Ujumbe uliochapishwa na Mange Kimambi kwenye ukurasa wa Instagram.
"Dada Mange moyo wangu unavuja damu, Watanganyika tumekuwa watumwa kwenye nchi yetu wenyewe. Tumekuwa mayatima, hakuna jeshi la kutusaidia, hatuna viongozi tuko wananchi kujipigania wenyewe
Hapo ni Nyamongo North Mara. polisi walikua wanapita kila nyumba kuvunja milango kutafuta vijana wa kiume tuh. Yani kila nyumba wanavunja Milango wanawatoa wanaume kama unabahati unapigika na wanaondoka na wewe kwenda kituoni, vijana wengi wamefia kituo cha polisi, wenye bahati mbaya zaidi walikuwa wanapigwa risasi hapo hapo kwenye majumba yao. Askari wenye kiswahili cha bongo walikuwa wanapiga na kubeba vijana lakini wenye kuongea kama Kizanzibari walikuwa wanaua hapo hapo tena wanahakikisha ni risasi ya kichwa au kifua."