Video: Polisi watoa tamko baada ya kuzuiwa kupita kwenye barabara ya mwendokasi

Video: Polisi watoa tamko baada ya kuzuiwa kupita kwenye barabara ya mwendokasi

Incompetence kama kawaida inaendelea.

Hii Incompetence kuna siku italeta maafa makubwa sana tukiendelea kuifanyia mzaha.

Serikali ijitathmini mara mbili mbili na kuruhusu mawazo na mifumo huru ili kuibadili hii hali yetu mbaya tuliyonayo kila mahala.

Mifumo huru na mawazo huru inaweza kuleta watu competent kwenye mifumo ambao wanaweza kuleta changes hapa na pale.

Watanzania competent wapo mitaani na sekta binafsi wamejaa tele tatizo mifumo sio rafiki kwa watu hawa baadala yake ni rafiki kwa wajinga, incompetent, na wapumbavu wengine, kikosi hiki kimejiwekea mifumo migumu kuwalinda na watoto wao matokeo yake wanaoteseka ni watanzania weengi sana.
 
Mara nyingi nimekuambia una matatizo ya akili. Na uzuri hutumii nguvu kuthibitisha hilo.
Humu jamii forum hakuna mitihani ya kuchuja kuwa wenye akili tu ndo muwepo. Huna namna zaidi ya kuishi na watu aina zote humu, jikaze.
 
Hawa ni walinda usalama wetu wanalinda mabenki, wanalinda wakuu wetu wa nchi, wanalinda hata ambavyo sisi kwa uelewa wetu hatuwezi ona! chukulia mfano kukawa na tukio hata la ujambazi ndani ya mwendokasi kituoni halafu hawa FFU wakawa karibu! najua watu wa mwendokasi watawakimbiloa polisi wawasaidie!
Unawasemea unaonekana chawa, wao wamekataa kuwa hawako juu ya sheria hivyo pamoja na upolisi wao hawatakiwi kupita humo, hiyo njia ni kama reli au runway ya ndege
 
Huyu mlinzi wa barabara za mwendokasi Hana adabu kabisa au alikuwa anataka sifa, Hawa kikosi Cha Askari wa Field Force unit Mara nyingi hawana tabu,na ukiona wamejazana hivyo kwenye gari zao ujue wanawai tukio sehemu, au wanaenda kwenye lindo either hata Ikulu, na kingine sasaivi Kuna oparation ya panyarodi usikute wanaenda kuwakamata sehemu,

Mimi nashauri huyo mlinzi wa barabara za mwendokasi atiwe adabu hili hawe na nidhamu, tofauti na hapo Wengine nao wataiga huo ujinga na dharau
Tanzania tumezoea uvunjifu wa sheria kwa wanaotakiwa kulinda sheria kiasi kwamba tunaona ni sawa. Huyo mlinzi yuko sawa kabisa.
 
Kwa hali hii panya road watatuua mwaka huu kama raia ataki polisi wafanye kazi zao kwa haraka afu panya road wakiuwa watu na kupora watu mnalalamikia polisi tena
Eeh mungu wabariki hawa wabongo na vichwa vyao vibovu
Raia hataki polis afanye kazi yao? You mean watumie barabara ya mwendo kasi pale wanapotaka wao si kwa kufuata sheria?
 
Tanzania tumezoea uvunjifu wa sheria kwa wanaotakiwa kulinda sheria kiasi kwamba tunaona ni sawa. Huyo mlinzi yuko sawa kabisa.
Mimi bado naona Kama amekosea! Hivi unajua Kuna siku gari ya mwendokasi ilimgonga mwendesha bodaboda, na raia wakataka kufanya fujo, haohao walinzi wa mwendokasi wakawapigia polisi wawai haraka,
 
hapana amekosea Sana, hao Ni walinzi wetu na usikute hapo labda walikuwa wanawai mtaani kwake huyo mlinzi wa mwendokasi Kuna vurugu imetokea.
1663303112380.png
 
hapana, sie kutwa tunalaumu polisi hawaji kwenye matukio ya uhalifu kwa muda sahihi, Sasa hapo ukute walikuwa wanawai kwenye tukio la uhalifu
Haitakiwi kuvunja sheria ili utekeleze usimamizi wa sheria.Hizi sheria walizitunga wenyewe kwahiyo kama polisi hawana msamaha wakupita hapo mlinzi yuko sahihi.Kama hawana hicho kibali unachokiongea ni hisia zako kwasababu sheria haiwatambui kuvunja sheria kwenye eneo hilo.
 
Back
Top Bottom