Tetesi: Uzi maalumu wa tetesi mbalimbali za usajili kuelekea msimu mpya wa ligi 2023/24

Inadaiwa kuwa Nabi anaweza kuondoka Yanga mwishoni mwa msimu huu

Nabi alishapewa kishika uchumba na team moja kubwa barani Africa hivyo mda wowote kuanzia sasa anaweza kusepa

Yanga wanapaswa kuanza mpango mwingne wakutafuta coach

Wananchi hapo vipi 👀
Hiyo timu kubwa Africa ni SIMBA SPORTS CLUB ya Msimbazi Kkoo. Lazima Nabi asajiliwe Simba.
 
1685511431722.png


Southampton na Middlesbrough wanamuwinda Novatus Dismas
Licha ya Klabu yake Zulte Waregem kushuka daraja huko Ubelgiji, kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Novatus Dismas ameziingiza vitani Southampton na Middlesbrough za England kupigania saini yake.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na timu hiyo msimu uliopita wa kiangazi akitokea Israel 🇮🇱 ambako alikuwa akiichezea Maccabi Tel Aviv na kuwashangaza wengi kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi.

Akiwa na Zulte Waregem, Novatus ametumika kama beki wa kati, kushoto, winga na kiungo mkabaji nafasi ambayo Watanzania wengi wamemwona akicheza tangu akiwa kwa mkopo Biashara United ya Mara.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Ubelgiji, Southampton iliyoshuka daraja Ligi Kuu England (EPL) ndio inayoongoza vita hiyo huku wakifuatiwa na Middlesbrough ya Daraja la Kwanza ‘EFL Championship’ na ipo tayari kutoa Euro 850k (Sh 2.2 bilioni).
 

1685511619037.png

Tetesi : Inaelezwa kwamba Beki Wa Pembeni Wa Simba Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amekubali kusaini dili la miaka mitatu kwa kupewa Shillingi 300 milioni na mshahara wa Shillingi 10 milioni.

Ofa aliyopewa na Kaizer Chiefs dau la Shillingi 200m na mshahara wa Shilingi 20m kwa mwezi imebuma baada ya mabosi wa Simba kupambana na kumalizana na beki huyo.
 
Tetesi: Kocha la Boli Luis Enrique kutua Napoli

1685511899152.png
Mabingwa wapya ligi kuu Italia, Napoli wapo kwenye mazungumzo na kocha wa zamani wa timu ya Taifa Uhispania, Luis Enrique kwa ajili ya uwezekano wa kuwa kocha mkuu klabuni hapo.

Enrique (53) raia wa Uhispania anatazamwa na Napoli kama mrithi namba moja wa Luciano Spalletti ambaye ameamua kuondoka klabuni hapo licha ya kuiongoza Naples kutwaa ubingwa wa Serie A.
 
1685535751097.png

AUBIN KRAMO raia wa Ivory Coast anahusishwa na kutua katika klabu ya Simba.

Nyota huyo akiwa na Asec Mimosas katika Mashindano ya Kimataifa msimu huu.

⭐️ CAFCL
🏟 4 mechi
⚽️ 3 mabao
.
🌟 CAFCC
🏟 12 mechi
⚽️ 04 mabao

Vipi wanasimba atawafaa?
 
Liverpool wako kwenye mazungumzo na kiungo wa kati wa Argentina Alexis Mac Allister, 24, kuhusu maslahi binafsi na wanatarajia kukamilisha usajili wake kutoka Brighton wiki ijayo. (Fabrizio Romano)
 
Joao Felix atapelekwa Newcastle kwa mkopo na klabu mama Atletico Madrid siku chache tu baada ya Chelsea kutangaza kutomsajili mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 23 kwa uhamisho wa kudumu. (Mail)
 
Nahodha wa England Harry Kane, 29, anataka kuhamia Manchester United msimu huu wa joto, badala ya kuhamia nje ya nchi, lakini yuko tayari kumaliza mkataba wake na kuondoka Tottenham kama mchezaji huru mwaka ujao. (Sun)
 
Nahodha wa England Harry Kane, 29, anataka kuhamia Manchester United msimu huu wa joto, badala ya kuhamia nje ya nchi, lakini yuko tayari kumaliza mkataba wake na kuondoka Tottenham kama mchezaji huru mwaka ujao. (Sun)
Aisee dogo huyu amekuja kuwaje sijui. Mwanzoni alitabiliwa makubwa
 
Juventus wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Mmarekani Christian Pulisic, 24, kwa mkataba wa $25m (£20.1m). (Mail)
 
Back
Top Bottom