Uzeeni mwanaume ana uhitaji wa ndoa zaidi kuliko mwanamke. Chukua hatua

Kikubwa vijana ni kujiwekeza na kutoka kuishi vijijini na miji midogo inayokupresha kuoa
 
Acha ubishi vibabu vilikuwa vibishi kama wewe saizi vinataabika mtaani.
 
Ningekuelewa kama ungetushauri tutafute hela maana hela ikiwepo hakosekani wa kukusaidia shughuli ndogondogo na "kubwa"
Vijana wangu #KATAANDOA
 
huu uzi mkweli,, kuna mzee jirani yangu alikuwa hatofautiani na Ba jesika ujanani ila watoto wamejitegenea kastaafu na madeni ya kusomesha juu saa hiikapoa km kiporo,, mke ndo kwaanza full kushine hadi tunasema alikosa furaha enz zao watoto ndo wanampendezesha..
 
mkuu usiseme sana. Babu yako bado ana nguvu na pia hana changamoto za kiafya. Muda ni muamuzi mzuri. Itafika wakati huyo babu atamkumbuka mkewe licha ya ugomvi wao wa mara kwa mara. Tena hivi umesema watoto na wajukuu kila mtu anaendelea na yake...siku moja mtakuta amejivutia kabinti tena ameoa kabisa ndio utajua naongea nini.
 
Ukishaishi na mwanamke miaka 5 kama sikosei na kukawa na uthibitisho huo, huyo ni mkeo.
 
Vyovyote vile kuwa na ndoa hakumaanishi utakuwa na uzee mzuri..
 
Ni muungano kati ya mwanamke na mwanaume kama mume na mke kuishi pamoja muda wote wa maisha yao.
Ni makubaliano ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja na kushirikiana katika mambo ya kijamii na kiuchumi.

Hiyo kuishi pamoja muda wote mpaka kifo inategemeana na mambo mengine kama dini na makubaliano binafsi. Kuna ndoa za mikataba pia. Ukikosea kuoa ni sahihi kuacha, ila kuwa na ndoa ni Jambo sahihi sana.
 
Nilikuwa nikimtazama mzee wangu, najiuliza hivi bila huyu mama huyu mzee ingekuaje? Watoto wote wapo busy na familia zao. Tukishahakikisha wana chakula ndo basi, sana sana ni simu za mara kwa mara ila mke wake ndo kila kitu kwake.
 
Una nyumba yako, una mali zako, una mke anayekujali kwann uopt kwenda kwenye nyumba za wazee?
 
Mkuu una dada wengi au watoto wengi wa kike.....? [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Unasahau kwamba wengi wenu mlilelewa na wazazi wote wawili.
UONGO.
Huwezi kulelewa na baba na mama halafu ukaona ndoa haina umuhimu. Umeiishi ndoa kupitia wazazi wako, kwann usione umuhimu wake? Unless ni suala la kipato au kukosa mwenza sahihi, na wa hivi hatahubiri ndoa haina umuhimu maana anajua umuhimu wake iwapo una kipato na mwanamke sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…