Viongozi wa dini waliokutana Rais Samia Wamemshauri kuifuta kesi ya Mbowe

Nawasiwasi lisu atakataa viongozi wa
 
Hapo kuna viongozi wa dini wametumika ili hata Mbowe akifutiwa kesi,ionekane ni kwa maombi ya viongozi wa dini lengo kuiondolea serikali aibu
"Mkubwa hakosei" Ndivyo walivyofanya
 
Lisu hatawagomea viongozi wa dini kama alivyomfanyia zito?
 
Hawa Viongozi Macho Yao Wameiona Kesi moja tu Mahakamani? Mbona ipo mikesi mingi tu Wameifumbia Macho..!
Wajikite Kumtangaza Mungu , haya mambo Sijui futa Kesi Ya Sabaya ,Sijui futa Kesi Ya Mbowe Waachane nayo...!
Sabaya hawezi kufutiwa kesi. Yule ni jambazi na tulipiga kelele sana humu ila mlimuona ni shujaa wa taifa, sasa atanyea ndoo kwa miaka 30
 
Mahakama Kutenda kazi inashirikiana DPP kwa hiyo hata DPP atatenda kazi
 
Hawa Viongozi Macho Yao Wameiona Kesi moja tu Mahakamani? Mbona ipo mikesi mingi tu Wameifumbia Macho..!
Wajikite Kumtangaza Mungu , haya mambo Sijui futa Kesi Ya Sabaya ,Sijui futa Kesi Ya Mbowe Waachane nayo...!
KESI za kuku ndio wahangaike nazo tumia Akili hata za jirani zako
 
Hawa Viongozi Macho Yao Wameiona Kesi moja tu Mahakamani? Mbona ipo mikesi mingi tu Wameifumbia Macho..!
Wajikite Kumtangaza Mungu , haya mambo Sijui futa Kesi Ya Sabaya ,Sijui futa Kesi Ya Mbowe Waachane nayo...!
Usiwapangie......
 
Mahakama ina kazi gani sasa kwa mujibu wa katiba ya JMT?

Hao viongozi wa dini wamelewa mvinyo!
Hapana hawajalewa mvinyo....

Bali ni namna nyingine ya wao kusema "MBOWE SI GAIDI" maana hata Rais Samia mwenyewe anajua hilo kuwa huyu bwana siyo gaidi...

Rais Samia alilikoroga mwenyewe na sasa anatumia njia ya mzunguko kulimaliza hili kwa kuwatumia hawa the called "vingozi wa dini" akidhani watu wazima wenye akili timamu hatuwezi kuelewa kilicho nyuma ya pazia....
 
Tuliyajua haya maana jaji ameshajichanganya kesi yenye kurasa zaidi ya elfu naaa aliitolea hukumu ndani ya dakika 5 tu
 
viongozi wa michongo hao hakuna lolote hapo
 
Ukinielewesha bila kutumia kebehi unapungukiwa nini pu.mbavu wewe au hujaona kuwa nimeuliza swali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…