Video: Polisi watoa tamko baada ya kuzuiwa kupita kwenye barabara ya mwendokasi

Utaratibu lazima kuheshimiwa. Mwendo kasi barabara zao zisiingiliwe. Wengi tumeona maofisa wa jeshi, polisi wa jeshi na vigogo serikalini wakipita kibabe kwenye barabara za mwendo kasi. Bodaboda ndio zaidi. Inafaa polisi waanze tena kuwakamata na kuwachapa viboko.
 

Sasa mkuu Hilo tamko si limetolewa na hao hao polisi wanaoelewa vizuri taratibu na mipango Yao kuliko Mimi na wewe?

Kama mambo yangekua rahisi hivyo msafara wa rais ungekua unapita kwenye barabara ya mwendo kasi tu.
 
We unafikir hapo hakukuwa na dharura?
Au unafikir walijikusanya tu nakusema ngoja tukasumbue watu wa dart kwa kupita hapo
Changamoto ni namna gani unajua dharura ya kweli au ni polisi tu wanarudi lindo.
 
kwahiyo wawe na kipaza sauti wanadi " jamani tuna emergency tafadhali tunaomba idhini yenu kupita Kuna tukio la ujambazi tunaenda kulizima 📢📢📢📢🎤
Ndio changamoto, iko hapo. Ni namna gani unatofautisha askari wanaokwenda kwenye dharura au wanarudi kutoka lindo.
 
Hawa Sasa washapewa kichwa,
 

Attachments

  • IMG_20220916_123304.jpg
    38.8 KB · Views: 2
ambulance na zimamoto ni ruhusa kupita mwendokasi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Jiulize swali dogo tu!!

Kwa nn wanawazuia kupita jibu la hilo swali litakupa mwelekeo kama Kuna ruhusa ya dharura au la??
 
Nadhani msemaji kajisemea yeye kama yeye. Ila ukweli unabaki pale pale, kwa mazingira ya miundombinu yetu hizo barabara zitatumika tu panapokuwa na dharula. Alichokitolea ufafanuzi ni siasa aseme wamewachukulia hatua gani hao polisi???? Ni bora angetoa ufafanuzi wa jambo husika. Haya mambo ya kukopy na kupaste toka nchi zilizoendelea yana madhara sana. Nchi za wenzetu unakuta kila upande njia nnne na kuna mwendokasi na kuna barabara zingine maalumu za taxi etc, wewe leo una njia moja tu eti unaanza kulalama.
 
Ingekua wakati wa uchaguzi au Chadema wameshinda Jimbo la Kibamba wangeruhusiwa kupita bila tatizo.
Polisi ni Wazuri Kwa watawala na Mali zao na miradi yao wakati wa uchaguzi ili kuzia wapinzani wasitangazwe.
 











Haya ni matokeo ya utawala kibogoyo
 
hao watu wa mwendokasi wamekosea huwezi kuzuia watu wa usalama kupita wao wakipata shida nani atawasaidia

Polisi huwa hawatoi msaada zaidi ya kuomba rushwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…