Tetesi: Uzi maalumu wa tetesi mbalimbali za usajili kuelekea msimu mpya wa ligi 2023/24
Huku tunapoelekea nyumba ya jirani inazidi kubomoka, bila shaka baada ya azam kuachana na Ongala tutegemee taarifa yoyote kuanzia sasa katika viunga vya azam maana nawaona msimu huu wanataka kuvunja benki.
 
#EXLUSIVE||; [emoji599] Klabu Ya Young Africans Huenda Ikatangaza Kuachana Na Kocha Wao Wa Viungo Helmy Gueldich, Kocha Huyo Ambaye Amehudumu Young Africans Zaidi Ya Miaka Miwili Anahitaji Kwenda Kutafuta Changamoto Sehemu Nyingine.

Nimuwendelezo Wa Young Africans Kuendelea Kupoteza Watu Wao Muhimu Kwenye Benchi La Ufundi.

1.. Kocha Mkuu Tayari Amesha Agwa.
2.. Kocha Wa Magolikipa Naye Ameshaagwa.
View attachment 2659533
Ndio maisha ya football hayo ila kwa mashabiki wa bongo linaonekana jambo la ajabu! Hata iweje wangeondoka tu hakuna mkataba wa milele
 
Hivi hii singida big stars iliyouzwa na kubadilishwa jina kuwa singida fountain gate itaendelea kusajili wachezaji mahiri wa gharama kubwa au ndio mwanzo na mwisho wake? Hao fountain gate wana uwezo gani wa kufanya usajili wa maana au ni abrakadabra tu timu ijifie zake kimyakimya?
 

1686915174124.png

JOASH ONYANGO UPDATE.

Baada ya tetesi za mda mrefu sasa nipo hapa kukuthibitishia kuwa beki kisiki wa Simba Joashi Onyango hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba msimu ujao baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Klabu ya Simba inaendelea na maboresho ya kikosi chake kwa kuondoa baadhi ya wachezaji ambao wanaamini hawatakua na msaada kwa msimu ujao huku timu ya Usajili ikiwa busy kutafta wachezaji wakubwa ili kurejesha makombe yote Msimbazi msimu ujao.

Mda wowote Simba itawatangaza wachezaji wote ambao imeachana nao huku kukiwa na mvutano wa mchezaji mmoja ambae ni kipenzi cha viongozi na mashabiki ila kocha anahitaji aletewe mchezaji mwingine ( anasema ni machachari na sio hatari
 

1686915280677.png

MILTON KARISA UPDATE
Mazungumzo kati ya Mshambuliaji wa Vipers, Milton Karisa yamefikia hatua nzuri hadi sasa kwa mchezaji huyo kujiunga na Simba kwa ajili ya msimu mpya.

Milton Karisa huenda akasaini mkataba wa miaka miwili ikiwa ni mapendekezo ya kocha mkuu wa Simba, Robertinho kwa ajili ya msimu mpya wa mashindano.

Mshambuliaji wa Vipers, Milton Karisa ameeleza nia ya kutaka kujiunga na Simba kwa ajili ya msimu mpya na inasemekana ndiye mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Simba.
 
Aliyewahi kuwa kocha wa Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini na Al ahly ya Misri, Pitso Mosimane ameripotiwa na gazeti maarufu la Afrika kusini IOL kuwa yuko mbioni kujiunga na Wakali hao wa Tanzania, Young Africans club.

Kocha huyo ambaye hivi karibuni ametoka kuvunja mkataba wake na timu ya Saudi Arabia, Al Hilal ameoneka Mjini Johanesburg akiwa na Eng Hersi katika mazungumzo.

Hata hivyo tangu Kocha huyo awe huru, timu nyingi zimejitokeza kuwania sahihi yake ikiwemo pia Klabu ya Kaizer Chiefs, ambao pia wameripotiwa kuwa katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa Nabi Nasreddine

Yanga ambao wametoka kuagana na Kocha wake Nabi, wako busy kuhakikisha nafasi hiyo inajazwa haraka iwezekanavyo.

Pia gazeti la Pulse Sports Nairobi, Kenya limeripoti juu ya uwezekano huo wa Pitso kutua Jangwani.
 
Back
Top Bottom