Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 32,270
- 44,403
- Thread starter
- #10,941
Wakikuekea wao ina maana unapewa Tu jina la WiFi na password yake, unakua huna hata uwezo wa kubadili Hilo jina na password, kwa mtaani watu wanaweza share password yako Hadi inakua WiFi ya mtaa na huna chochote cha Kuwafanya.Kaka naomba utufahamishe utofauti uliopo kati ya kutumia configurations wanazokupa wao na namna ambayo wadau wengi wanapenda kupewa uhuru wa kuichezea Router kwa namna wanavyotaka wao?.
Ukiwa na user na password ya router utaweza Fanya mambo mengi kama
1. Kubadili jina na password ya WiFi
2. Router ya TTCL ina uwezo wa Ku whitelist na blacklist, kama unauza WiFi mtaani hii inasaidia sana unaiset watu ulio wa whitelist pekee wapate internet, hata MTU akishare password na mwenzake hapati internet.
3. Uwezo wa kutengeneza WiFi zaidi ya moja, unaweza ukawa na WiFi moja yako private na nyengine kwa ajili ya public kutumia.
4. Uwezo wa Ku connect na VPN, hasa kwa hizi TV zetu smart zisizo na VPN apps kama tizen ya Samsung, webos ya LG, vidaa Ya hisense etc unaconect VPN na router, TV inafanya hivyo unaangalia content za nje kwa urahisi.
5. Kutengeneza media server kwa kutumia Hard disk, na vifaa vyako kupata, unaweza ukaweka HDD ya movie na vifaa vyako vyote ndani vikaweza kuplay. Router nyengine advanced zinauwezo wa kutengeneza Torserve na jacket kwa ajili ya kuparse torrent na kuzi convert kwenda http kwa ajili ya vifaa vyako.
Hivyo lakini unafanya na router ya TTCL, router nyengine hazina features nyingi kama ya TTCL ila still utapata baadhi ya features.
Long story short router ni computer, ina processor, Ram, storage etc, ukiwa na router ambayo ni advanced unapata features nyingi Sana ambazo zinakusaidia kwenye day to day tasks za nyumbani.