VIDEO: Rais Ruto apigwa na kiatu akihutubia Wananchi wa Kehancha

VIDEO: Rais Ruto apigwa na kiatu akihutubia Wananchi wa Kehancha

Viongozi wa afrika wakitenda haki ni ulinzi tosha kwao na usiyo hitaji gharama yoyote ya kutumia kodi za wananchi.
 
Mpangilio wa ulinzi wa rais wa kenya ukoje mpaka anarushiwa kiatu kinamfikia? Kwetu ulinzi wa rais umeimarishwa sana tofauti na zamani unaweza kumshika rais mkono bila shida. Kwetu rais ametengwa mbali huwezi kumfikia kirahisi kuna vizuizi vingi, utaishia kumuona kwenye luninga zilizopo uwanjani, yeye yuko mbali. Kenya naona rais wao yuko karibu mno na anaowahutubia
Kwetu si kwamba ulinzi ni bora saana, ni vile hakuna wadhubutu wa kufanya hivyo. Kenya wana katiba ambayo haipendelei viongoz na imewapa nguvu raia( yes kuna saa wanapitiliza) lakini haimaanish security ya rais ni mbovu.
Bush yaliwah kumkuta na ni rais wa america
 
Tangu Wakenya wapigane Mwaka 2007, raia wake wameshindwa kabisa kuwa waoga Kwa Viongozi wao

Tofauti na hapa nyumbani, ambapo raia anaweza kutekwa Mchana kweupe na wasiojulikana na raia wote kubaki kimya bila hata kuchukua hatua 🙌
Ubaya wa hapa ni kuwa watapigana kivyama, CCM wanajulikana ila wa upande mwjngine hawajulikani
 
Wakenya wanafundishwa elimu ya uraia ko hawanaga kuogopa.... Umewahi kusikia chawa wa Ruto? Huko hata wafuasi wa Ruto wanampinga akikengeuka!..

Nyerere aliambiwa anaongoza maiti zinazotembea😃😃😂
Kupiga Rais na kiatu ni elimu ya uraia?
 
Huku kwetu isingekuwa Mwl Nyerere kidai Uhuru hadi leo hii tungeendelea kuwa Chini ya Ukoloni

Maana nina uhakika akina Mwijaku na mwenzake Steve Nyerere wangeendelea kuwa Machawa wa Wakoloni🙌
Eeh majitu ya hivyo hayakosekanagi, wasaliti
 
Ubaya wa hapa ni kuwa watapigana kivyama, CCM wanajulikana ila wa upande mwjngine hawajulikani
Ndiyo tatizo letu, tunaendekeza uvyama badala ya maslahi ya pamoja ya Taifa

Kwa maana kama issue ni ukosefu wa ajira, hili tatizo Lina athiri Vijana wote bila kujali itikadi

We kaangalie issue ya betting, ni Vijana wote cha CDM na CCM wote Wana bet
 
Ndio maana ya maiti zinazotembea

Kwa miaka kibao bado hatuna dalili yoyote ya kum prove wrong mzee Kenyatta
 
Ndio maana ya maiti zinazotembea

Kwa miaka kibao bado hatuna dalili yoyote ya kum prove wrong mzee Kenyatta
Sahihi Mkuu, na kadri miaka inavyozidi kwenda mbele ndiyo hali inazidi kuwa mbaya Kwa Vijana wetu

Kwasasa wanaona uchawa unawalipa kuliko ustawi wa maisha yao Kwa ujumla
 
Mtu mmoja amemrushia kiatu Rais wa Kenya William Ruto wakati akizungumza na wananchi wa Kehancha, Kitongoji cha Migori ambapo leo alikuwa anazindua mradi wa nyumba 298 zenye nafuu kwa wananchi.

Kiatu hicho kilimkosa Rais Ruto ambaye aliendelea kuzungumza na wananchi wa eneo hilo bila kujali kilichotokea.
View attachment 3324644
Wahuni hao...
 
Back
Top Bottom