hawana historia kama taifa, hawajawahi kuwa na mji mkuu ingawa wana machifu wao, hawajawahi kuwa na mpaka sasa wakianza kudai nchi yao tutawashangaa kama Wakurdi na Wapalestina.
Hata hivyo Wakurdi wananyanyaswa kila nchi walipo, hivyo basi wapewe ardhi ya asili yao kama nchi ili ambapo kote hawatakiwi warudi kwao. Huwezi goma kuwashirikisha kitaifa alafu unagoma wasijitenge. Biafra ingekuwa taifa sababu ya kutengwa, South Sudan imetokana na hiyo sababu.
Huo si uwendawazimu!??
Mbona tangia karne zilizopita walikubali kuwa chini ya himaya moja ya Persia???
Sasa remnants wa Persia hawawataki, na hawatakiwi kwingineko wanabaguliwa. Ni sawa kulazimisha Austria na Hungary kurudia kuwa nchi moja kisa "mbona zamani zilikubali kuwa Austro-Hungary".
Kwanini karne hii ndio watake kujitenga!??
Huko Syria na Iraq hapamuhusu huyo KURDI.
Kurdi panapomuhusu ni IRAN na Uturuki ambapo Uturuki yenyewe imeiba sehemu ya IRAN/ANATOLIA ilipohama toka Central Asia.
Hawajataka kujitenga karne hii, wameanza tangu karne iliyopita. Walianza wanataka watambuliwe, ikashindikana wakataka basi wakae peke yao. Kila jamii zinazowazunguka zinawaona makafiri.
Wakurdi unaosema panapowahusu ni Iran tu ndio haohao wana jimbo la Kurdistan ndani ya Iraq, wana special representative bungeni. Na wanatengwa wamevamiwa na Repuplican Forces ya Iraq enzi za Saddam Hussein. Unasemaje wanahusika na Iran pekee.