Mleta mada hujawahi kuona mtu:-
1. Kafungua duka, bar, saloon, hoteli, n.k halafu vikafa kabla ya kumpa faida?
2. Kalima shamba, kafuga, n.k halafu hakuna alichopata?
3. Kagombea udiwani, ubunge ama urais kwa kutumia rasilimali zake nyingi halafu kaangukia pua?
4. Kajenga jumba kubwa akafa siku 2 kabla ya kuhamia, kanunua mabasi yakaungua wiki 1 baada ya kuanza route.
Nataka kusema nini hapa?
Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kila kitu ktk maisha ni kubahatisha (kubeti).
Hivyo wanaobeti ktk mpira waendelee kama wengine wanavyoendelea ktk nyanja nyingine