Darkhorse001
JF-Expert Member
- Dec 19, 2020
- 306
- 538
Hatujasema kuoa kutakufanya ufie masikini wala tajiriKuoa sio sababu ya kufa masikini au kutooa na kuishi pekee yako ikawa sababu ya kuwa tajiri maisha haya fomla leo masikini waleo ndie tajiri wakesho tajiri waleo ndie,,,, mambo haya yako kiiimani zaidi
Tunachojaribu kusema hapa ni kwamba, kama kijana kakosa mahari ya kulipa (Tena kijana wa kiislamu ambako mahari haifiki hata 2M)
JE ataweza kuhudumia familia na ikakua kwenye ustawi!
Haya mambo hayahitaji hata nguvu kubwa kubishana
Umesema kwamba anaweza kuwa anaingiza 15k kwa siku, kama hawezi kuweka akiba ikafikia Kiasi Cha kwenda kutoa mahari basi hata kaa akioa ataongeza majukumu na hvyo hyo 15k itakua si kitu kwake (labda kama atabahatika kuoa mwanamke mpambanaji au mwenye kazi)
Just assume, unaingiza 15k kwa siku, unatakiwa kulipa Kodi, ununue chakula, ulipe bills, ununue mahitaji mengine na baada ya miaka kadhaa uanze kuhudumia watoto!!
Hata ww inakuja kweli?