Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Nimecheka Mpaka wananishangaa
Mzee wa liver

CantstopwontStop
Hahahahaha acha ndio mambo ya likes
 
0330b42089ee651e59bff9319bf4f3cb.jpg
 
Kashata za maziwa mazito (condensed milk. 1. vikopo 2 maziwa mazito sona 2.kikombe 1 cha chai sukari 3.nazi fresh ilokunwa vikombe chai 2 4.ufuta ulokwisha kaanga nusu kikombe 5.blue band vijiko vya mezani 2 6.vanila vijiko vya chai 2 *Changanya vitu vyote uweke kwenye sufuria isipokua Ufuta na Nazi.hivi unaweka mwisho wakati mchanganyiko wako unapoanza kuwa mzito wakati unakoroga. Ukishachanganya vitu nilokutajia koroga taratibu ukiwa unatumia Moto mdogo. Koroga mpaka mchanganyiko unakuwa mzito ndio weka Ufuta na Nazi.endelea kukoroga mpaka Rangi inapobadilika kuwa brown. Paka sinia mafuta kisha mwagia mchanganyiko wako.weka upoe kisha kata shepu utakayo. Yaani hizi Hazina tofauti na tofi. Enjoy -
 
Maandazi sidhani kama kuna mtu hayapendi.lugha nyingine watu huita Mahamri. Kipimo nilichotumia ni hiki. .Kg 1 unga Wa Bakhresa PPF .Hamira kijiko cha mezani 1 (tbspn) .Baking powder robo kijiko cha Chai.hata ile iloandikwa chapa mandashi in sawa. .Mafuta mepesi vijiko Vya mezani 5 .Sukari weka kikombe kimoja cha Chai usijaze sana.ninavyosema kikombe cha Chai no kila cha kawaida huja na kisahani chake.sio mug. Weka hiliki ilosagwa kijiko 1 cha Chai.ukipenda weka vanilla nusu kijiko.angalia vanilla ukizidisha huleta uchungu.
 
Namna ya kufanya. Chukua unga chekecha,weka kwenye bakuli,tia sukari,hamira,baking powder,hiliki changanya vizuri.kisha weka Mafuta pikicha vizuri,weka Maji glasi 1 ya kawaida ulotia vanilla ndani.anza Maji weka kati ya unga kidogo kidogo,ule unga unaopata Maji weka pembeni.kisha ukande wote kwa pamoja,kama Maji yatapungua ongeza kidogo.unga usiwe mgumu na usiwe mtepe uwe Wa kawaida. Kata madonge 5 weka duara nzuri.kisha sukuma usiwe mwembamba mduara wako.halafu kata Mara 4 .ina maana ukimaliza hapo utakuwa na maandazi 20. Weka sinia nyunyizia unga panga Mandazi na ngoja yaumuke yavimbe.ukitaka kujua kama andazi limeumuka,libebe,kama jepesi basi litakuwa tayari kuchomwa.na kama ni zito basi subiri liumuke. Unapotenga karai La Mafuta kabla hujatia andazi,kwanza tupia kipande kidogo cha andazi kuona kama Mafuta yapo tayari kuchoma maandazi yako.Mafuta yakiwa ya moto sana maandazi usiyaweke ujue yatatoa vipelevipele.ukiweka Mafuta kama hayajachemka ujue maandazi yako yatanyonya Mafuta.yawe ya moto Wa kawaida.
 
Vitu vinavyo Fanya Nyama iwe laini katoka kuiunga. 1.Tangawizi fresh 2.papai bichi 3.majani ya chai 4.mtindi. 5.tunda liitwalo kiwi. Sina maana uvitie vyote kwa pamoja.hii nimekupa mfano ukiwa utakosa hiki weka kile. Utakacho chagua hapo hakikisha umesaga na ndio uweke kwenye mchanganyiko wa Nyama yako. Nyama haitaki makorokoro kuipata ladha yake. -
 
Usizigeuze changamoto za ofisi kuwa matatizo. Hii itakupelekea kuwa na msongo wa mawazo unaotokana na changamoto za ofisi husika.

Kila linalozungumzwa kuhusu kazi ni muhimu sana kwani ukiteleza kupitia hilo litakuletea matatizo ambayo yanaweza kuanza kidogo na kulipuka kuwa chanzo cha msongo wa mawazo kwa kuhisi unasakamwa ofisini.

Jifunze kusikiliza zaidi ya kuongea,tafakari ulichosikia na uliza swali kujiridhisha kile ulichoelekezwa ili mambo yako yaende sio tu kwa sababu umeambiwa ufanye bali ulichoambiwa na matokeo yanayotarajiwa.

Hii itakusaidia pia kujenga uhusiano mzuri kati yako na wafanyakazi wenzako na mwisho kuunda urafiki zaidi ya uadui.

Kuwa na mtazamo chanya
Kuwa na mtazamo chanya juu ya mambo yanayoendelea ofisini. Usichukulie kila unachoambiwa na usichokipenda kuwa ni sehemu ya tatizo na manyanyaso kwako.

Ichukulie kwa mtazamo chanya, unapovuka kikwazo ndio chanzo cha kuongeza uaminifu zaidi kwa wakuu wako wa kazi.

Kumbuka, huwezi kuitwa bora kwa njia ya mteremko tu, ubora wako hupimwa pia na namna unavyozikabili changamoto zako ofisini.
 
Vitunguu vina faida nyingi. Leo tutazungumzia vitunguu licha ya kuwa kiungo kizuri kwenye Chakula,vitunguu kinga Kubwa kwenye Chakula chako ikiwa kwa bahati mbaya umezidisha chumvi kwenye Chakula,basi chukua kitunguu kimoja kikubwa menya na weka ndani ya Chakula kilozidi chumvi.basi utastaajabu hicho vitunguu kitakavyo nyonya hiyo chumvi. -
 
Back
Top Bottom