Video: Mwanamke aliyetambulika kwa jina la 'Rose' adaiwa kutekwa maeneo ya Mlimani City

Video: Mwanamke aliyetambulika kwa jina la 'Rose' adaiwa kutekwa maeneo ya Mlimani City

Huyu Dada kajulikana kwa jina moja Rose, Leo akiwa maeneo ya Mlimani City amevamiwa na watu Wasiojulikana, wamemchukua na kuondoka nae.

Mashuhuda wanasema baadhi ya watu walijaribu kuwahoji waliomchukua kwamba wao ni akina nan? Wametokea wapi? Na wanampeleka wapi Rose? Wakaishia kupigwa.Tukio limetokea masaa mawili yaliyopita, Hakuna aliyesalama Ndugu zangu


Nashangaaa watu wamesimama pembeni , tabia gani hii watanzania
Sasa wewe huoni hiyo 'clip' iliyowezekana?

Ulitaka wafanye nini kwa watu wenye mitutu!
 
Naona mpaka sahv hakuna
Taarifa rasmi ,huyo rose ni nani anajishugulisha na nini
Tusubirieni pdf la PT wenyewe
Yawezekana wakasema alikuwa bwiiii,au mgonjwa

Ova
 
Mmemuona hadi mwanamke mmoja hapa naye ni mtekaji akiwasaidia watekaji wa kiume.

Niseme tu hadi sasa njia zote za kistaarabu zimeshindikana , hatuwezi kupata muafaka mpaka pande zote ziumie ili tukija katika meza ya mazungumzo tuna plasters na bandages kila upande utachagua kuheshimiana maana wote tumeumia.

Jifunzeni wasomali wanafanyaje , mpaka kumfikia mtu chimbuko lake la chini ngazi ya ukoo ili kusudi ukiharibu tu basi ujue nyuma yako umewauza ndugu zako wote.

Bila hivyo kundi la wasio na silaha litaendelea kuumiza wasio na silaha.
 
Mungu amlinde na kumpigania Rose,na usikute hapo kulikuwa na watu na hawakufanya kitu,tumekuwa kama Nyumbu
 
Mbona hapukuwa na fujo yoyote
Yumkin kuna Ajali ya pkpk Askari wamemsaidia uyo Dada kumpeleka hospital 👈

Mazingira yote ayaoneshi msuguano wowote kati ya mpakiwaji na Askari❗️
na wapita njia wapo free kuendelea na mishe zao❗️

Kama ingekuwa ni utekaji naamini yule Dada mwenye Simu angetakiwa kupotea alaka iyo sehemu ❗️

Lkn Askari wapo poa na yoyote pale sioni
Kwanini mmewaza utekaji

Michadema ni Janga kwa Taifa Uchochezi waziwazi kabisa hawana akili nyengine kukuza Umoja wao zaidi ya Uchochezi tu❗️

kwenye ilo tukio ni rafiki kabisa kusaidiana tu kosa 🤔🤔

kisa kushika Mtutu mmoja wao ndio Ushahidi wa utekaji 🤠🤠

mizwazwa vichwani nyinyi kusoma tukio mmeshindwa✍️
 
Lakini kuchukuliwa namna hii kwenye nchi ya amani, utawala bira na mifumo ya ulinzi na usalama ni sawa kweli gentleman?

Hii inaacha picha gani kwa wananchi? Kwamba tujitetee wenyewe bila kuviamini vyombo vyetu vilivyokabidhiwa jukumu la kulinda usalama wa raia na mali zao?

Lakini acha tusubirie, huenda taarifa ikatolewa yenye maelezo ya hili tukio, tuvute subira Gentleman.
picha ni kwamba ishi na watu vizuri gentleman otherwise utapata tabu sana aise politically speaking 🐒
 
Hii Nchi saivi kila mmoja anaweza kutekwa na hao wasiojulikana

Maana unaweza kuwa mmoja wao na bado ukatekwa vile vile

Kwahiyo suala hili linapaswa lipigwe vita na Kila mmoja

Hakuna aliyesalama
 
Kama wanampeleka Kituo cha Polisi harafu waje kutoa taarifa sababu ya kukamatwa raia tusingekuwa tunaogopa! Tunajua haki itafuta mkondo wake! Lakini huyo sasa kijana huenda tukamsahau!
 
Unajua nani kamteka? Mbona utekaji upo tangia zamani? Watu hutekana kwa mambo yao binafsi, wamedhulumiana, wamechukuliana wake/mume, wapenzi. Kwanini kila wakati tufikirie ni jeshi la polisi? Polisi kazi yao ni kuteka? Hiyo ni siasa za hovyo, kishamba, za maji taka hasa kutoka nyumbu wa chadema.
Kwa hiyo kila anayepaza kukemea uovu na utekaji ni chadema tu, hakuna raia mwema na mwenye hofu ya Mungu anayefurahia haya mambo.
wewe na nyumbu tofauti yenu ni idadi ya miguu tu
 
Back
Top Bottom