Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hyperion tree' mti unaotajwa kuwa mrefu zaidi duniani, haujulikani eneo sahihi ambalo upo kwaajili ya kuulinda dhidi ya uharibifu wowote ambao unaweza kufanyika japo inasemekana upo katika moja ya misitu huko California. Una urefu wa mita 115 .85
images (3).jpeg
 
Katika uso kuna eneo ambalo hutakiwi kuminya chunusi. Hupatikana kati ya pua na mdomo, huitwa Pembetatu ya hatari. Mishipa ya damu eneo hili ina muungano na mishipa ya kwenye ubongo hivyo ukiminya chunusi unaweza safirisha maambukizi hadi kwenye ubongo.

Sasa kwenye mdomo ukiminya chunusi, domo sii litavimba kama umeng'atwa na nyuki...



Cc: mahondaw
 
"Watafiti wanadai mtoto aliyetumboni huanza kusikia sauti za nje akiwa na umri wa wiki 25, hivyo wazazi wanapaswa kuepuka kelele kupitiliza ili mtoto akue vizuri," Dr Mabula
Pia wanasema ndo kipindi ambacho mzazi anatakiwa aanze kumuongelesha mtoto aliyetumboni,hii huchangia kujenga mapenzi kati ya mzazi na mtoto pindi atakapo zaliwa
 
Pomboo (Dolphins), ni wanyama pekee wanaopeana majina wenyewe, kama binadamu. Wanasayansi wanasema kuwa samaki hao wanaitana kwa kutoa sauti fulani kama mluzi ambapo kila mmoja huitikia kila anaposikia sauti fulani ambayo ni kwa ajili yake pekee. (National Geographic)
 
Back
Top Bottom