Vijana mnakwama wapi? Kuna kijana nilimuunganisha ajira hata asante hajanipa anataka nimtafutie ajira sehemu nyingine sasa

Huyo dogo kakosea. Ila sasa na wewe usitumie wema uliomfanyia kama fimbo ya kumchapia yaani akifanya kitu kidogo unaanza sii mimi ndio nilinsaidia inaudhi sana tubadilike

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
Yeye anajitegemea huko kwake na Mimi nina maisha yangu. Ni mke wangu pekee anayejua kuwa nimemsaidia kupata ajira. Hata ndugu zake hawajui nani kumsaidia.
Sijawahi kumsema vibaya, tunaongea vizuri tu.
Kilichoniboa mpaka kuleta Uzi huu na ninawaza nimwambie wiki Moja au mbili alinikopa pesa nikamwambia siwezi kukukopesha nakupa tu. Tusiishi kwa kukopana. Nikamtumia zaidi ya alichokopa, leo kanitext nilijua anataka kuituma ile pesa kumbe anataka nimpigabie ajira mahali.
Huyu ana akili kweli?
Si mtoto wangu
Si ndugu yangu
Nampa njia mjini anataka nimpeleke mbali zaidi huku hata padogo kashindwa kusema Asante
 
Mtu wa hivyo unamchelewesha wa nini mpige chini hafai

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
 
Vijana wetu wa kileo wengi ni tatizo, shida inasnzia kwenye malezi ngazi ya familia.
 
Afadhari wewe huyo uliemsaidia bado yupo kazina na hakuna kashifa yeyote ili iliyotokea, sasa mimi nilimpambania mtoto wa dada binamu ktk ukoo na ukizingatia elimu yake ni fomu 4 mwenye D 2 na akapata kazi nzuri tu mshahara laki 5, lakini cha ajabu kaenda kazini siku mbili tu na kuacha kazi hadi dada (mama yake mzazi) alidondosha kilio na machozi baada ya kuona binti yake kagoma kwenda kazini.

Leo hii nimepita ktk kampuni fulani wameniomba niwatafutie mfanyakazi nikakimbuka lile sakata nikasema moyoni simtafutii tena mtoto wa mtu kazi nilikumbuka issue ya yule binti alivyonidhalilisha baada ya kuacha kazi.
 
Jmn kweli kwenye miti hakuna wajenzi
😞
Ila hapana, usiache kufanya Kwa sehemu Yako mkuu huwezi jua
 
Mjinga huyo mm nlipigania vijana wawili wakapata kazi ya udereva wa maroli ya kokoto aisee wale vijana nliishi nao vizuri sana popote watakaponikuta hawaniachi nasafiri buleee na pesa ntapata. Matunda naletewa. Nliishi kibosi sana
 
Jambo kama shukrani ni tabia ya mtu ya ndani sio kabila wala kikundi cha watu ...sema mimi ni wa kusini watu wa kusini tuna kakiburi flani iv na kwa asili Ka uvivu kamo cha kutaka mtu akubebe kla mahala sema sio wote ila asili ya walio wengi
😍😍Kuchidachi wamakonde wenzangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…