Uvujaji wa taarifa nyeti: Je, TISS kuna tatizo?

Uvujaji wa taarifa nyeti: Je, TISS kuna tatizo?

Yes or No ila angekuwa mtu wao asingeruhusiwa kumtusi Sponsor wake
Huyu jamaa inawezekana anacheza na akili za watu tu!
Na siyo ajabu ikawa ni mbinu ya hao tiss kuwatafuta wale wanaompinga meko kwa kumtumia huyo mshikaji!
Ipo siku atawageuka wote wanaomshadadia, then ataishia kutukanwa!
Kuna wakati anageuza upepo na kuwafumua akina zitto, mbowe n.k! Hivyo inawezekana yupo kimkakati, na tunavyoaminishwa anatafutwa, ni moja wapo ya mbinu za kutekeleza mkakati mzima!
Huyo ni system kabisa huenda!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Serikali ilivyo kama angekubali muamala lazima wangemuexpose tu
Mange wametumwa mpaka watu Marekani! Mahiga R. I. P kafanya transaction Mange kapoa ! we endelea kujifungia kwenye korido za lumumba huna unachojuwa!
 
Sponsor asingekuwa anatukanwa matusi makubwa
Kwanza tukubali hio ID ya kigogo haiendeshi na mtu mmoja sasa kuanzia apo tukiconnect dot na ilo wazo lako huenda ni sytem linaweza kuwa na uzito mana ingekuwa wa nje wangefahamika as unavyojua siri ni mtu mmoja tu
 
Sio kwamba kwenye utawala wa BM na JK siri za serikali na viongozi wake zilikuwa hazivuji zilivuja ila sasa imekuwa too much.

Alianza Mange kuvujisha mambo very sensitive na alileta taaruki kweli na baadhi ya mambo ulikuwa ukitizama unaona kabisa yanatoka ndani jikoni.

Sasa hivi Kigogo kuna muda anazusha sawa ila kuna muda anaongea ukweli 100%.

Tujiulize nani anampa taarifa? je kama yupo ndani hakuna tatizo? hata kama hayupo ndani je waliopo kama hawana umoja hakuna tatizo? TISS kuna tatizo lazima tukubali kwanza!

Je ni kutokana na "TISS field officer" wakienda na kuleta taarifa hazifanyiwi kazi kulingana na matakwa ya mtu mmoja? Wakipuuzwa wanauza taarifa za usalama?

Pls Diwani rekebisha mambo ingawa its to late! Kwako kuja kutolewa kama Kapilimba kuna viashiria vyote vinaonyesha Idara imegawanyika sana kuliko kipindi chochote toka tupate uhuru.
Utakua bado kijana Sana
Siri za sasa ni petty

Enzi zile tulikua tunaona Siri sirini kwelikweli

Siku hizi ni rumors tu
 
Naomba niwashauri idara yetu nyeti ya TISS kuhusu jinsi mnavyomfuatilia Kigogo2014 ili kumweka mikononi mwenu kwa sababu ya kutoa siri nzito nzito za Serikali.

Niwaeleze ukweli kwamba, Kigogo2014 hamuwezi kumkamata hata iweje kwa sababu Kigogo siyo mtu mmoja bali ni syndicate kubwa ndani ya syndicate nzito na yenye nguvu kubwa.

Inasemekana zimetumika zaidi ya Bil 1.4 kumsaka Kigogo, mmeshindwa kubaini ukweli na badala yake mnazidi kupoteza pesa za umma kumsaka mtu ambaye hamuwezi kumpata.

Ujio wa Kigogo umesababishwa na uwepo wa utawala mbovu, unaominya haki za Binadamu Uhuru wa Habari, Demokrasia na uharibifu mkubwa wa uchumi.

Badala ya kujikita kwenye kuleta maendeleo, awamu ya Tano imetumia Pesa za umma kununua wapinzani na kuvuruga Demokrasia.

Ajira ya TISS imejikita zaidi kwa vijana wa UVCCM na siyo kwa intelligence experts, sasa watu Kama hao watawezaje kumpata mtu mwenye level ya Mossad na CIA?

Uongozi hauhitaji mabavu bali hekima, unapoamua kuwa mbabe na kwa sababu unawaongoza siyo mbuzi, ni watu wenye akili zao, tarajia kukutana na ma whistle-blowers wengi.

Na mwisho wa siku utashindwa tu, tatizo lenu mnatumika kisiasa sana, yaani mpo kwa ajili ya kuhakikisha CCM inatawala milele na siyo kwa ajili ya ustawi wa nchi.

Awamu hii hii ya Tano inayosifika kwa kukamata wakwepa kodi, kuna kampuni nyingi tu nazijua na nina ushahidi mkubwa kuwa zinakwepa kodi. Ajabu eti serikali makini haijui, ila serikali hiyo hiyo inajua ni lini Mbowe atafanya mkutano wa ndani ili waweze kumdhibiti asichafue amani ya nchi, kichekesho kweli.

Kama Trilioni 1 ilipotea na CAG akatolewa kwa kusema ukweli, basi acha watu wakwepe kodi. TISS wapo bize kuwarekodi kina Steve Nyerere wakiigiza sauti ya Mbowe anamnyanyapaa kimapenzi mbunge wa Chadema (jina linahifadhiwa)

Yaani badala ya kufanya mambo ya msingi kwa Taifa mnatumika na mambo ya hovyo, baada ya Kigogo kuwavua nguo huko Twitter sidhani kama bado mnaendelea tena na hujuma dhidi ya Mbowe.

Fanyeni ishu za maana kwa Taifa, acheni roho ya usaliti kwa Taifa, vinginevyo mtadukuliwa mno.
Long live Kigogo2014.
 
Tupo macho tunawachunguza hao TISS. Nikumbusheni yule jamaa aliyesumbua serikali ya Mzee Mgabe kule Zimbambwe hadi akatangaza donge nono la madolae ili akamatwe kisa anatoa taarifa nyeti ya serikali iliyoshindwa, bado walishindwa kumkamata.

Watumishi wengi wa TISS hawajui majukumu yao bali wanatumika kwa wenye nia mbaya na nchi yetu.
 
Back
Top Bottom