Video: Rudia kusikiliza maneno yaliyomtia matatani Lissu; Serikali ilichukua hatua mwafaka

Video: Rudia kusikiliza maneno yaliyomtia matatani Lissu; Serikali ilichukua hatua mwafaka

Kwani alimtaja mkuu gani wa nchi anataka kumuua au kupindua serikali yake? Je, ukisema "mwaka huu sitalipa kodi..." utaweza kushtakiwa kwa kutotaka kulipa kodi ya serikali, na ni sheria gani utakuwa umevunja?
Unaamini kabisa ni kichaka cha kujificha hicho?? Lissu kuchamba kwingi kayavagaa mavi. Kajipangeni na utetezi
 
Hiyo fujo anayotaka kuleta unaweza kuithibitishaje? Je, neno "kukinukisha" kwa sheria za Tanzania lina maana gani au ni sheria gani inayofanya "kukinukisha" liwe kosa la jinai?
Unataka nikupe majibu hapa ya awali?? Yeye sasa ndiyo atatumbia maana ya kukinukisha bila kutarajia!!
 
Pumbavu kabisa...

Ni sheria ipi inawapa polisi mamlaka kutoa amri ya kuzuia watu kwenda mahakamani?

John Heche alikamatiwa Salender Brdge. Hapo ni mahakamani? Alivunja sheria gani?

Hao hawakuwa polisi....!!

Matendo yao siku hiyo yanasadifu kuwa, hao hawakuwa polisi waliofundishwa kutenda kwa mujibu wa sheria...!

Wale walikuwa wahuni na majambazi yaliyokuwa na kichaa cha mbwa na kuvikwa magwanda ya polisi...
Na wewe next kesi ya Lissu inatajwa nawe uende ndiyo utajua kuwa amri ya Polisi ni sheria. Usipimane ubavu na mtu amevaa kofia yenye crown ya Serikali (Bibi na Bwana na zile pembe)
 
Huyo hamjamkamata mmemzuia tu yaani hana uhuru wake...............sasa jiandaeni ceo wote wa tanzania kuja ulaya ,marekani na Canada itakuwa ndoto nyevu.............
Una mawazo ya kikoloni sana, nyie endeleeni tu kuishi diaspora hamujitambui
 
Treason is the crime of betraying your country or government, typically by actions like assisting its enemies, levying war against it, or attempting to overthrow it. It's a serious offense with severe consequences
Sedition is the crime of inciting rebellion or resistance against a government or governing authority, typically involving words, speech, or actions that incite discontent or insurrection. It often includes the intent to disrupt the peace and stability of the state and to subvert the established order.
Nakunukuu "It often includes the intent to disrupt the peace and stability of the state and to subvert the established order".

Je hiyo hali kwenye clip ya Lissu hujaisikia pale mwishoni? Anasema "Tutakunukisha, tutaleta vurugu, uchaguzi hauyafanyika"
 
Kuchochea watu ili kufanya mapinduzi dhidi ya utawala wa kiraia au wa kifalme
Kwa vile Ban Barka yupo kimya; nimeuliza AI na haya ndiyo majibu


Ah, thank you for the clarification and the definition of "sedition." Now I understand the context.

In Kiswahili, the most direct and commonly used translation for "sedition" in this legal and political sense is:

uchochezi

This term encapsulates the meaning of inciting rebellion or resistance against the government.

Here are some related phrases you might also encounter or find useful:

  • Kosa la uchochezi: The offense/crime of sedition.
  • Kuchochea uasi: To incite rebellion.
  • Kuchochea upinzani dhidi ya serikali: To incite opposition against the government.
  • Maneno ya uchochezi: Seditious words/speech.
  • Vitendo vya uchochezi: Seditious acts.
  • Kupandikiza chuki dhidi ya serikali: To sow hatred against the government (often a component of sedition).
  • Kujaribu kupindua serikali kwa nguvu: To attempt to overthrow the government by force (a more extreme form of rebellion that sedition can lead to).
So, if you were to talk about the crime of sedition in Tanzania, you would most likely use the word uchochezi.
 
Unataka nikupe majibu hapa ya awali?? Yeye sasa ndiyo atatumbia maana ya kukinukisha bila kutarajia!!
"He who claims must prove". Hii ndiyo kanuni ya kisheria - yaani kwamba unadai X kaiba, then wewe unsyedai
Unataka nikupe majibu hapa ya awali?? Yeye sasa ndiyo atatumbia maana ya kukinukisha bila kutarajia!!
Kuna kanuni ya kisheria inasema "he who claims must prove" - yaani kama X anadai kwamba Y kaiba, basi X ndiye mwenye jukumu la kuthibisha na si Y.
 
Unaamini kabisa ni kichaka cha kujificha hicho?? Lissu kuchamba kwingi kayavagaa mavi. Kajipangeni na utetezi
Wewe na mimi "we wait and see" na ndiyo maana sisi wadau wa sheria tunatamani sana kesi hii iendeshwe kwa uwazi, na watu wsnaohudhuria mahakamani wasikamatwe, kupigwa na kuumizwa ili wote tujifunze tusitende makosa kama haya.
 
View attachment 3322296

Yeye mwenyewe Tundu anasema anataka nafasi fulani, hataipata kwa sheria hii ya uchaguzi. Inabidi aanzishe uasi na walio tayari. Anaendelea kusema akianzisha uasi atakinukusha, uchaguzi hautafanyika. Atakamatwa, atashtakiwa kwa uhaini....
Hii video nimechelewa kuisikiliza...ukiwa na akili timamu utangundua Lissu ameyasema haya kwa makusudi,mtu wa kada yake hawezi kusema maneno ya kujifunga kiasi hiki na anarudia kuwa atachochoa maasi/uhaini huu ni mchongo Lissu anatumika.
Hakika wanasiasa si wa kuaminiwa
 
Kwenye video kaanza na maneno …” wanasema hivi…”
Hao wanao sema ni akina nani? Si maneno yake…
Mpaka hapo tayari kachomoka…
Mbeleni kajifunga, kwanini hakutumia maneno kama "nitahasisha jamii iunge mkono mabadiliko" kuliko kutumia uasi kukinukisha??
Hapa naona Lissu aliamua kujikabidhi kwenye vyombo vya dola kwa makusudi
 
Tatizo mkuu Lord denning mumemfanya Tundu ni kama nabii au malaika wenu. Hamtaki akosolewe, laiti mungekuwa mnasahihisha anapokosea, kamwe asingetoa ile kauli.

Ananyea debe Ukonga, nyie mko huku MNAKINUKISHA kama ma key board warriors
Wa upande wako unaweza kuwasahihisha?
 
Hii nchi watu wengi ni aina ya mwenye uzi huu. Bado wapo utumwani. Utumwa wa fikra.
Mtu aiongea uhalisia wanaona anatukana sijui hivi mara vile ila mamtu yanaiba pesa yanaiba uchaguzi pamoja na uhai wa watu huko Zimbabwe yenyewe hapo kimya tu.
Inakera sana.
 
Hii video nimechelewa kuisikiliza...ukiwa na akili timamu utangundua Lissu ameyasema haya kwa makusudi,mtu wa kada yake hawezi kusema maneno ya kujifunga kiasi hiki na anarudia kuwa atachochoa maasi/uhaini huu ni mchongo Lissu anatumika.
Hakika wanasiasa si wa kuaminiwa
Asante Mkuu kwa kuliina hilo. Ila nashukuru kuwa Serikali haicheki na kima, imeamua kuchukua hatua
 
Hii nchi watu wengi ni aina ya mwenye uzi huu. Bado wapo utumwani. Utumwa wa fikra.
Mtu aiongea uhalisia wanaona anatukana sijui hivi mara vile ila mamtu yanaiba pesa yanaiba uchaguzi pamoja na uhai wa watu huko Zimbabwe yenyewe hapo kimya tu.
Inakera sana.
Wewe mwenye busara mbona uko huru huku nje? Lissu anasota Ukonga wewe unaandika upumbavu hapa
 
..kwa hiyo hukumu ya kunyongwa, au kifungo cha maisha, inamhusu?

..CCM mnapenda njia ngumu, wakati njia zenye nafuu zipo.

..kufanya REFORMS ni rahisi kuliko kuuwa wanaharakati.
Wafanye reforms ili waachie madaraka??
Ili wakose ugali wao waliuzoea??
Sio rahisi ndugu
 
Back
Top Bottom