VIDEO: Mlinzi wa Rais Samia alivyotaka kudondoka wakati Rais akihutubia

Huu usawa tunaulazimisha ila kiukweli ni kazi ngumu Kwa mwanamke kusimama muda mrefu
Iwepo division of labor, majukumu ya ulinzi yafanywd na wanaume
Huenda hukumbuki, au ulikuwa mdogo, au una kitu kinachoitwa superiority compleex. Jakaya Kikwete ni mwanaume, mwanajeshi aliyefikia cheo kikubwa. Yalimfika haya akiwa mgombea urais. Tujifunze kuweka kumbukumbu na kuwa 'fair'.
 
Ni mwanamke huyo, vipi kama alikuwa kwenye siku zake kikamjia kizunguzungu?. Unavyoongea utadhani wewe umekamilika kila unachokifanya kinakwenda vizuri.
 
Mbona unatetea Sana au kaguswa wa imani yetu😁😁😁

Angekuwa ngosha magufuli ungekenua😁
 
Huenda hukumbuki, au ulikuwa mdogo, au una kitu kinachoitwa superiority compleex. Jakaya Kikwete ni mwanaume, mwanajeshi aliyefikia cheo kikubwa. Yalimfika haya akiwa mgombea urais. Tujifunze kuweka kumbukumbu na kuwa 'fair'.
Kikwete ulikuwa umri alikuwa above 60
Sasa huyo Binti mdogo ujue ni mambo ya kibaolojia na maumbile
Mwanamke hapaswi kushiriki shughuli za ulinzi ili kulinda stara yake
 
Ni jambo la kawaida kibinadamu, lakini inaonekana alianza kumpa taarifa ADC mapema, wenzake hawakumsikia kupitia vifaa vyao vya mawasiliano? Naona kama kuna kauzembe.​
 
Ni mwanamke huyo, vipi kama alikuwa kwenye siku zake kikamjia kizunguzungu?. Unavyoongea utadhani wewe umekamilika kila unachokifanya kinakwenda vizuri.
Kama huyo bodigadi ameshindwa kazi aseme kuna walimu na makonda wanasimama siku nzima yeye ameshindwa kusimama kwa masaa machache na ni mwanajeshi are we serious ? Kuna watu wanatafuta kazi na ukiwapa nafasi ya kufanya mafunzo ya kijeshi wanapita kwa viwango vya juu. Tatizo hizo nafasi wanapeana wao kwa wao .
 
Ku
Kikwete ulikuwa umri alikuwa above 60
Sasa huyo Binti mdogo ujue ni mambo ya kibaolojia na maumbile
Mwanamke hapaswi kushiriki shughuli za ulinzi ili kulinda stara yake
Kumbuka kwamba ulijenga hoja ya ujanajike. Nami nikakukumbusha kwamba haya yanamtokea hata mwanamume ambaye ameshapitia jeshi na kufikia cheo cha kanali. Hujataja umri. Sasa ukitaka tujadili umri na tufanye hivyo. Ndo maana nimesema huenda una kitu kinachoitwa 'superiority complex' na unasahau ukweli ulivyo.
 
Jamii umeacha miiko
Kazi ya jeshi na ulinzi ni kazi ngumu Kwa maumbile na uweZo wa mwanamke haimfai
 
Wanachoka maana hawabadilishwi wanadhani ni sifa kufanya kazi mara kwa mara.
 
Huwa sioni ni nini walinzi hawa wa kusimama nyuma ya viongozi wanaweza fanya kumuokoa kiongozi na lolote baya lililopangwa kutekelezwa.
 
Huwa sioni ni nini walinzi hawa wa kusimama nyuma ya viongozi wanaweza fanya kumuokoa kiongozi na lolote baya lililopangwa kutekelezwa
 
Alijikaza kweli ikashindikana
Uchovu au ana pressure imepelekea kupata kizungu zungu
Hope atapewa matibabu na kupata mda wa kupumzika
kuna yule binti wa form three anaekata ngumi ka mandonga wangempa hii position
 
 
Mbona inaonekana kabisa anaomba msaada hapo kwamba amezidiwa? Mimi hapo namlaumu sana huyu ADC aliyevaa magwanda ya jeshi ,amefanya uzembe mkubwa sana,mlinzi wa rais aliona dalili ya kuzidiwa akampa taarifa ADC amsaidie na yeye kaleta uzembe ,ADC alikuwa karibu lakini aliyekuja kumzuia asidondoke ni jamaa mwingine ambaye alikuwa mbali kidogo,jamaa aliyekuja kumzuia yupo makini sana maana ukimtazama alikuwa wala amuangalii lakini alistukia mchezo fasta akaenda kumdaka kuliko ADC aliyekuwepo karibu na ameshindwa kuzuia fedheha....Dada mlinzi naye yupo vizuri japo amepata changamoto za kibinadamu.
 
Wazee wanatest mitambo 😊😊, Dah hatari sana, chuma kimetumwa, kikashindwa kika twist around ha ha haπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Katika nyakati hizi za karibu na chaguzi, umakini unahitajika sana, post ya urais huwa na fitna sana, tumuombee dua Rais wetu, yule alikuwa subiani 😊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…