Vijana mnakwama wapi? Kuna kijana nilimuunganisha ajira hata asante hajanipa anataka nimtafutie ajira sehemu nyingine sasa

Vijana mnakwama wapi? Kuna kijana nilimuunganisha ajira hata asante hajanipa anataka nimtafutie ajira sehemu nyingine sasa

Huyo dogo kakosea. Ila sasa na wewe usitumie wema uliomfanyia kama fimbo ya kumchapia yaani akifanya kitu kidogo unaanza sii mimi ndio nilinsaidia inaudhi sana tubadilike

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
Yeye anajitegemea huko kwake na Mimi nina maisha yangu. Ni mke wangu pekee anayejua kuwa nimemsaidia kupata ajira. Hata ndugu zake hawajui nani kumsaidia.
Sijawahi kumsema vibaya, tunaongea vizuri tu.
Kilichoniboa mpaka kuleta Uzi huu na ninawaza nimwambie wiki Moja au mbili alinikopa pesa nikamwambia siwezi kukukopesha nakupa tu. Tusiishi kwa kukopana. Nikamtumia zaidi ya alichokopa, leo kanitext nilijua anataka kuituma ile pesa kumbe anataka nimpigabie ajira mahali.
Huyu ana akili kweli?
Si mtoto wangu
Si ndugu yangu
Nampa njia mjini anataka nimpeleke mbali zaidi huku hata padogo kashindwa kusema Asante
 
Mtu wa hivyo unamchelewesha wa nini mpige chini hafai

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
 
Hello!
Huyu dogo kama atakuwa humu atasoma bandiko hili maana si baya kivile.
Imepita mwaka sasa tangu nimuunganishe kwenye ajira (sekta binafsi) kama dereva wa malori. Kampuni kubwa tu hapa Bongo. Anapokea around 500k -800k kwa mwezi.
Sasa ile stori na wenzake anapata kujua fursa zaidi kwenye kampuni zingine.
Si unajua stori za wafanyakazi kupenda kuambiana sehemu B wako vizuri kimaslahi.
Lengo langu si kutazamia malipo kwake, nilimsaidia tu , kilichonishangaza bado anataka tena connection kutoka kwangu anashindwa kujisimamia afike huko anakowaza.
Sasa akisikia kuna sehemu wanalipa vizuri zaidi ananipigia simu kutaka nimuunganishe ajira huko.
Mtu alikuwa juu ya mawe umemfanyia mpango hajakumbuka hata ile brother Asante kilo ya sukari hii hapa unywe chai na watoto leo anataka umpigañie sehemu nyingine.
Ikumbukwe huyu dogo hatuna undugu , nilidanhanya ni mtoto wa dada yangu ili apate ajira maana ningesema mdogo wangu majina yangeumbua.
Sikuhitaji malipo, nilikuwa nikimpa kampani ndogo ndogo kabla hajaajiriwa. Hata alipoajiriwa kuna siku alikwama akaomba nimkopeshe pesa kidogo atalipa mwisho wa mwezi. Nikamtumia pesa zaidi ya aliyohitaji na nikamwambia siwezi kukukopesha nakupa tu free, si vyema tuishi maisha ya kukopana fedha. Leo kanitext nilijua anataka anishukuru arudishe kiutu uzima ile pesa niliyomtumia kumbe anataka nimpigabie ajira ofisi fulani ya umma.
Nadhani hii tabia ya kutojielewa sijui ni mazao ya origin ya mtu. Watu wa kusini shukrani kwetu ni kitendawili.
Ok . Badala ya kujipambania sasa unataka ubebwe tena.
Note: Mimi si dalali wa ajira na sihitaji pesa ya mtu . Nimezungumza tu kijana lazima uwe na akili timamu katika utafutaji wako wa maisha.
Vijana wetu wa kileo wengi ni tatizo, shida inasnzia kwenye malezi ngazi ya familia.
 
Afadhari wewe huyo uliemsaidia bado yupo kazina na hakuna kashifa yeyote ili iliyotokea, sasa mimi nilimpambania mtoto wa dada binamu ktk ukoo na ukizingatia elimu yake ni fomu 4 mwenye D 2 na akapata kazi nzuri tu mshahara laki 5, lakini cha ajabu kaenda kazini siku mbili tu na kuacha kazi hadi dada (mama yake mzazi) alidondosha kilio na machozi baada ya kuona binti yake kagoma kwenda kazini.

Leo hii nimepita ktk kampuni fulani wameniomba niwatafutie mfanyakazi nikakimbuka lile sakata nikasema moyoni simtafutii tena mtoto wa mtu kazi nilikumbuka issue ya yule binti alivyonidhalilisha baada ya kuacha kazi.
 
Jmn kweli kwenye miti hakuna wajenzi
😞
Ila hapana, usiache kufanya Kwa sehemu Yako mkuu huwezi jua
 
Mjinga huyo mm nlipigania vijana wawili wakapata kazi ya udereva wa maroli ya kokoto aisee wale vijana nliishi nao vizuri sana popote watakaponikuta hawaniachi nasafiri buleee na pesa ntapata. Matunda naletewa. Nliishi kibosi sana
 
Jambo kama shukrani ni tabia ya mtu ya ndani sio kabila wala kikundi cha watu ...sema mimi ni wa kusini watu wa kusini tuna kakiburi flani iv na kwa asili Ka uvivu kamo cha kutaka mtu akubebe kla mahala sema sio wote ila asili ya walio wengi
😍😍Kuchidachi wamakonde wenzangu.
 
Back
Top Bottom