Ulichokiandika ni utafiti ambao ulishafanywa na wanasaikolojia. Mwanamke aliyelelewa na single mother watafiti wanasema wana changamoto zifuatazo kwa uchache:
1) Wanajiamini sana (overconfidence)
Kitu ambacho muda wote wanajiona wapo sahihi kwa kila wanachokisema na wanachokifanya. Tabia hii inawajengea wanakuwa wajuaji mnoo! Na tabia ya ujuaji mnamfanya ni mwanamke asiyemsikiliza mwanaume wake na ni tabia ambayo hata ukithubutu kumsahihisha hakubali kosa.
2) Hajui nafasi ya mwanaume ipi kwenye mahusiano
Kwa sababu kwenye malezi yake amekosa father figure haijui nafasi ya mwanaume ni ipi kwenye mahusiano. Hii inapelekea kutoweza kuthamini jitihada za mwenzake.
3)Anataka a-control kila kitu
Wataalamu wanasema kwa kuwa kila kitu alisimamia mama kwenye malezi hivyo kwa binti hudhani mwanamke ndivyo inavyompasa kuishi kwenye maisha yake. Hivyo binti huyu akiwa kwenye mahusiano naye atataka kum control mwanaume yaani awe juu yake. Yeye ndiye aamue kila kitu na ndiye mwenye kauli ya mwisho.
4) Ana ujike udume
---------------------
Aina hii ya mwanamke huwa hafahamu nafasi yake ni ipi! Kukuheshimu na kukupatia nafasi yako kama mwanaume ni ngumu. Ili uweze kumdhibiti ni kwa namna mbili: Mosi, kupitia kwa mama yake ikiwa kama mama yake ni muelewa kwani aina hii ya wanawake wanawasikiliza sana mama zao, mama yake ndiye kila kitu. Kwa msingi huo ufahamu ya kwamba atakayekuwa anafanya maamuzi kwenye ndoa yako ni mama yake.
Pili, awe amesoma masomo ya dini. Hii itasaidia kwa kumuogopesha kuwa anayoyafanya anamuasi Mungu wake. Kwa kuwa dini inamtaka mwanamke amheshimu mwanaume wake inamfanya kwa kiasi fulani kumfanya afakirie yale yanayomsukuma kutokana na malezi aliyoyaishi.
Mbaya zaidi hawa wanawake huwa hawafahamu kama wana matatizo mpaka yawakute mambo mengi ndipo atakapojihisi kama ana dosari.
Na hata familia ambazo mwanamke ndiye mwenye sauti sana kuliko mwanaume ndani ya ndoa huwa zinatoa mwanamke wa namna hii! Kwa sababu kiigizo cha mwanamke ni mama yake. Ikiwa mama kwenye familia ni kila kitu fahamu ya kwamba utatoa aina hii ya mwanao (binti) kwenye jamii.
Nukta ya nyongezea, aina hii ya mwanamke huwa anamsikiliza sana mama yake na rafiki zake kuliko wewe mwanaume wake.