Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MOROCCAN BREAD ( BATBOUT ) / MIKATE YA MOROCCO ( BATBUT ) : Mahitaji : Unga Hamira Maziwa ya unga Sukari Chumvi Mafuta Kuhusu vipimo inategemea wingi wafamilia yako,kwamfano mm nilipika : Vikombe 3 vya unga wa ngano Hamira kjk cha kulia 1 Maziwa ya unga kjk cha kulia 1 Sukar kijiko cha kulia 1 Chumvi kijiko cha chai 1 Mafuta kiasi Jinsi ya kupika : Changanya vitu vyote kwenye unga.. kisha tia maji kiasi uchanganye unga kama vile unachanganya unga wachapati, kisha kata madonge yaache yaumuke kidogo kisha yasukume kama ya chapati lkn haya uyafanye yawe manene kidogo. Kisha anza kuyapika uyaache yavimbe Yakitokea brown yanapendeza zaidi. ( UNAZIPIKA BILA YA MAFUTA HAZIKAANGWI NA MAFUTA.. CHOMA KWENYE CHUMA CHA CHAPATI BILA YA KUWEKA MAFUTA ZINAIVA BILA YA MAFUTA ) Hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa,enjoy
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 



Humu kuna shule ya
Afya
Saikolojia
Falsafa
Sayansi
Michezo na nyingine nyingi
Naona degree inanukia
 
Leo tunaangalia namna nyingine ya kuandaa tambi. Pishi hili maarufu kama Sphagetti bolognese,ni mchanganyiko wa tambi,nyama ya kusaga na njegere(optional). MAHITAJI: 1. Tambi mfuko mmoja 2. Nyama ya kusaga nusu kilo 3. Nyanya 4 4. Kitunguu swaumu 1 5. Kitunguu maji kikubwa 1 6. Njegere glass ndogo 1 7. Karoti 1 na Hoho 1 8. Chumvi kiasi JINSI YA KUANDAA: -Weka mafuta yachemke,kisha kaanga kitunguu swaumu kilichopondwa pamoja na kitunguu maji,hoho na karoti. -Weka nyama katika mchanganyo huo na ikaange hadi itakapobadilika rangi kuwa ya brown. -Weka tambi zilizochemshwa na njegere. -Koroga kisha ongeza nyanya(ni vizuri zikawa zimesagwa kuliko kukatwakatwa) kisha ongeza maji kidogo. -Funika acha ichemke,kisha weka chumvi. -tayar kwa kuliwa, inaweza kuliwa kama chakula cha wakati wowote,pamoja na kinywaji chochote. Enjoy -
 
TAMBI ZA DENGU Mahitaji : Unga wa dengu kilo 1 Chumvi kiasi Pilipili manga kiasi Pilipili ya unga kiasi Manjano kijiko 1 cha chai Baking soda 1/2 kijiko cha chai Mafuta ya kula kikombe 1 Maji vugu vugu kiasi cha kukandia NAMNA YA KUTAYARISHA: 1. Changanya vitu vikavu vyote vizuri katika bakuli, tia mafuta kisha changanya tena ufanye chenga. 2. Anza kutia maji taratibu hadi upate unga mlaini, paka mikono yako mafuta kisha kanda unga kwa muda wa dk 5 3. Funika na uache ukae kwa muda muda wa dk 10. Bandika mafuta jikoni juu ya moto wa kiasi 4. Utie unga wako katika mashine ya tambi kisha binya taratibu kuruhusu tambi kutoka na kudondoka kama mvua katika mafuta ya moto kisha taratibu zungusha mzunguko mmoja na acha ziive na kupata rangi pande zote mbili (angalia picha katika comments) 5. Epua katika chujio zichuje mafuta, rudia utaratibu kwa unga wote. Taratibu zivunje vunje na tambi zako zitakuwa tayari kwa kula. Enjoy!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…