Viongozi wa Afrika watakiwa kutoa ushahidi wa pesa za misaada

Viongozi wa Afrika wanahitaji kutupatia ushahidi wa kile wamekuwa wakifanya katika zaidi ya dola bilioni 13 wanazopokea kutoka Marekani kila mwaka au warudishe fedha hizo." — Elon Musk
Waje tu maana tunaona fedha zinazotajwa ni nyingi lakini hatuoni cha maana ila tunaona "wakubwa" wakiogelea ktk utajiri wa kutisha kuliko hata wafanyabiashara maarufu nchini!
 
waanze na consultant wao wamepiga pesa sana,tenda nyingi wamefaidi wamarekani ukianza na ARVs.
 
Wamarekani walisifiwa sana kwa kutoa misaada tangu zama za miaka ya sitini kuja kwa uponi mpaka misaada ya miradi ya afya kama malaria, ukoma kifua kikuu na UKIMWI. Sasa wameshituka misaada yao haitumiki vema. Sali la kuuliza, utampangiaje mtu namna ya kutumia msaada uliompa?
Unampangia pale unapokuwa umempa misaada ya kujikwamua, umepewa pesa kwa ajili ya kupambana na malaria unatumiaje misaada hiyo kununua mabasi ya CCM.
Screenshot_20250314-095211.jpg
 
"Viongozi wa Afrika wanahitaji kutupatia ushahidi wa kile wamekuwa wakifanya katika zaidi ya dola bilioni 13 wanazopokea kutoka Marekani kila mwaka au warudishe fedha hizo." — Elon Musk

"Fedha zinatumika vibaya zaidi unapokuwa unatumia fedha za mtu mwingine kwa watu usiowajua. Utajali kiasi gani jinsi unavyotumia fedha wakati si zako? Hivi ndivyo Serikali yetu ya Shirikisho inavyotumia fedha zetu. Wanatumia fedha za mtu mwingine kwa watu wasiojua. Na tunapotaka kupitia jinsi fedha zote zimetumika, hatuoni chochote. Watu wanaopokea fedha wanataka kuendelea kupokea fedha na hawafanyi kile wanachopaswa kufanya nazo. Wanataka tu kuzitumia kujinufaisha wenyewe. Sababu ya mimi kuweka juhudi nyingi katika kusitisha USAID ni kwa sababu nafikiri ni hali mbaya sana. Si hiari na kama viongozi wa Afrika hawawezi kutoa ushahidi wa kile wamekuwa wakifanya na mabilioni tunayowapa kila mwaka, basi hawazihitaji. Marekani inafilisika na hatuwezi kuruhusu hilo." — Elon Musk kiongozi wa Idara ya Ufanisi ya Serikali ya Marekani

Kulingana na ripoti, nchi za Afrika zinadaiwa kupokea zaidi ya dola bilioni 13 mwaka 2024 kwa ajili ya kujenga shule, hospitali nk

View attachment 3269171
Kwani tuliwalazimisha watupatie huo msaada na kuna kipengele katika mkataba kinasema tunaweza kydaiwa kurudisha hiyo pesa?
Tumejengea majumba na nyingine tumeweka huko kwenye akaunti za nje kwa ajili ya familia zetu.
 
c mama alikuwa anatembeza bakuli huko duniani kufungua nchi
 
Hiyo misaada wametoa tangu na tangu ndio maana USAID imekuwa hapa kwa miaka mingi.
Halafu hiyo misaada ukitazama vzuri hata haikuwa ya bure, ilikuwa inatunika kuinfluence agenda na ukubwa wao. Sasa kama hunipi chochote utanipaje masharti.
Ila pesa tulikuwa tukanunua na majumba nje
 
si muhimu na wala sio Lazima kufanya hilo licha ya kua ushahidi upo wa kutosha tu.

hakuna alazimishwae kusaidia anae jiweza 🐒

Ni muhimu sana sababu ya kukosa uadilifu na uwajibikaji. Tunanunua magari mengi kwenye project husika. Magari ambayo tunaishia kugawana bila kuhakikisha project zinakamilika.
Kusema kweli USA wamefanya kitu sahihi. Mtegemea cha ndugu hufa maskini. Tuanze kuwajibika wenyewe kwa maendeleo yetu
 
Hiyo misaada wametoa tangu na tangu ndio maana USAID imekuwa hapa kwa miaka mingi.
Halafu hiyo misaada ukitazama vzuri hata haikuwa ya bure, ilikuwa inatunika kuinfluence agenda na ukubwa wao. Sasa kama hunipi chochote utanipaje masharti.
Ila pesa tulikuwa tukanunua na majumba nje

Tunakataa sasa hivi sababu tumenyimwa. Mbona tulikuwa hatusemi lolote tulipokuwa tunapokea?
Tuanze kutumia tunachokusanya kufanya maendeleo yetu. Haya mambo ya misaada yana mwisho. Tulikataa ujamaa...kwanini tunakataa kujitegemea?
 
"Viongozi wa Afrika wanahitaji kutupatia ushahidi wa kile wamekuwa wakifanya katika zaidi ya dola bilioni 13 wanazopokea kutoka Marekani kila mwaka au warudishe fedha hizo." — Elon Musk

"Fedha zinatumika vibaya zaidi unapokuwa unatumia fedha za mtu mwingine kwa watu usiowajua. Utajali kiasi gani jinsi unavyotumia fedha wakati si zako? Hivi ndivyo Serikali yetu ya Shirikisho inavyotumia fedha zetu. Wanatumia fedha za mtu mwingine kwa watu wasiojua. Na tunapotaka kupitia jinsi fedha zote zimetumika, hatuoni chochote. Watu wanaopokea fedha wanataka kuendelea kupokea fedha na hawafanyi kile wanachopaswa kufanya nazo. Wanataka tu kuzitumia kujinufaisha wenyewe. Sababu ya mimi kuweka juhudi nyingi katika kusitisha USAID ni kwa sababu nafikiri ni hali mbaya sana. Si hiari na kama viongozi wa Afrika hawawezi kutoa ushahidi wa kile wamekuwa wakifanya na mabilioni tunayowapa kila mwaka, basi hawazihitaji. Marekani inafilisika na hatuwezi kuruhusu hilo." — Elon Musk kiongozi wa Idara ya Ufanisi ya Serikali ya Marekani

Kulingana na ripoti, nchi za Afrika zinadaiwa kupokea zaidi ya dola bilioni 13 mwaka 2024 kwa ajili ya kujenga shule, hospitali nk

View attachment 3269171
Mwamba apewe maua yake
 
Ni muhimu sana sababu ya kukosa uadilifu na uwajibikaji. Tunanunua magari mengi kwenye project husika. Magari ambayo tunaishia kugawana bila kuhakikisha project zinakamilika.
Kusema kweli USA wamefanya kitu sahihi. Mtegemea cha ndugu hufa maskini. Tuanze kuwajibika wenyewe kwa maendeleo yetu
Kama Taifa,
tutaendelea kuwajibikia maendeleo ya wananchi na waTanzania wote bila kushurutishwa na mmatumbi kutoka taifa lolote duniani,

Tutaendelea kununua vifaa vya kazi kwa fedha zetu wenyewe na kuvitumia kwa maslahi mapana ya wananchi wote wa Tanzania.

anaejitia kimbelembele cha kutoa misaada anakatibishwa na misaada yake itapokelewa lakini kamwe hatutakua na haja ya kubabaika nae kama Taifa huru linalojitegeamea 🐒
 
Tunakataa sasa hivi sababu tumenyimwa. Mbona tulikuwa hatusemi lolote tulipokuwa tunapokea?
Tuanze kutumia tunachokusanya kufanya maendeleo yetu. Haya mambo ya misaada yana mwisho. Tulikataa ujamaa...kwanini tunakataa kujitegemea?
Eeeh kama wanataka tuwape ripoti hatuwapi hata wasipoleta waache sisi tushajijengea majumba na nyingine tukaweka huko uswiss.
 
Kununua magari ya washawasha kwa ajili ya uchaguzi. ushahidi namba tatu huo
 
Naunga mkono hoja hyo.
Nafurahi viongoz watabanwa na maendleo yataonekana ila naskitika waafrica tutalipa nin? Au jamaa wanamipango yao juu ya rasilimali zetu. Napata HISIA MCHANGANYIKO
 
naomba tu wamarekani watambue kuwa, ss waafrica wenye uchungu na bara la africa, tunamtaka trump ikulu ya marekani (white house) mpaka 2040 tu. Wakifanya hvo roho zetu zitasuhuzika sana.
 
Elon ameamua kutukalia kooni, ana haki ya kujua pesa zinafanya nini, ila hajui kuwa ripoti ya uongo inaweza kutengenezwa.
 
Back
Top Bottom