Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Shetani lengo lake ni kutawala dunia. Huwezi kutawala dunia bila elimu!

Shetani anajua kwamba sisi ni warithi wa wokovu na kwamba dunia hii ni kitu kilichoahidiwa kwa Ibrahimu na watoto wake. Sisi wote ni watoto wa Ibrahimu. Anajua kabisa kwamba baadaye sisi ndiyo tutakaokuwa watawala halisi wa dunia hii. Hivyo, anajitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote ili hilo lisitokee. Shetani na malaika wake ni wengi sana, na wanatumia kila silaha waliyokuwa nayo kutawala dunia.
 
Kuna elimu ya kidunia na kuna elimu ya kidini. Huwezi kutawala dunia bila elimu ya kidunia, kwa sababu Shetani anajua ukiipata elimu hiyo hutajua kama yupo; na huwezi kutawala dunia bila elimu ya kidini, kwa sababu Mungu anajua ukiipata elimu hiyo utajua kama yupo. Hivyo, utamdharau Mungu ukipata elimu ya kidunia, utamheshimu Mungu ukipata elimu ya kidini.
 
Kama Shetani anatumia elimu kutawala dunia kama vile Mungu anavyotumia elimu kutawala dunia, nani alisema kuwa baadhi ya wasanii wa ‘Bongo Movie’ na ‘Bongo Flava’ ni wanachama wa chama cha siri cha kusaidiana cha wajenzi huru? Je, wana elimu? Jibu unalo.

Anayesema fulani ni mwanachama wa chama cha siri cha kusaidiana cha wajenzi huru ana hakika? Haya mambo ni siri. Amejuaje? Kumbuka, usiamini, jua.
 
Kama wana elimu wanaweza kuwa wajenzi huru; lakini kama hawana elimu, hawawezi kuwa wajenzi huru.

Shetani ni mjanja sana. Anajua bila elimu hataweza kutawala dunia, baada ya mpango wa Mungu kukamilika. Anajua, mtu akipata elimu ni rahisi sana kujua kama Shetani hayupo. Hivyo Shetani atatimiza malengo yake bila watu kujua.
 
Mungu hatakubali kuwa na mtu katika ufalme wake ambaye hatakubali kutawaliwa naye. Usikubali kutawaliwa na Ibilisi, kubali kutawaliwa na Mungu. Ni jukumu letu kuanza kuishi sasa kama vile tutakavyoishi mbinguni. Shetani anataka uwe na hekima ya duniani ili akupumbaze. Lakini hofu ya Mungu ndiyo msingi wa hekima ya kweli. Ukitaka asikupumbaze, pokea roho ya Mungu kwa kubatizwa. Ukiipokea roho ya Mungu utajua mambo ya Mungu, ambayo dunia haiwezi kujua.
 
Wengi katika dunia hii hawajui kama wanadanganywa au walishadanganywa tayari. Shetani hataki tujue kama anatudanganya au ameshatudanganya tayari, na hataki tujue kama yuko hapa kwa ajili ya kutudanganya sisi. Tunajua tu kwa sababu Neno la Mungu hudhihirisha ukweli huu kupitia Roho Mtakatifu na malaika wema, na tunauamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…