VIDEO: Mlinzi wa Rais Samia alivyotaka kudondoka wakati Rais akihutubia

Itakuwa naye anashauriwa na Prof Janabi kuhusu afya na lishe.
 
Kitaalamu hii hali ya kudondoka ghafla inaweza kusababishwa na:

-sukari kushuka (hypoglycemia)

-presha ya damu kushuka (hasa kwa mtu anayesimama kwa muda mrefu au kusimama ghafla: orthostatic hypotension)

-matumizi ya aina fulani za dawa

-upungufu wa maji mwilini (dehydration)

-hali ya kihisia mfano hasira, maumivu, uchovu nk

-maradhi mengine kama vile matatizo ya moyo nk
 
Huyo hakuwa mlinzi (Bodyguard)wa Prince charles alikuwa royal guard alidondoka kwenye parade.
 
Labda Jana yake kakesha klabu na mipombe, inapaswa waliopangiwa kusimama na rais wanakaa sehemu ikulu Jana yake bila raha au mbwembwe zozote.
Hizo ni pombe nyingi, kukosa chakula cha kutosha na maji...Hakuna kingine!
 
Ni mambo ya kawaida kwa binadamu, majukumu yake ya kusimama mda mrefu, huenda kuna wakati pressure inashuka ghafla hivyo kusababisha ubongo kukosa oxygen ya kutosha.

Anaweza kupata hali hiyo mtu yoyote. Pole yake.
Kweli kabisa. Pole sana kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…