Tetesi: Uzi maalumu wa tetesi mbalimbali za usajili kuelekea msimu mpya wa ligi 2023/24
Hivi hii singida big stars iliyouzwa na kubadilishwa jina kuwa singida fountain gate itaendelea kusajili wachezaji mahiri wa gharama kubwa au ndio mwanzo na mwisho wake? Hao fountain gate wana uwezo gani wa kufanya usajili wa maana au ni abrakadabra tu timu ijifie zake kimyakimya?
Soon itakuwa Mtibwa isiyolima miwa.
 
Tetesi : Inaelezwa kwamba Beki Wa Pembeni Wa Simba Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amekubali kusaini dili la miaka mitatu kwa kupewa Shillingi 300 milioni na mshahara wa Shillingi 10 milioni.

Ofa aliyopewa na Kaizer Chiefs dau la Shillingi 200m na mshahara wa Shilingi 20m kwa mwezi imebuma baada ya mabosi wa Simba kupambana na kumalizana na beki huyo.
Duuuuh so huyu jamaa kaona milioni 660 ni Bora Bora kuliko milioni 920
 
Helmy Gueldich(kocha wa viungo Yanga) kutimkia Afrika kusini kwenye klabu ya Orlando Pirates au Kaizer Chiefs
 
1687762658225.png

ANGA inawasiliana ili kumsaini Zougrana(21,🇮🇪)!

Young Africans sasa wanaendelea na mazungumzo ya kumsajili Mo Zougrana baada ya kumuongezea mkataba Sure Boy 🚨

- Mazungumzo yanaendelea sasa kutafuta ‘muundo’ sahihi wa dili hilo huku Yanga wakisukumana tangu jana kumsajili Zougrana.🔰

- Yanga sasa wanajiamini kufikia makubaliano katika siku chache zijazo 🇮🇪
🚨Elewa:::: Yanga wanasukuma kukamilisha Dili hili ndani ya wiki hii

- Msukumo wa Aziz Ki kutaka Zougrana awe Yanga na bodi inajitahidi kufikia makubaliano haraka iwezekanavyo. ⌛️
 
1687762753359.png

Hakuna kilichobadilika, kama nilivyoripoti hapo awali kwamba Malone amekubali na yuko tayari kujiunga na kilabu

Cotton Sports pia ilikubali zabuni ya nne ya Simba ya karibu $275k

Malone alitarajiwa kuwa Tanzania wiki hii lakini Salim Abdalah atasafiri kwenda Cameroon kukamilisha dili hili

Wiki ijayo Klabu ya Simba inatarajiwa kukamilisha dili mbili MALONE& SYLLA kama watakubaliana katika masharti binafsi na kiungo huyu
 
1687762831158.png

Rasmi, imethibitishwa

Denis Kibu(🇹🇿,24) ameongeza mkataba na Simba sc kwa msimu mmoja zaidi. 🦁⭐️ #SimbaSc

Mazungumzo yalikuwa ya haraka sana kwani alitaka tu kubaki - mkataba mpya hadi Juni 2025.

🚨Fahamu
Mkataba wa sasa wa Kibu unaisha Juni 2024
 
View attachment 2669109

ANGA inawasiliana ili kumsaini Zougrana(21,🇮🇪)!

Young Africans sasa wanaendelea na mazungumzo ya kumsajili Mo Zougrana baada ya kumuongezea mkataba Sure Boy 🚨

- Mazungumzo yanaendelea sasa kutafuta ‘muundo’ sahihi wa dili hilo huku Yanga wakisukumana tangu jana kumsajili Zougrana.🔰

- Yanga sasa wanajiamini kufikia makubaliano katika siku chache zijazo 🇮🇪
🚨Elewa:::: Yanga wanasukuma kukamilisha Dili hili ndani ya wiki hii

- Msukumo wa Aziz Ki kutaka Zougrana awe Yanga na bodi inajitahidi kufikia makubaliano haraka iwezekanavyo. ⌛️
Yanga kumbe wana bodi
 
1687785340496.png

TETESI ZA USAJILI | Beki wa kushoto Yahaya Mbegu kupitia ukurasa wake wa instagram amechapicha ujumbe wa kuishukuru Ihefu “THANK YOU Mbogo Maji.”

Mbegu anahusishwa kujiunga na Simba kuchukua nafasi ya Gardiel Michael ambaye mkataba wake na Simba umemalizika na ameruhusiwa kuondoka.

Mbegu amekuwa kwenye kiwango kizuri tangu alipokuwa Polisi Tanzania, Geita Gold na Ihefu.

Singida Fountain Gate FC pia inatajwa kuwa kwenye mbio za kuwania saini ya mchezaji huyo aliyewahi kupita timu ya vijana ya Simba.
 
Back
Top Bottom