Enzi za wazazi wetu walikuwa wanahusudu sana binti aolewe akiwa na bikra yake, au kijana aoe binti mwenye bikra, na hii sio kwasababu walitaka kijana afungue njia wa Kwanza, no, lengo ilikuwa ni kijana afungue moyo wa binti akiwa wa kwanza. Kuna kampeni kipindi cha nyuma ilikuwa inaendeshwa humu JF, kwamba kama sio bikra usioe, coordinators wa hii kampeni walikuwa wanadhani binti ukimtoa bikra, basi hawezi kukusaliti, huo ni uongo, wapo wengi waliotolewa bikra na bado waliweza kusaliti. Ila advantage ya mwanamke uliyemtoa bikra, moyo wake unakuwa hauna majeraha ya mapenzi, hauna vinyongo wala visasi.