Video: Makonda yamkuta makubwa, Ghalib wa GSM adai nyumba yake

Alaah!! Kumbe unaumia sababu tu alikukataa?? sasa nani anapenda uchafu?..... heee!....Njoo wewe uone navo faidi km unanionea wivu!!......na bado mtalia sana tu!
Mwaka huu mtanyooka
 
Hii Tume inawajibu wa kukusanya taarifa za Mali na madeni ya viongozi, hebu watoe taarifa kuhusu ndugu Makonda,Je alitoa taarifa kumiliki Mali hiyo?
 
Na alikua mtoto wa baba, lakini baba akafa! Hata mama hataishi milele! Kwa hiyo naye alitakiwa aishi kwa kufuata misingi ya maadili, sheria na katiba. Hakuna kuwatisha GSM wala nini, wacha bashite avune!
 
Watu wamejanjaruka, kila alichonyang,anya Makonda kwa watu kitarudi labda tutashindwa kumrudisha Ben Saanane.

Ila tutambana japo atuonyeshe walipomzika au walipomtupia baharini
Na siku moja apigwe viboko hadharani kwa kutumia madaraka vibaya
 
Huijui hii nchi, Kalaghabao.
 
Yoote sawa....lakini TAKUKURU wameomba mwenye ushahidi wa haya mambo aupeleke kwao.
Mnasubiri nini kupeleka huko?

Humu kijiweni kwenu sio TAKUKURU...

Humu ni kijiwe majungu tu.
TAKUKURU wanalipwa kutafuta ushahidi sio kusubiri kupelekewa ofisini.
 
Umenena vyema. Karibu sana FaizaFoxy.
 
Asante Sana kwa taarifa hii, naomba Mimi Mwanajeiefu mwenzenu, niwe mtu wa kwanza kuwajulisha kuwa hii vita ya kutaka kumdhalilisha mpakwa mafuta wa Beans, Paul Makonda, sasa ndio mwanzo WA mwisho wa hasidi huyu!. Karma ndio itamaliza kila kitu. Simaanishi Makonda ni malaika, bali, ni binaadamu kama binadamu wengine, hakuna mkamilifu, hivyo na yeye kuna makosa ametenda na tayari karma imeisha mshughulikia, hivyo kwa maonevu anayotendewa na hasidi huyu, ni Mungu, Baba ndiye atamlipia.
Kwanza mafanikio yake ni kutoka kwa Mungu.

Kisha, Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!

Hivyo, hata kampeni batili ya kutaka kumpora kiwanja, ni upepo tuu na utapita.

Watu kumfanyia fitna na majungu, Makonda, hawakuanza leo

Yote haya yatapita, na Makonda atasimama.
P
 
Nadhani GSM kama wana akili waache kucheza michezo ya wanasiasa. Hakuna aliyejua Nape atakuja kuwa Waziri karibuni.

Makonda anaweza kuja kuwa Rais au Waziri na mwenye ma mlaka ndipo utakapoona GSM wanakimbia nchi.
Mfano mzuri wamuulize Manji wakati wa baba Riz halafu yalomfika wakati wa Jiwe.
 
Yoote sawa....lakini TAKUKURU wameomba mwenye ushahidi wa haya mambo aupeleke kwao.
Mnasubiri nini kupeleka huko?

Humu kijiweni kwenu sio TAKUKURU...

Humu ni kijiwe majungu tu.
Enzi zile ukikutwa unakunywa tubia twako tuwili tutatu kwa siku, utakuta umewekewa barua mezani kwako ili ujieleze kuhusu ulicho nacho. Hiyo ni pamoja na mshahara wako kwa mwezi, mali unazomiliki n.k. Hawakuomba ushahidi toka kwa raia, bali wao wenyewe walifanya uchunguzi. Leo hii ukijifanya unayajua usiyopaswa kuyajua utapotezwa na usionekane tena katika sura ya dunia.
 
View attachment 2146208

Download
720
MAKONDA ANUSURIKA KUUWAWA

View attachment 2146206
Kama huyo anaesikika akihemka kwa jazba hapo ndie Gharib, basi sina mashaka kuwa ni muhuni mwenye akili za kitoto. Bilionea mkubwa unatishia mtu ambae hajabeba silaha kwa kupiga risasi?

Simkubali makonda na kinachompata hivi sasa ni KARMA; wala asilalamike, asilie, ajikaze kiume na ajiandae kuuonja mkuki!

Hata ile kuisusia taifa Starz kisa ugomvi wa nembo yake na simba ilikua ni akili za utoto pia.
 
Makonda anahujumiwa sababu ya misimamo yake isiyoyumba hususan kupambana na wauza unga na mafisadi.
EEh na mali ya zaidi ya billion 2 (kwa jumba moja tu) kwa muda mchache alioajiriwa ni akiba kutoka mshahara wake, au siyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…