VIDEO: Mlinzi wa Rais Samia alivyotaka kudondoka wakati Rais akihutubia

Hizi drama za moshi zilitolewaga maelezo kweli yakaeleweka? Ndiyo safar ya mzee mwendazake ilipoanza.

Inji inapitia wakati mgumu,tuliombee taifa.

Walisema JPM alikanyaga fire extinguisher / mtungi wa kuzima moto wa ndani ya motokaa kwa bahati mbaya alipo kuwa anakitubia kutoka ndani ya gari.

Lakini hata JPM alistuka hakukubali maelezo ya kuwa kafyatua kizima-moto, akawauliza wana wa Ruangwa Lindi yaani kweli mnanitumia mioshi ya ajabu ajabu, akavunja mkutano na kuondoka kwa kasi.

Hivyo hili la Dodoma hatujui kama ni aina ya hewa ilimkabili mlinzi, uchovu, maradhi ya mwili au afya ya akili n.k

Inabidi 'vyombo' husika kuchimba kila aina ya dhana, na kuyapatia majibu sahihi kuondoa chochote kitu kinachoweza kuwa kimetokea lakini kikampata mlinzi wa karibu kabisa wa kiongozi jukwaani.
 
Gentamicin anasema ana kuja na machimbo ya taarifa zaidi kutokea Mzena
 
Wa kuitwa "mama yao" ni katili sana na mtu asiyejali hata kidogo yaani hajaguswa na kilichotokea kwa msaidizi wake hata kuuliza kuna nini. "Boss is an animal"
 
Huu ni uzembe wa timu. Uzembe wa kuchelewa kutafsiri taarifa alizotoa Mlinzi, pili ni kuchelewa kuchukua hatua stahiki kwa wakati baada ya tafsiri, tatu, ni Mlinzi wa akiba (Mwanamke-anaekimbia kuja kutoa back-up) kukaa mbali, kukimbia kule kungeweza kuleta taharuki miongoni mwao wenyewe na kupoteza umakini, kama kungekuwa na nia ovu.

Mlinzi Kaanza kuwaambia kupitia vifaa, no response, mpaka amemwambia ADC (Mpambe) na ndipo (Mwanaume wa nyuma) kachukua hatua. Pia mwanaume wa mbele kushoto aliekaa, ameonekana hana habari na ni timu (Mtu wa kushoto).

ADC (Huyo mwanajeshi) sio Mlinzi ni Mpambe. Mlinzi ni huyo dada, na ndie yupo full package (armed with guns, well trained body defence, detectives and equipped information accessories).

Utaona ana kifaa kutoka sikioni kuja mdomoni. Ndie "informer" mtoa taarifa wa kwanza kwa timu kwa lolote linalotokea/analoliona hapo mbele au kwa audience. Yeye anaona kila "angle" ndio maana anakaa kulia-pembeni-nyuma.

ADC anakaa nyuma, haoni mbele anaona kisogo cha Raisi, sio kazi yake kuona kila "angle" yeye ni Mpambe. Huyo dada ndio "primary security ya Raisi" anaona kila kitu hapo na taarifa za ulinzi binafsi za Raisi zinaanzia kwake.

Kuhusu kuanguka: Ni suala la kawaida, na dada wa watu kachukua hatua zote stahiki hasa ya kuanza kutoa taarifa na kujikaza kutoleta taharuki na kunuia kuangukia nyuma bila kumletea taharuki Mkuu.

Ni kosa kumletea taharuki Amiri Jeshi, kumuogopesha, kumtia wasiwasi au kumshtua kwa namna yeyote ile.
 
Wa kuitwa "mama yao" ni katili sana na mtu asiyejali hata kidogo yaani hajaguswa na kilichotokea kwa msaidizi wake hata kuuliza kuna nini. "Boss is an animal"

Mahubiri ya 4R dhana yake ni kujali lakini kimatendo ni kinyume chake.

Kilichotokea kinadhihirisha kuwa 4R za kujali ni kauli zisizoaminiwa na mhubiri
 
Wewe umeongea kiume
 
Hata mimi nimeshangaa sana, DADA KAANZA MAWASILIANO MUDA MREFU NO RESPONSE ... THIS IS PATHETIC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…