Valentine hiyoo, kama unampenda mtu mwambie kupitia hii post

The One and Only One Mama E.

Wewe ni binadamu wa kipekee sana.
Wewe ni rafiki yangu wa kweli.
Wewe unayajua maisha mno.
Wewe ni mwanamke wa Mithali 31
Wewe ni mshikaji wangu wa kudumu!

Wewe ni ua waridi lenye fumbo
Wewe ni shairi tamu litoneshalo mtima
Wewe ni hadithi tonofu isiyo na mwisho
Oooh! Binti mwema asiye na mawaa
Mpendwa wangu nipendezwaye nawe sana.

Happy Valentines rafiki yangu mwema. Mungu Akubariki na Azidi kukulinda.

Mimi nitakupenda na kukuenzi daima.
Upo! Nipo! Tupo! Njoo! πŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ˜˜πŸ˜˜πŸ˜˜



➑️➑️➑️ Asante kwa kuokoa maisha yangu. Sitasahau kamwe! πŸ™πŸΏ
 
Kweli kale katoto nakapenda ni kazuri sana 😍πŸ₯°
Umemtibua mpk siku hizi hanitumii pics za auntie yangu nimuone Mtseeww 😹😹🀣🀣
Ni kazuri sana uongo dhambi....kwani hukuzisave ukikamiss unakaangalia ka aunt akeπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Da Evelyn Salt unaitwa 😹😹
 
Nyumbani unawahi kufanya nini? Hebu mpe simu muhudumu niongee nae kwanza 😹😹
HahahπŸ˜„πŸ˜„πŸ˜‚,. Mji una vijana wa hovyo sana huu mwisho kujichanganya nikaonekana kwenye gazeti kesho., Wacha niwahi naona Boda wangu kashakuja 😊😊
 
Ila wasukuma mna mahaba jamani...
 
Nawatakia valentine njema Wana jamii forum wote wake kwa waume pamoja na familia zenu..... Bila kusahau wakaka na wadada,, kataa ndoa wote pamoja na ma jobless wote happy valentine kwenu nyote.
Asante Sana mkuu, imagine being KATAA NDOA & jobless valentine lazima Inoge sana
 
Ni kazuri sana uongo dhambi....kwani hukuzisave ukikamiss unakaangalia ka aunt akeπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Umeona na wewe kalivyo kashunu kale katoto? Pale bro alijua kufanya kweli, apate na mishepu ya auntie zake ya kibantu mbona itakuwa balaa πŸ₯°πŸ₯°

Sikusave mwaya, pia nilitaka mpya nimuone anavyozidi kuwa tishio..!! 😹
 
Ila wasukuma mna mahaba jamani...
Jichanganye uone...ila tu uwe mweupe na mwenye tako!

Hapa nimetoka kuuza malori mawili ya ng'ombe pale Pugu. We acha tu! 😁

➑️➑️➑️ On a serious note: Mama E aliokoa maisha yangu tena kwa kujitolea sana. Mwanamke kama huyo utamlipa nini mbali na kumpenda na kumheshimu sana?
 
Mimi sitaki kujichanganya.....nawaombea kila lenye heri na mama E wako.....mpendane sanaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…