Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kama tujuavyo mitandao ya kijamii inamruhusu mtumiaji wake kuandika na ku-post chochote anachotaka kama vile ujumbe, picha na video bila kujali vitu hivyo vina maadili au havina maadili. Mfano unaweza kupost picha au video za ngono au kumdhalilisha mtu mwingine.
 
Na kila kinachoonekana kuchapishwa (posted) kwenye account/ profile yako ya mtandao wa kijamii kama vile facebook n.k kinaaminika kuwa kimewekwa na wewe mmiliki wa account/ profile hiyo.
 
Madhara ya mtu mbaya kuingia kwenye profile/ account yako ya mitandao ya kijamii;
Taarifa zako zote za siri zilizopo kwenye profile ya mtandao huo wa kijamii zitajulikana na pengine kuweza kutumiwa vibaya na mtu huyo mbaya.
 
Mtu huyo mbaya anaweza kutuma ujumbe mbaya kwa marafiki au watu wako wengine wa karibu uliojiunga nao kwenye huo mtandao wa kijamii kama vile Facebook n.k. Mfano anaweza kutuma ujumbe wa kuwatusi au kutoa maneno ya vitisho na itaonekana kuwa wewe ndiye uliyetuma.
 
Mtu huyo mbaya anaweza kuchapisha (post) vitu visivyofaa kwenye wall (timeline) ya account/ profile yako. mfano anaweza ku-post maneno, picha au videos za uchochezi, matusi, kukashifu au kudhalilisha mtu au watu wengine.
 
Kama post zilizowekwa kwenye profile yako zitakuwa ni za mambo ya kudhalilisha kama vile picha au videos za ngono, basi tarajia hata kama ulikuwa na heshima na ustaarabu kiasi gani, marafiki na watu wengine waungwana na wastaarabu watakaoziona watakushusha thamani na kukudharau. Utaonekana huna maana kwa sababu pia na video za ngono zina mahali pake na sio ku-post ovyo hadharani kwenye mitandao ya kijamii.
 
Lakini hebu sasa piga picha au kufikiria nini kitakutokea endapo kwenye profile/ account yako ya mtandao wa kijamii kama Facebook, Twitter, Instagram, Linkedin n.k kutaonekana post ya maneno, picha au video inayomdhalilisha kiongozi yeyote wa nchi kama vile Rais, Waziri mkuu n.k, au ni post ya uchochezi wa kuvunja amani. Hakika utaingia kwenye matatizo makubwa na vyombo vya usalama kumbe sio wewe uliyepost. Hata kama utajitetea haitokuwa rahisi kukuamini kuwa sio wewe kwa sababu wewe ndio mwenye profile hiyo.
 
Kwa hiyo ili kuepuka watu wengine wasiweze kuingia kwenye account/ profile yako ya mtandao wowote wa kijamii jitahidi kutunza password yako kwa usiri na umakini mkubwa mtu mwingine asiifahamu na pia jitahidi ku-log out kila wakati unapotoka kwenye profile yako baada ya kumaliza mambo yako. Fanya hivyo bila kujali unatumia simu au computer yako binafsi, simu au computer ya kuazima kwa mtu au computer za public yaani kwenye internet cafe, vyuoni, maofisini, n.k
 
Jamani nimeamua kuandika post Madhara/ hasara za kutoka kwenye facebook na mitandao mingine ya kijamii bila ku-log out hii ili kuwatahadharisha na kuwakumbusha watumiaji wa mitandao ya kijamii kuhusu umuhimu wa kuwa makini katika kulinda usalama na matumizi ya mitandao hii ya kijamii. Ni vizuri kutumia mitandao ya kijamii kwa sababu ina faida zake, lakini ni vizuri zaidi kuhakikisha hatutumii vibaya mitandao hii kama vile kupost matusi, kudhalilisha wengine, kuchafua status za wengine au kuweka jumbe za uchochezi zinazoweza kuhatarisha usalama na amani.
 
Back
Top Bottom