Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Msongo mkubwa wa mawazo;
nguvu za kiume na hamu ya kushiriki tendo hili huanzia kichwani mpaka kwenye uume wa binadamu, watu wenye misongo ya mawazo sababu ya kushindwa kutimiza wajibu wao wa kazi waliopewa kwa wakati, misongo ya mawazo sababu ya majukumu makubwa ya kifamilia ambayo yanakuja na huenda hakuna fedha za kukabiliana na hali hizo, msongo wa mawazo wa biashara zinazoyumba humfanya mwanaume asiweze kushiriki kabisa tendo la ndoa... omba msaada kama kazi zimekuzidi tafuta msaidizi kama umeajiajiri, kama waliokuajiri hawakuelewi tafuta kazi nyingine na uachane na hiyo kazi ya kufanya kazi usiku mpaka usiku lakini pia muda wa kazi ukiisha undoka kwenda nyumbani haraka kwenda nyumbani hakuna sifa ya kufanya kazi masaa mengi wakati mahusiano yako yanakufa.watu wanaofanya kazi benki ni wahanga sana wa matatizo haya.
 
Wadada sio kila neno mnaongea kwa pozi
Kwenye gari leo wakati natoka Mbagala naelekea Gomz, kuna mdada alikuwa anaongea simu sasa hiyo Gongo la mboto alivyoitamka watu wote walimgeukia, naomba ninukuu "Enhe ndio nipo kwenye gari naelekea Gongo la mb.o.o.o.to"
 
Ulevi wa kupindukia;
unaweza kua unapenda kunywa pombe angalau kustarehe na kuonana na ndugu na jamaa lakini unywaji wa pombe kupitiliza ni hatari sana, humaliza nguvu za kiume na kukosesha hamu. habari njema ni kwamba pombe kidogo angalau pia moja mpaka mbili kwa siku ni nzuri kwa nguvu za kiume na afya ya moyo.
 
e3279e4a7dc1a86718de3810ffee6f43.jpg
[emoji23] [emoji23] [emoji23] ngoja nijaribu

Umeamkaje bebi? Za jumapili?
 
Dawa mbalimbali;
baadhi ya dawa zinzotumika kwa shida mbalimbali au magonjwa mbalimbali zimethibitika kupunguza nguvu za kiume hasa zile zinazomezwa mara kwa mara au kila siku mfano dawa za presha, dawa za maumivu na dawa za msongo wa mawazo.

kumbuka usiache dawa kama una ugonjwa unaohitaji dawa kila siku sababu umesoma hapa, kwa upande mwingine uhai unaweza kua muhimu kuliko nguvu za kiume.
 
kufikiria sana;
huwezi kupata nguvu za kiume kama unafikiria mambo mengi yanayokuathiri labda maumivu ya vifo ya wapendwa, maumivu ya kuachishwa kazi, maumivu ya kusalitiwa na mpenzi au kuachwa, na uchovu sana wa shughuli za kila siku. jaribu kurelax, kukubali matokeo, kupata usingizi wa kutosha na kushiriki mazoezi na kumbuka mazoezi yakiwa makali sana humaliza nguvu za kiume.
 
Wasiwasi;
wanaume wakishapata matukio kadhaa ya kuadhirika na kushindwa kufanya tendo la ndoa huanza kuogopa kukutana tena na mwanamke kwa hofu kwamba wataadhirika tena...tafuta chanzo ni nini na urekibishe, huenda siku hiyo haukua vizuri au ulikua na njaa...kisha jiamini kwamba sasa ntafanikisha.
 
Vitambi na unene;
vijana wengi kwanzia miaka 30 mpaka 40 hilo ndio tatizo lao kubwa, yaani kukosa nidhamu ya kupambana na ungezeko la miili yao na matokeo yake uume hua mdogo na nguvu kidogo sana lakini pia ulaji wa vyakula vya haraka kama chips na mikaango mbalimbali wakati wa kazi na kusahau vyakula asilia kama mihogo,karanga, ugali,wali, matunda na mboga za majani...asikudanganye mtu kama umeshindwa kupungua uzito nguvu za kiume utazisikia redioni.
 
kutojiamini;
baadhi ya wanaume hushindwa kujiamini kwa kujikosoa vitu mbalimbali vilivyoko kwenye miili yao ambavyo wakati mwingine hata mwanamke mwenyewe havijali sana mfano kuhisi ana uume mdogo sana wakati uume wake ni wa kawaida, kuhisi hana mwili mzuri na kadhalika.
 
Back
Top Bottom