Uvujaji wa taarifa nyeti: Je, TISS kuna tatizo?

Uvujaji wa taarifa nyeti: Je, TISS kuna tatizo?

Uzuri wake ni kwamba anavujisha kabla hila za CCM halafu inavurugika
Ngoja nirudi twitter kumsoma kigogo, maana nondo zake sio za dunia hii.

Mm nachomsifia kautonya umma juu ya mipango haramu juu ya Mbowe na sasa wanaona aibu jinsi ya kuileta kwa hadhara.
 
Naomba niwashauri idara yetu nyeti ya TISS kuhusu jinsi mnavyomfuatilia Kigogo2014 ili kumweka mikononi mwenu kwa sababu ya kutoa siri nzito nzito za Serikali.

Niwaeleze ukweli kwamba, Kigogo2014 hamuwezi kumkamata hata iweje kwa sababu Kigogo siyo mtu mmoja bali ni syndicate kubwa ndani ya syndicate nzito na yenye nguvu kubwa.

Inasemekana zimetumika zaidi ya Bil 1.4 kumsaka Kigogo, mmeshindwa kubaini ukweli na badala yake mnazidi kupoteza pesa za umma kumsaka mtu ambaye hamuwezi kumpata.

Ujio wa Kigogo umesababishwa na uwepo wa utawala mbovu, unaominya haki za Binadamu Uhuru wa Habari, Demokrasia na uharibifu mkubwa wa uchumi.

Badala ya kujikita kwenye kuleta maendeleo, awamu ya Tano imetumia Pesa za umma kununua wapinzani na kuvuruga Demokrasia.

Ajira ya TISS imejikita zaidi kwa vijana wa UVCCM na siyo kwa intelligence experts, sasa watu Kama hao watawezaje kumpata mtu mwenye level ya Mossad na CIA?

Uongozi hauhitaji mabavu bali hekima, unapoamua kuwa mbabe na kwa sababu unawaongoza siyo mbuzi, ni watu wenye akili zao, tarajia kukutana na ma whistle-blowers wengi.

Na mwisho wa siku utashindwa tu, tatizo lenu mnatumika kisiasa sana, yaani mpo kwa ajili ya kuhakikisha CCM inatawala milele na siyo kwa ajili ya ustawi wa nchi.

Awamu hii hii ya Tano inayosifika kwa kukamata wakwepa kodi, kuna kampuni nyingi tu nazijua na nina ushahidi mkubwa kuwa zinakwepa kodi. Ajabu eti serikali makini haijui, ila serikali hiyo hiyo inajua ni lini Mbowe atafanya mkutano wa ndani ili waweze kumdhibiti asichafue amani ya nchi, kichekesho kweli.

Kama Trilioni 1 ilipotea na CAG akatolewa kwa kusema ukweli, basi acha watu wakwepe kodi. TISS wapo bize kuwarekodi kina Steve Nyerere wakiigiza sauti ya Mbowe anamnyanyapaa kimapenzi mbunge wa Chadema (jina linahifadhiwa)

Yaani badala ya kufanya mambo ya msingi kwa Taifa mnatumika na mambo ya hovyo, baada ya Kigogo kuwavua nguo huko Twitter sidhani kama bado mnaendelea tena na hujuma dhidi ya Mbowe.

Fanyeni ishu za maana kwa Taifa, acheni roho ya usaliti kwa Taifa, vinginevyo mtadukuliwa mno.
Long live Kigogo2014.
Sijaona ushauri. Nikajua 40 za kigogo 2014 zimefika kumbe upupu tu.

TISS we iache tu.
 
Kigogo Ni mwongo mi nlishaachaga kufuatilia post zake huko tweetani,kunasiku kamzushia kifo mama mmoja anawadhifa serikalini Ni jiran yetu hapa eti amekufa kwa covid 19 na familia yake wamelazwa 🙂🙂
 
Hapoa sijaona hata ushauri pumba tupu tuu. Sijaona athari za huyo kigogo acha aendelee na maisha yake ashapuuzwa tuuu.
 
Kigogo Ni mwongo mi nlishaachaga kufuatilia post zake huko tweetani,kunasiku kamzushia kifo mama mmoja anawadhifa serikalini Ni jiran yetu hapa eti amekufa kwa covid 19 na familia yake wamelazwa [emoji846][emoji846]
Uliweka evidence kuonesha sio sahihi?
 
Uliweka evidence kuonesha sio sahihi?

Mtoto wa huyo mama aliweka evidence na kuthibitisha wako fine,ningeweka mm isingesaidia.Kigogo mda mwingine anacheza na akili za watu kwa mfano ile ishu za tuhuma ya mbowe zilizotolewa na wabunge walio Hana chama,hata mtoto mdogo angejua what next
 
Hivi mtu anayejielewa atapoteza muda kumtafuta mtu ambaye hajulikani?

Huyo ni mropokaji tu
Ona unavyoyavaa mabomu ya kuwalipua ccm wenzako! Kumbe mawaziri na hata wakuu wako wa ccm walioagiza kigogo asakwe kwa gharama yoyote hawajielewi?
Hebu weka hapa sifa za mtu anayejielewa aliyepo ccm tumjue! Bora leo umeamua kuuishi ubinadamu wako na ccm wanaoagiza kukamatwa kwa kigogo wamekuelewa!
 
kwakuwa anayooandika huyo kigogo hayazuii barabara, reli,meli, hospitali, shule na n.k kujengwa wacha aandike tu, wananchi wanaona
Wananchi hawapo kuona maflyover Wala mabarabara yanayojengwa Bali wanataka kuiona uchumi Bora na umaskini wa kipato unaondoka! Acha kuwasemea wasiyoyahitaji!
 
TISS haipo simple kama mnvayo ichukulia. Ina watu smart na wenye IQ kubwa sana na wanatenda kwa sehemu zao kwa weledi wa hali juu,vivyo hivyo kuna vichwa maji mle na ndio wanaipaka idara matope ya mavi...
Nakubaliana na wewe. Mle kuna agents smart sana, pia kana mazwazwa sana yaliyotokea Uvccm na waloajiriwa kimjomba
 
Wananchi hawapo kuona maflyover Wala mabarabara yanayojengwa Bali wanataka kuiona uchumi Bora na umaskini wa kipato unaondoka! Acha kuwasemea wasiyoyahitaji!
uchumi bora pia unapatikana kwa kuwa na miundo mbinu bora ili kurahisisha bidhaa au mazao kufika sokoni haraka na kwa wakati ili muuzaji auze na kurudi shamba kuendelea na shughuli nchi zote zenye uchumi bora zina miundo mbinu bora pia, kuhusu umasikini wa kipato huisha kwa kufanya kazi tu ni serikali chache duniani zinazotoa hela bure kwa watu wake bila kufanya kazi, nakushauri achana na kuzungusha mikono chapa kazi.
 
kwa mfano kigogo mm namuona ni mzalendo wa kweli. na anaipenda tanzania. kama kigogo angekuwa ni mtu mbaya angewaua wote anao wapinga kwa7bu siri zao zote anazo kiganjani. kwamba wanalala saa ngapi wanakula nini nk.
 
Wanaomfatilia kigogo hawana tofautina zama za Mange, upupu mtupu. Hakuna siri yoyote zaidi ya umbea, na sisi kwa kupenda umbea hata hatuchuji mambo.
 
Back
Top Bottom