So kulingana na maelezo yako hapo inamaana umechukulia assumption zifuatazo:
1. Mwanaume lazima awe mgonjwa akifika uzeeni
2. Mwanaume ana mwili mbovu unaochoka haraka kuliko wa mwanamke.
3. Mwanamke hawezi kuumwa akawa mgonjwa wa kutegemea misaada.
4. Mwanaume mzee ni sawa na mtoto mchanga.
5. Jamii humtenga mwanaume anayezeeka.
6. Hakuna taasisi au watu au wasamalia wema wanaweza kumsaidia mwanaume anapofika uzeeni.
So kimsingi umetumia assumptions ambazo zimetokana na mapokeo ya historia za maisha ya wazee wetu kujijibu kuhusu uhalisia wa maisha na kutengeneza matarajio yako kuhusu future ya wanaume wote. HUU NI UBATILI.
1. Unaweza kuwa na mke na familia wakafariki wote kwa ajali au ugonjwa then ukarejea kuwa bila kuwa na mtu. So usiweke guarantee kuwa maisha yako yanakuwa assured sababu upo na mke na watoto ujana wako.
2. Wanawake hutumia survival instinct na techniques kuishi sababu wanajijua hawana uwezo wa kupambana na changamoto za kiasili katika nature. Nitakufafanulia hapa kidogo.
Mwanamke uzuri wake huwa upo kati ya miaka 15 na hauwezi vuka 40 especially akiwa ameshapata watoto mara kadhaa so anajua hakuna mwanaume wa hadhi ya juu na mwenye pesa atamtamani katika umri huo na kutoa pesa na mali zake in exchange for kids and bills zake.
So mwanamke anapambana tokea usichana wake kuhodhi rasilimali ambazo atakuja zitumia baadae akishachuja. Na hili anafanikiwa kwasababu kuna mifumo ameshaimanipulate ili hili lifanikiwe mfano kwenye maswala ya kidini kisheria na kijamii ameweza kutengeneza utaratibu kuwa akiolewa basi watoto na mali za mumewe zote ni mali zote atavihodhi. Ukutaka kujua hili mwambie mkeo unataka muuze kila kitu muhamie sehemu mpya uone roho yake ipo wapi.
So, hii inamfanya mwanamke kuwa makini katika maisha yake ili kupata mali na mwisho kabisa kupata watoto ambao wewe utawasomesha kwa bidii ili waje kumtunza yeye uzeeni wewe ukiwa unapambana na magonjwa kama kisukari, pressure, ukimwi, kansa ambayo ni matokeo ya wewe kutumia takriba miaka 40 ya ujana wako kumhangaikia yeye na watoto wake na kusahau kuwa ukishachoka yeye hakuhitaji tena anachotaka ufe ili usimsumbue na watoto wake aache kula raha wakae kukuuguza.
3. Mwanaume kufika umri mkubwa na kuwa tegemezi kwa mkewe na watoto ni matokeo ya poor planning na resources wastage tokea ujana wote.
Wanaume tunatumia zaidi ya miaka 40 ya ujana wetu pengine na zaidi kuwapambania watu ambao wakisikia tumestaafu tumechakaa hawataweza tuhangaikia kwa miaka hata mitano 5 kabla hawajaanza tuombea tufe maana tunakuwa mzigo wa kudumu kwao jambo ambalo hawapo tayari kulibeba.
Imagine kumhudumia mzee wa kuanzia miaka 60 ambaye hana pesa na anakutegemea kama mtoto utaweza? Miaka 60 akihudumiwa vizuri anaweza fika hata miaka 120 akiwa na nguvu za kutembea mwenyewe na kuongea ni chakula tu na matibabu mazuri. Sasa hii ni kitu ambayo mkeo hatokuwa tayari kuona inatokea maana itabidi mojawapo afe ili watoto au mtoto asiwe na mzigo mkubwa sana wa kuhudumia wazazi wawili ndio maana umri huu akina mama ndio huwa wanaanza kukengeuka na kuwageuka wanaume zao kwa watoto na kuanza figisu za kuwafitini watoto na baba zao ili wao waishi vizuri na ombi kubwa la mwanamke mzee ni mume wake atangulie mbele za haki ili yeye apumzike aishi kwa starehe uzeeni pake.
4. Nikuulize je umeshawahi kuhoji ulaji wako na namna unacheki afya yako katika umri wako huu wa ujana? Jukumu la afya yako si la mkeo wala watoto wako, ni jukumu lako binafsi. Therefore, usitegemee mkeo afanye kazi hii aache kujitazama afya yake kwanza maana yeye anajijali zaidi kuliko wewe.
Ipo hivi mkeo atakupikia chakula ule unenepe asifiwe anamtunza mumewe but nini hutokea kwa mtu anayenenepeana na kujaza mafuta mwilini mwake? Kisukari, pressure, stroke siku za baadae, na mengineyo ni matokeo ya kutozingatia afya na haya huja kutokea uzeeni huko umri wa kuanzia miaka 60+ ndipo haya maradhi huanza kazi.
But wakati wako wa ujana ukiwa makini na life style yako kwenye diet yako yaani chakula gani unakula,umakini na unywaji wa madawa makali hovyo ambayo huchosha figo na ini lako na moyo wako especially viagra, painkillers kali kama ibuprofen,pombe kali kila siku,dawa za nguvu za kiume etc, mazoezi ya mwili, kuwa makini na nani unalala nae kitandani kupunguza risk za magonjwa yatayodhoofisha mwili kupitia madawa ya kuyatibu, namna unapumzika na kulala, unadeal vipi na stress za mahusiano na kuzikomeshaje mfano unaishi na mwanamke anayekusumbua kichwa na si muelewa why upo nae sasa na anakuzeesha mwili na kukuchosha akili piga chini.
5. Unatabia gani za kifedha katika haya maisha yako. Mfano unatumia vipi mapato yako yote hadi ukifika uzeeni ukose hata mia unaanze kulaumu watu kuwa ukiwasaidia au kuwasomesha na wao sasa wanakutenga.
Muda wako wa miaka ya utafutaji yaani kuanzia miaka 10 hadi 50+ itumie kuweka mpango wako wa pembeni ambao haumhusu mkeo wala watoto wako. Mkeo akijua umekwisha maana na kile kidogo atataka kiwe chake na akishakihodhi wewe kwake utakuwa ni threat ambayo atatakiwa kuitokomeza ili akitumie kwa uhuru bila bugudha.
Nyakati hizi ukiishi kwa mifumo ya babu na baba zetu ya kuhudumia bibi na mama zetu kwa asilimia 200% , kisha bado ujitoe kwa ukoo wako na ukoo wa mkeo, then tegemea matokeo yale yale ya kufika miaka 60+ ukiwa hoi na kukosa msaada sababu binadamu hupenda kusaidiwa ila sio kusaidia. Roho yako nzuri iwekeze kwako kwanza kwa 90% then 10% uwekeze nje yako. Nasema hivi kwasababu usijekutegemea kuna mtu atakumbuka huruma zako na kujitoa na yeye ajitoe kwa kadiri ile ile kama yako hiyo sahau.
Imagine ukitumia 90% kwenye mipango yako ya kuwekeza. Sio unapokea mshahara unampa mkeo apange matumizi. Unaokota milioni kumi unampa mkeo apange matumizi, ndugu utakuja juta. Why usiweke mkakati wa biashara ili kuongeza mapato, kuwa na bodaboda, kuwa na bajaji, kuwa na mradi wowote ambao wewe ndie utaratibu kila kitu. Ili pesa yako ianze kukua ukifika by the age 50+ account yako iwe na not less than 400milions in savings na huko mtaani una vitega uchumi ambavyo vipo active. Ukipewa kiinua mgongo chako inakuwa kama ela ya vocha tu.
Hii itakupa maisha marefu na mambo ya kufanya uzeeni na utaishi bila stress za kipato wala kuhangaika na watoto. Wacha watoto wadeal na mama yao maana ndio investment yake. Wewe unafocus na chakula, mazoezi na kuendelea kusimamia baishara zako bila stress. Utaona kama huo umri wa utu uzima ukifika hizi story za sijui nani atakutunza utakutana nazo.
Kuna mengi ambayo tunakosea kama wanaume then tuna assume kuwa ni namna maisha yalivyo au ni nature while si kweli. Ukipanga maisha yako yaende kwa mfumo fulani ndivyo itakuwa hivyo hivyo hadi uzeeni.
So kama utaishi kwa kutapanya kile unachokitafuta kwa jasho la damu then utegemee uzeeni kuna sehemu utapata sapoti then jua unajiandaa kuumia. Mwisho wa siku utajua hujui. Jiandae mapema mazingira ya kustaafu ili uishi kwa starehe baadae sio kuanza kuwaza waza na kupata msongo wa mawazo uzeeni.