Viongozi wa Dini wanazungumza na Serikali kuhusu Mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na Dubai
Maoni yangu hayana tofauti na mjadala uliofanyika bungeni.

Ule ndio ukweli wenyewe, tunachojadili ni azimio tu la bunge kuweza kuingia mikataba ya utekelezaji ambayo mpaka sasa aipo.

Mengine kwenye hiyo IGA ni mambo ya kawaida kabisa kwenye FDI contracts, implied terms za sheria za nchi husika, dispute resolution processes na kadhalika yaliyomo mule.

Why unafikiri hili swala limegeuka "kuuzwa Kwa bandari"??
 
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anazungumza na viongozi wa dini mbalimbali kuhusu mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii wa bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai.

Mkutano huo unafanyika kwenye Ukumbi wa Kurasini Centre, TEC Jijini Dar es Salaam, leo Jumatatu Juni 12, 2023.

Baadhi ya viongozi wa Dini mbalimbali walioshiriki katika mkutano huu ni;
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mchungaji, Moses Matonya
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Stanley Hotay
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Mkuu, Gervas Nyaisonga
Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Viongozi wa Dini kuhusu haki za kiuchumi na uadilifu wa uumbaji (ISCEJIC), Sheikh Khamis Mataka
Katibu mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKATWA), Alhaj Nuhu Jabir Mruma
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Pwani na Mashariki, DkT. Alex Malasusa
Mwakilishi wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA)

Prof. Makame Mbarawa...
Azimio hilo la ushirikiano limepitishwa na Bunge Juni 10, 2023, lakini pamoja na hivyo Serikali ya Tanzania imeona kuna umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu mkataba huo.

Nchi yetu imeendelea kuwekeza katika Bandari zetu kwa vyanzo tofauti, pamoja na hatua mbalimbali, bado Bandari hazijafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.

Mfano wa Meli kusubiri kutia nanga kwa Dar es Salaam ni siku tano tofauti na wastani wa siku 1 na saa 6 kwa Bandari ya Mombasa.

Ufanisi wa Bandari unashindwa kufikia kiwango cha kimataifa unatokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa mifumo mizuri ya TEHAMA na mitambo ya kisasa inayobadilika kutokana na teknolojia.

Athari za kutokuwa na Bandari ya kisasa ni meli kusubiri muda mrefu, kunakosababisha gharama kuongezeka, mfano kwa meli kusubiri kwa siku ni Tsh. Milioni 58.

Kukosesha mapato ambayo yangeweza kutumika kuboresha uchumi wa Taifa.

Ufanisi wa uendeshaji wa Bandari bado ni wa kiwango cha chini, Meli kutumia muda mrefu kupakua mzigo, meli kubwa kushindwa kuingia kwenye Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kuchukua muda mrefu kuingia Bandarini.

Kutokana na changamoto hizo, Mwaka 2000 Serikali ya Awamu ya Tatu iliingia mkataba na Kampuni ya TICTS uliodumu kwa miaka 22, ulioipa haki kampuni hiyo katika Gati namba 8 hadi namba 11 wakati maeneo mengine yakiendelea kuwa chini ya Mamlaka ya Bandari Tanzania.

Mwaka 2017 Serikali ilifanya mabadiliko makubwa katika mkataba lakini Mwaka 2022 Serikali iliona hakuna umuhimu wa kuendelea kufanya kazi na TICTS.

Desemba 2022, baada ya kuona mkataba huo hauendani ma matarajio ya Serikali, ndipo ikaanzisha mchakato wa kupata mwekezaji Bandarini.

Serikali ilipokea mapendekezo ya kampuni mbalimbali kutoka Hong Kong, Ubelgiji, India, Ufaransa, Denmark.

Baada ya mawasilisho ya kampuni hizo na sifa zao za kimataifa, Serikali iliamua kufanya mazungumzo na Kampuni ya DP World kutokana na uzoefu wake katika soko la Barani Ulaya, Asia, Marekani ya Kaskazini na Kusini na Afrika.

DP World ina uzoefu mkubwa wa usafirishaji, Kampuni hiyo ina miliki zaidi ya meli 100 za mizigo.

Uamuzi wa Serikali iliona makampuni mengine yaliyoomba hayana uzoefu wa shughuli za uendeshaji wa Bandari Afrika wakati DP World inaendesha zaidi ya bandari 30 Duniani.

Februari 27, 2022, Serikali ilisaini makubaliano ya kulenga ushirikiano, baada ya hatua hiyo Serikali iliunda timu ya Wataalamu kufuatilia ushirikiano huo baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai.

Lengo la Mkataba huo ni kuweka msingi wa makubaliano ya Nchi na Nchi ili kuwezesha kuingia makubaliano ya mikataba mingine mbalimbali kama ya upangishaji na uendeshaji.

Kulingana na Katiba, Serikali ya Tanzania ilianzisha mkachato wa kuridhiwa na Bunge ili utekezaji wake uweze kuanza.

Mkataba huo umeweka vifungu muhimu kwa ajili ya kulinda maslahi ya Nchi ikiwemo ajira za Watanzania, ardhi ya Watanzania, ukomo wa mikataba, masuala yanulinzi na usalama na masuala mengine yote yenye umuhimu wa Nchi.

Mikataba hiyo pia itazingatia, kuweka bayana ukomo wautekelezaji, muda wa marejeo ya mkataba mwaka mmoja hadi mitano kutegemea na mkataba husika, viashiria vya utendaji wa mkataba, itakuwa chini ya ofisi ya Mwanasheria wa Serikali kwa kuzinagatia maslahi ya Taifa

Italinda wafanyakazi wazawa na kuwajenga uwezo, mifumo ya TEHAMA ya Kampuni ya DP World itasomana na ile ya Serikali.

Taasisi muhimu zote za Serikali zitaendelea na utekeleaji wake wa majukumu katika maeneo ya Bandari, mwekezaji atachukua hatua zote za Utafiti wa masoko ya Dar es Salaam.

Updates....
Viongozi wa Serikali wakiongozwa na Waziri Prof. Mbarawa bado wanaendelea na mazungumzo ya pamoja kabla ya kutoa tamko juu ya mkataba wa Bandari ambao ndio hoja Kuu inayojadiliwa ukumbini.

TAMKO LA VIONGOZI WA DINI
Baada ya majadiliano ya muda mrefu, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima anasema:

Tumesikia baadhi ya Wananchi hawaridhiki na huo mkataba kama ilivyo kwa baadhi ya Wabunge, ndipo tukaomba kuonana na viongozi wa Serikali kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa mkataba huo wa Bandari.

Wametufafanulia kifungu hadi kifungu na kugundua kuwa Sheria iliyotumika kuingia mkataba huo ni kama ambayo imekuwa ikitumika katika mikataba mingine.

Serikali imekiti kuwa haikutangaza kuhusu tenda ya mkataba huo, imesema kuwa ilimtafuta mwekezaji ambaye iliamini ni mbobezi kagtika tasnia hiyo.

Tanzania tangu tupate uhuru tuliaminishwa na bado tunaamini kuwa mali asili zote na mali yetu wote, hivyo mtu anapotumia tofauti lazima tuulize na tuna haki hiyo.

Bandari ni yetu sote na tumewekeza fedha zetu hapo, hivyo mtu anapokuja na kutaka kuwekeza lazima tuna haki ya kuhoji.

Baada ya kikao na Serikali tumeamua kuwa bado tutaendelea kuchukua maoni ya Wananchi na Waziri amesema kuwa tandike na kuwapelekea maoni yetu.

Mkataba unaweza kurekebishwa
Waziri kuwa amesema pamoja na kuwa Bunge limepitisha bado mkataba huo unaweza kurekebishwa.

Kutokana na hali hiyo tumeunda Kamati ndogo ya kufuatilia kwa akili ya kuwasilisha maoni yetu kwa Serikali.

Pamoja na hivyo tunahakikisha sauti ya Wananchi hazipuuzwi, lazima maoni ya Wananchi yasikilizwe.

Tumewakumbusha Serikali kuwa miaka ya 90 kulitokea wawekezaji kama ilivyo sasa tukaambiwa kuwa Wananchi hawataathirika, lakini tunaona Wananchi wanavyoteseka, wanatolewa kwa nguvu.

Ndugu zetu wale wametolewa kwa nguvu na kupewa nyumba yenye vyumba vitatu wakati unakuta wana watoto 10.

Hivyo, kuna umuhimu wa kuzingatia haki za binadamu pale mwekezaji anapopewa eneo, Serikali isitumike kuumiza raia wake, tumekumbusha hilo.

Mwekezaji (DP World) anawenda kuwekeza baharini lakini wamesema kuwa kila eneo la ardhi litakalokugwa wananchi watahusishwa.

MAREKEBISHO YAKIFANYIKA
Sisi viongozi wa Dini hatuwezi kumkataa mwekezaji, tunachopima ni kama wananchi wanapata taarifa sahihi na wao ndio wanaoweza kuamua.

Hata Rais mwenyewe anasema mikataba lazima ilinde maslahi ya nchi, sisi viongozi wa dini lazima tujali maslahi ya Nchi.

USHAURI WA VIONGOZI WA DINI
Moja kati ya ushauri tulioutoa ni kushauri Serikali kuunda Kampuni ambayo hata ikitokea migogoro inayoshitakiwa ni Kampuni na sio Nchi.

Wenzetu wameunfa kampuni badala ya Serikali kujimwaga moja kwa moja, si umeona kilichotokea kwa Dubai.

Hali hiyo inasaidia hata inaposhitakiwa wa haishitakiwi Nchi bali kampuni.

Unaona mfano inatokea unamnyang’anya mtu heka 10 anaenda kushikilia ndege ya mabilioni.

Kuna vipengele vya kuzingatia siyo kila kipengele tunakikubali, unakuta mtu umempa mageti mawili matatu pale bandarini lakini ikitokea nataka kuendeleza bandari ya Kilwa lazima nikutaarifu, wewe ni nani?

Katiba ya Nchi yetu ni inasema lazima kuwe na usawa, kwanini mwekezaji awe tofauti na wengine.

Vifungu vingine vina makosa madogo madogo ambavyo navyo vinatakiwa kurekebishwa, tumeshauri na wamesema watashughulikia.

NENO LA KATIBU WA BAKWATA
Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Alhaj Nuhu Jabir Mruma anasema:

Tumemaliza salama kikao chetu kati ya viongozi wa Dini na Serikali, kubwa zaidi ilikuwa viongozi wa dini kuelimishwa kuhusu suala la Bandari yetu.

Sisi viongozi wa dini hatukuzungumza kwa kuwa hatukuwa na elimu juu ya mkataba huo, baadhi ya maswali yaliyokuwa yakizungumzwa na Wananchi ndio ambayo tulikuwa tukijiuliza sisi viongozi wa dini.

Tumewaomba Serikali kuendelea kutoa elimu zaidi kwa Wananchi, inaonekana ni jambo zuri lakini elimukwa wananchi ndio haipo.

Pia, soma DOKEZO - Viongozi wa Dini kuunguruma kesho kuhusu suala la Bandari na DP World
WATANZANi WAlIFUNGULIWA NA JPM
 
Upotoshaji

Ndio maana serikali inatakiwa kutoa elimu sahihi.

Kama wasomi wanapewa elimu sahihi na haiwasaidii labda kuna tatizo lingine ..
Binafsi naona kama wawekezaji wangekuwa wazungu..labda ingekuwa tofauti..
Nafikiri chuki Kwa waraabu na religious biased zimechangia zaid
 
Huo mkataba ulitakiwa kuwa kati ya DPW na TPA na siyo DWP na JMT
 
Mbarawa, umewaambia hao mapadre muda wa huo mkataba?

2. Je ni namna gani ya kujiondoa tukitofautiana

3. Asilimia ya watanzania watakao ajiriwa na DP world.

4. Kwanini Rais alisaini mkataba kabla ya wananchi kupitia bunge kuridhia?

5. Kwanini Mwanasheria mkuu wa serikali hajasaini mkataba huo amesaini mbarawa na Saa100 tu.

6. Kwanini DP world hskupewa bandari ya Dar tu amepewa bandari zote Bara na sio visiwani.

7. Kwanini mkataba ulisainiwa Dubai na Rais badala ya DP world kuja kusaini mkataba Tanzania?
Hiyo namba 4 nimesoma hadi mwili unatetemeka, tumefikaje hapa
 
Nini kifanyike ikiwa wale wapumbavu bungeni wameshatokwa povu kwa kutetea?
 
WAWEK MKATABA MEZANI NA WATOE MJADALA HURU WAJIBU MASWALI YA WANASHERIA WETU WA KITAA


TUWAULZE MASWALI 10 WAKIJUBU TUKARZK BAS TUENDELEE
 
Hilo swala sio mambo MTAMBUKO [emoji4][emoji19] wanatakiw wabobez wa kisheriA /mikAtAba, wanauchumi na wanasiasa wenye uwezo wakuchambua mambo


Huyu jamaa wa ACT Yupo Kimyah , kashalamb asali n nn
 
Kama wanajua una tija wasitumie nguvu kubwa kutuaminisha badala yake wasubiri waje watuoneshe matunda yake
Akili zako wewe ni ....! Ni saw na kusema kama njia hii kuna Simba MLA watu ,Mimi napita nione kamaal ataniyafuna au la!
 
WAWEK MKATABA MEZANI NA WATOE MJADALA HURU WAJIBU MASWALI YA WANASHERIA WETU WA KITAA


TUWAULZE MASWALI 10 WAKIJUBU TUKARZK BAS TUENDELEE
Spika alisema huu sio mkataba lkn waziri anasema mkataba huu..........
 
Nchi yetu imeendelea kuwekeza katika Bandari zetu kwa vyanzo tofauti, pamoja na hatua mbalimbali, bado Bandari hazijafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.
Uhuni mtupu, kwanini tuseme inawekeza badala ya inawekezwa? Ubinafsi na uchawa ndiyo unaleta statement za kipumbavu kama hizi, kwanini msiwajengee uwezo watu wa ndani ili kuwapanulia raia wenu soko la ajira wakati?
 
AZIMIO LA MWISHO WA KIKAO HICHO LIWE NI KUCHUKUA MKATABA HUO NA KWENDA KUUTUPA CHOONI.TUACHE UPUMBAVU KAMA TAIFA,NCHI IMEJAA VYUO VIKUU VYA KUZALISHA WAPUMBAVU TU,LI NCHI LINAZIDI KUJAZA WATU AMBAO HAWANA AKILI NA BAHATI MBAYA WASIO NA AKILI NDIO VIONGOZI.WATU MILIONI 63 WANASHINDWA KUENDESHA BANDARI?AJABU SANA HII,NCHI YA WATU MILIONI 3 NDIO INATUDRIVE,CCM ACHIENI NCHI KWA SASA HAMNA AKILI YA KUONGOZA TAIFA HILI MMEFELI KWA ASILIMIA 1000%.YAANI UPINZANI HAUPO BUNGENI NA MMESHINDWA KABISA KUFANYA KAZI KWA AKILI.BUNGE LIMEJAA VILAZA WATUPU,HV BUNGE KAMA HILI LILILOSHINDWA KUELEWA MKATABA RAHISI KAMA HUU TENA WENYE TERMS ZA KIPUMBAVU NA ZA WAZI KWA NN TUSISEME HILI NI BUNGE LA VICHAA.
Kichaa hawezi kusaini huo mkataba atakimbia tu labda umshike mkono.
 
Hakuna mkataba uliosaniniwa kwa sasa ila ni makubaliano tu ambayo yapo kwenye maandishi

Kilichotokea ni kwamba TUCHUKULIE MFANO kwamba wewe nyumbani kwako unafuga mbuzi, na mimi kwangu nafuga ng'ombe. Ikafikia mahali tukaamua mimi na wewe tushirikiane kuchunga mbuzi na ng'ombe zetu kwa zamu na hivyo vijana wetu wachungaji wakakutana na kuweka makubaliano hayo kwenye maandishi kwamba tutaKapokuwa tumeanza ushirikaino wetu, vijana wangu kutoka nyumbani kwangu MZEE A watakuwa wanachunga ng'ombe na mbuzi kwa wiki moja, halafu baada ya hapo wanachunga vijana wako wewe MZEE B

Hadi kufikia hapa MJI WA MZEE A ukawa umeweka maubaliano ya aina hii na MJI WA MZEE B ambayo yatakuja kutekelezwa baadaye

Muda ukishafika, wachungaji wenyewe sasa (tuseme MCHUNGAJI A KUTOKA MJI WA MZEE A na MCHUNGAJI B KUTOKA MJI WA MZEE B ) watasaini sasa mkataba wao wawili unaosema kuwa kuwa kila mmoja wao atakuwa anachunga mbuzi na ng'ombe kwa wiki moja, halafu baada ya hapo anachukua zamu mwingine

Kwa hiyo hadi hapa, WACHUNGAJI A NA B bado hawajasaini mkataba wowote, isispokuwa kuna makubaliano tu kati ya MIJI YA WAZEE WAO A NA B

Ikija kutokea tuseme muda wa kuweka mkataba kati ya wawili hawa ukafika halafu mmoja wao (MCHUNGAJI A AU MCHUNGAJI B) akawa hajaridhika, mkataba kati ya wachungaji hawa hautawekwa na hakuna mmoja wao atakayekwenda kushtaki mahakamani kwa sababu hapajawahi kuwepo mkataba kati yao, isipokuwa makubaliano tu kati ya KAYA/ MIJI ya wazazi wao

Bora ungelinganisha mfugaji wa mbuzi na mfugaji wa simba
 
Kama wanajua una tija wasitumie nguvu kubwa kutuaminisha badala yake wasubiri waje watuoneshe matunda yake
Watuoneshe matunda wakati tukiwa tumeishapigwa? Heri nusu shari kuliko shari kamili
 
Back
Top Bottom