Wazo zuri sana, kazi kwao kwa wahusikaMkuu, hivi Hostel za UDOM huwa inawezekana wanaruhusu watu wa Saili kulala?
Kuna wazo hapa limenijia, hivi kwanini Chuo Kikuu UDOM kisingeanzisha utaratibu maalumu wa kuongea na Wanafunzi wao, ambao watakuwa tayari vyumba vyao vitumike kwa wanaofanya Saili kisha mapato yanayopatikana yawe ni sehemu ya ada yao ya Hostel na Chuo kipate kidogo!
Kuliko kuacha watu wateseke mitaani, naliona hili kupunguza sana gharama za wanaokwenda kufanya Saili na hata hao wanafunzi kupunguza au kuepuka kabisa kulipa ada za Hostel.
Akalale hostel za UDOM, Humanity/ social. Au aende COED, ng'hong'hona Au alale nanenane stand, mbona pazuri tu. Au aende uswahilini huko mailimbili nk
Na ukizingatia vikao vya kamati za bunge vimeanza, dodoma inafurika 😀😀🙌
Lala stand au kanisa lolote mtoe tu mlinzi
Dah maisha haya, unalala kituo cha basi na bado kwenye interview huenda usifanikishe🤔Kama huna pesa lala kituo cha mabasi tu
Wakuu, sio vibaya wakati tunasubiri wenye uzoefu wa sehemu nzuri za kulala, tukaendelea kutaja na magari au namna rahisi zaidi za kufika Dodoma kwenye Saili.
Usafiri upo sabasaba utapanda daladala au bajaji wewe tuWakuu, sio vibaya wakati tunasubiri wenye uzoefu wa sehemu nzuri za kulala, tukaendelea kutaja na magari au namna rahisi zaidi za kufika Dodoma kwenye Saili.
Inaitwaje mkuuSikieni sasa kama huna kabisa hela, kuna guest moja bei ni 5k choo nje, na 7k(self) kama sijasahau, hii ipo karibu kabisa na Chuo yani unakiona chuo kile pale na unaweza ukatembea kabisa ila kuna mwendo.
Jinsi ya kufika: ukifika stend ya Mabasi panda gari zinazoenda mjini saba saba, ukifika mjini panda hiace zinazoenda ntyuka eeh ndio jina ilo ilo sijakosea.... shuka mwisho wa gari alafu nenda mbele barabara inapoelekea upande wa kulia utaiona iyo guest ni Local flani ila kama huna hela inaweza kufaa.
Wewe huwa unatumia mabasi au mbinu gani kufika Dodoma?