Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

3.Ntapata vipi kazi Tanzania?
Wajua Tatizo linakuwa wapi? Mtu anaishi Marekani, amesoma, anataka kurudi nyumbani apate kazi, akiangalia kwenye mtandao anakuta kazi zinatangazwa, anaziweza vizuri, lakini zinahitaji uzoefu miaka mitatu, Ndio anao uzoefu kazini, lakini kazi aliyokuwa anafanya ni kutengeneza bustani! No hawataweza kuniajiri, Ngoja nibaki hukuhuku labda maisha yataendelea vizuri!.
 
4.Sitaki Kuishi kwa wazazi wangu, Nina Familia, Ntawezaje Kupata Nyumba nyingine?
Kuna Idadi kubwa ya watu wanaoishi na familia zao nchini Marekani, wana watoto kule, na wameshazoea kuishi hivyo. Maisha yanapokuwa magumu, inakuwa ngumu kwa wao kurudi tena nyumbani. Suala la kusafirisha familia ni gumu, pia mahali pa kukaa ni tatizo linguine kwani kwa sasa huwezi tena kuishi na wazazi wako.
 
4.Sitaki Kuishi kwa wazazi wangu, Nina Familia, Ntawezaje Kupata Nyumba nyingine?
Kuna Idadi kubwa ya watu wanaoishi na familia zao nchini Marekani, wana watoto kule, na wameshazoea kuishi hivyo. Maisha yanapokuwa magumu, inakuwa ngumu kwa wao kurudi tena nyumbani. Suala la kusafirisha familia ni gumu, pia mahali pa kukaa ni tatizo linguine kwani kwa sasa huwezi tena kuishi na wazazi wako.
 
Ntaweza Kufanya Kazi ninazozifanya nikirudi nyumbani? Au Kuna Kazi zinazohusiana na hiki nilichosomea?
Mazingira ya kazi katika nchi za Magharibi ni tofauti kabisa na afrika. mathalani, Mtu amesomea uokozi (lifeguard) na kuna kazi zinapatikana Huko, Tatizo linakuja kwamba, Kiafrika, suala la kujiokoa na usalama wako uko mikononi mwako kwa asilimia 99 (99%) hivyo kumuajiri mtu aliyesomea kuokoa watu kwetu ni matumizi mabaya ya fedha. Hili pia ndio sababu inayomfanya mtu aone ni bora abaki ugenini japo maisha ni Magumu.
 
Ntapata Shule nzuri kwa ajili ya wanangu? Na je watazoea kuishi Tanzania?
Hii huwa sehemu ngumu zaidi kwa wenzetu hasa ikishafika kipindi kwamba maisha ni magumu, hawawezi kuendelea kukaa ugenini lakini je, watoto watasoma shule gani? Na wameshazoea maisha ya kimagharibi, sasa je watafurahia kuishi ugenini?.
 
Ninampenzi wa huku, atakubali nirudi nae nyumbani?
Hapa ndipo penye shida, Hata kama atakubali, je wazazi wake watamkubali mpenzi wake huyo asiyejua mila na tamaduni za nyumbani? Hivyo ili kumfurahisha mpenzi wake, huona bora aendelee kukaa ugenini hata kama maisha yake ni magumu.
 
Nimeshakuwa “Mzungu” Siwezi tena “uswahili”. Ntapata wapi bima za afya nk?
Kuna aina mbili za Ubaguzi, ubaguzi wa kuzaliwa nao, na ubaguzi wa kuurithi/kujifunza, Huu ubaguzi wa kurithi ndio unawapata sana ndugu zetu walio nchi za magharibi, na wana kipato kizuri. Kwanza wanasafiri kwenda nje, baadae wanasahau yote ya nyumbani na licha ya “uweusi” wao wanaanza kujiona wao ni wazungu na hawawezi tena kuishi maisha bila baadhi ya vitu na kusahau kabisa nyumbani.
 
Nyumbani Kila Kitu Ni siasa na Kujuana!
Kuna Watanzania Wengi sana wanaotamani warudi nyumbani kuanzisha biashara au miradi mbalimbali lakini wanakumbuka kuwa ili kufanya chochote nyumbani lazima ujuane na watu Fulani, au “uwaone” watu Fulani la sivyo hakuna utakachoweza kufanya.
 
Back
Top Bottom