Uzeeni mwanaume ana uhitaji wa ndoa zaidi kuliko mwanamke. Chukua hatua

Naona labda wewe hujaelewa, nasio wewe tu bali ni wengi humu ndani hamjaelewa.

Watu wanaposema kataa ndoa haina maana ya kuwa single au usiishi na mwanamke ...

Nadhani mifano hiyo ipo na imetolewa humu mara nyingi tu na sio vyema kuirudia rudia .

Mfano Ronaldo hajaoa lakini anaishi na mwanamke na anawatoto.
 
Uwongoo..
Siku hizi mwanamke ukiwa mzee anakusaidia ufe mapema atawale miradi...
Mimi binafsi babu yangu alikuwa mwalimu na alistaafa 1996..

Bibi yangu alikufa kitambo ila babu yangu babu anaonekana kama si mzee kabisa na anaishi pekee yake anapika mwenyewe na kazi ndogo ndogo za hapo kwake na nguo anamashine yake ya kufua licha ya kwangu ana watoto 9 wa kuzaa lakini kila mtoto anapambana na hali yake na wamesambaa na wengine ni wagonjwa, sisi wajukuu hatuna msaada sana kwake tunapambana na hali zetu kifupi hatutegemei hata kidogo...

Kipindi bibi yupo kuliko na magomvi sana hapo kwa babu..
hivyo usiwe na wazo hilo eti ndoa ni muhimu mzeeni
 
Kuwa na adabu weye kijana, mwanaume kamwe hazeeki bali anaongezeka umri tu, ndiomaana hata kibabu cha 80 kinaweza kumpa mimba mwanamke,.

Mna mawazo ya kishirikina kuwa nilazma mtu augue akipata umri mkubwa, wew hauna tofauti na wale wanawake wanaodhania wao wataishi umri mkubwa kuliko waume zao, hivyo basi ndoa isiwe kisingizio kuwa ukifikia umri mkubwa utakosa wa kukusaidia, je huyo mwanmke akifa? Utaoa mwngne nae akifa ama asipotimiza wajibu wa kukuhudumia? Ungesema vijana watafute pesa ili hata wakipata madhaifu waweze kujitibu bila utegemezi wala usumbufu kwa watu wengine,

Vijana kataeni ndoa za michongo
 
Ni kweli kabisa hii nimeona kwa wanaume wengi wakipata shida sana uzeeni. Yaani hadi unamuonea huruma anataka msaada wakati alikuwa Mwenyekiti wa Kijiwe cha Kataa Ndoa.
 
Kwa hali mbaya ya umaskini hapa nchini tuweke nguvu kubwa kuwahamasisha vijana wajikomboe kiuchumi. Fikiria mtu anaoa hana ajira wala kipato cha kumwezesha tu kulipia bima ya afya kwa familia yake... ikitokea dharura tu ya kwenda mkoani lazima aumize kichwa kwanza kupata nauli.... hana akiba ya kumtosha kutumia hata kwa mwezi mmoja mbele... yaani zile basic needs tu kwake ni tia maji tia maji!!.. haya mambo ya ndoa tuache NATURE ifanye kazi yake.. hakuna haja ya kushawishiana wala kulazimishana sana. UMASKINI NDO UNALETA MATATIZO MENGI SANA KWENYE FAMILIA NA JAMII KWA UJUMLA. VIJANA TAFUTENI TU HELA KWA SASA TUJIKOMBOE KIUCHUMI.
 
Umeandika maneno mengi ila pointi ni kuwa "ndoa haikuhakikishii kuwa na uzee mzuri, unaweza ukawa na ndoa na ukawa na uzee wenye full stress na hata ukafa"

Pia jamii nayotoka mimi wazee wenyi tu wanaishi pekee yao licha kwa waliwahi kuwa ndoa
 
Ujinga mtupu

1. Una uhakika gani kama utafika hata 50 years ?

2. Kuoa hai guarantee wewe ukizeeka utaishi vizuri .

3. Sikweli kwamba wanawake wanaumaliza uzee vizuri na wanaume vibaya ninaweza kukupa mifano lukuki tu iliyo hai (mfano mdogo tu sijui umeshawahi kufuatilia maisha ya wale shaolin monks mtu anafika hadi miaka 100 bado ana nguvu na anajitegemea kwa manbo mengi , Au umewahi kuishi kijiji chochote chenye wazee wengi? )

4. Kuwa mwanaume na kuzeeka vibaya inategemeana na factors nyingi NDIYO MAANA UNAAMBIWA UTUNZE MWILI WAKO NA UWE KARIBU NA MUUMBA WAKO SANA UNAKUTA MTU HAULALI VIZURI , UNATUMIA MA VINYWAJI MAKALI YANAYOTESA NA KUUMIZA INI ,HAPO UNAKULA MLO USIO KAMILI HAUFANYISHI MWILI KAZI ANGALAU UTOKE JASHO KIDOGO HALAFU UNATARAJIA KUFIKA UZEENI MWILI UWE SAWA ??
 
Tatizo mnaendekeza umama sana kifupi you are dick driven.


Ni hivi hawa wanawake ni wajanja sana kwa wanaume wapumbavu.

Tangia unapo muoa anakutenganisha wewe na marafiki, wewe na hobby zako, wewe na ndugu zako, yaani anahakikisha umebaki wewe kama wewe......na wewe ulivyo zoba unachekelea na kukenua mimeno ukisema my woman she loves me......men wewe ni boya. Huyo mwenzio anakufanyia hayo ili umtumikie fully usibakishe hata dakika. Ukisha maliza kumsomeshea watoto kumjengea na nguvu zimekuuisha na watoto wanajiweza basi biashara yako ndio imeishia hapo.

Huna marafiki, huna kijiwe cha kucheza bao na kuzuga taani ndugu zako ulisha kosana nao.,marafiki nao uliwakimbia sasa unabaki wewe na korodani zako.

Lkn ukikutana na mwanaume aliwajulia wanawake na michezo yao huji kumkuta analia lia na sijui stress sijui upweke nk....yeye akikaa na vijana burudani akikaa na wazee wenzie wanasema hajiheshimu , na mbususu mbichi na kali bado anaendelea kuzilamba ambazo hata vijana wanaziogopa
 
Yote haya yatakukuta ikiwa umezeeka ukiwa lofa
 
Really
 

Uliwahi ishi na babu au kwenu kuna wazee?

Kwa Sisi tuliokua tukizungukwa na Wababu na wabibi zaidi ya 10 wenye umri usiopungua miaka 80 kitu muhimu Kwa uzee ni Pesa za kuwahudumia wazee na sio hizo habari za ndoa.
 
Kibailojia mwanamke ndio mhitaji mkubwa wa ndoa kuliko mwanaume.
Adamu alikaa miaka mingi bila mwanamke
Mwanaume hata kwenye miaka 60 anaweza oa na kuzalisha watoto.

NIKIJIBU HOJA YAKO,
1.NCHI ZA MAGHARIBI ZOTE, UKIISHA ZEEKA UNAPELEKWA KWENYE VITUO VYA KULELEA WAZEE. HATA HAPA TANZANIA TAYARI VIPO.KUNA KITUO KIKUBWA SANA BAGAMOYO CHA DR.FROLENCE.
2.KUNA HOME NURSING (WAUGUZI WA KUJITEGEMEA WA MAJUMBANI)

#MWANAUME KATAA NDOA KUOKOA UHAI WAKO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…