Vita ya marafiki ni kali sana kwenye mafanikio kuliko mtu baki

Vita ya marafiki ni kali sana kwenye mafanikio kuliko mtu baki

Rahisi Sana kuandika hivi ukiwa uko kwenye amani au mda ambao changamoto ya kuhitaji msaada wa watu ijakufiks
Mkuu aisee umejua nimekua desperate namna gani halafu nina marafiki matajiri kabisa sikuwafata.
Nilifata tuliokua karibu hasa niliowahi kuwasaidia..
!
 
Nadhani ni busara kumwambia pia kuwa akisaidia mtu asitegemee kurudishiwa wema!! Hii itamisaidia kujua kuwa kwemue mapambano ya utafutaji yupo alone na kama misaada si ya kutegemea hata kama uliowasaidia wanakuona ukitaabika.
Ni kweli hii nimejifunza halafu boss...msaada na deni ni sawa...au msaada na kukopeshana?
 
Kuna kazi nimefanya mahali...sasa kuna mpunga mrefu natakiwa nipewe...kikwazo ikaja kuna documents inatakiwa (CODE) Na hiyo code ni hela inatakiwa 2,500,000 nikapambana nikatoa 1.5 bado 1m nikakwama...!

Nikiri na umri huu nimejifunza kitu kipya ambacho nilikua nakiskia na kukiona kwa watu sa hv kimenitokea...

Nikawafata ma hommies wale wa ndani kabisa (Inner Circle) nikiwaomba wanisaidie hiyo 1m...

Hola...wa kwanza akaniambia ni mtee kabisa...!
Hola... wa pili mtee
.
.
.
.wa sita akaniunganisha mahali nikope....baadae mkopeshaji na alienipeleka hawashiki simu

Nikakaa nikawaza nimekosea wapi?

Kumbe nawachana live kwamba nadai so na so...aisee kumbe wanapanick...uzuri deal nimekamilisha ila kulipwa bado na mzigo ushatumika....so lazma nilipwe...

Nimeweka pozi...

Nasubiria mda wowote nitamalizia hiyo 1m ila nimejifunza kitu..hawa hawa ndio mm huwaokoa kwenye angle ngumu sana..mmmoja kodi..mmoja central mmoja harusi...na hela yenyewe wanarudisha dusco dusco...ila this tyme wataniona kauzu kama sielewi hv..!

Usimtegemee Mtu Yoyote...Yoyote ukiwa na shida!
!
We ushatapeliwa........yaani upate dili kwa kutoa dili? Ulisikia wapi?

Ndugu yangu kabisa alinipigia simu akiniambia kuwa Kuna Mchongo wa Uteuzi wa kuwaAfisa Elimu Wilaya fulani. Ila mchongo wenyewe inabidi utoe 1M ya Chapu chapu so Jamaa yangu anataka nimpige Tafu 500k.

Kwa sisi watoto wa shamba tunajua kabisa huo ni Utapeli 100%.

Aidha anataka kunitapeli mimi au Yeye anaelekea kutapeliwa.

Ile pesa nilikuwa nayo sikumpa na nilimuona ni mjinga.
 
Ukishakuwa mwanamume kumbuka hili;

No one cares about your struggles, pain or hustles, they only care about your SUCCESS

Sasa wewe pambania hapo kwenye SUCCESS
Ni kweli kabisa mkuu, ukiwa unatafuta unapitia mengi sana kuna muda unaanguka, unaumia na hakuna wa kukujali. Wewe ndio msaada wako pekee usiposhtuka ukaendelea na mapambano hakuna atakaefanya hivyo kwa ajili yako.
 
We ushatapeliwa........yaani upate dili kwa kutoa dili? Ulisikia wapi?

Ndugu yangu kabisa alinipigia simu akiniambia kuwa Kuna Mchongo wa Uteuzi wa kuwaAfisa Elimu Wilaya fulani. Ila mchongo wenyewe inabidi utoe 1M ya Chapu chapu so Jamaa yangu anataka nimpige Tafu 500k.

Kwa sisi watoto wa shamba tunajua kabisa huo ni Utapeli 100%.

Aidha anataka kunitapeli mimi au Yeye anaelekea kutapeliwa.

Ile pesa nilikuwa nayo sikumpa na nilimuona ni mjinga.
Siwezi kuweka kila kitu...ila ungekua unafanya biashara ungeelewa kwa watu wa supply wanajua naongea nn...!
Ila kesho namaliza mchezo mkuu...

Sijisifii...ila kunitapeli mm ni ngumu sana...! Ngumu niamini!
 
Yaaap unajua hii ni sawa kabisa...
Hili nimeliweka...
Nimepitia mengi kwenye ishu za hela uzuri nilishajifunza mapema cha mtu sio changu na sina haki nacho including marafiki. Huwa nilivyo msiri wa mambo yangu naamini kwa wengine nayo ni hvyo hivyo, nikikwama kifedha na nikakosa msaada kwa walionizunguka nnaamini pia hata wao ni watu kama mimi, naelewa hali zao huenda na wao wanapitia hali fulani ni vile hawajaamua kuweka wazi.
 
Sijasema mwandiko kuhusu usahihi namaanisha style.

Hao unaofahamu ulitakiwa utarajie matokeo uliyopata kutokana na wao kusumbua kurejesha hela yako.
Mtu anayesumbua kurejesha hela, huwa hakusaidii endapo utataka. Na mara nyingi atakusema vibaya au kuleta kinyongo ukitumia nguvu kiasi kupata hela yako. Ni sawa na wateja njaa kali, huomba discount kubwa na hununua vitu cheap, hulalamika zaidi na huwa hawarudi.

Kuna classmate wangu anasona MD yeye ni rafiki kwenye kula bata, kukulazimisha mtoke out ukatumie 150k yake ni kawaida kwake ila kukusaidia 100k kwenye mambo yako umrejeshee baadae ni vigumu. Huyu anakupa 150k yake utumie akitarajia baadae atakwama umpe 150k atumie kula bata.
Nina mzee ndugu yetu kwenye ukoo ni billionaire, kwenye list ya watu wa kuaminika kwake nipo ila hawezi nikopesha hata 1M ila ukimpa proposal ambayo atapata share anakupa hela. Anataka ombi liwe na details zinazogusa hivi "nipe 20M kuna deal 1,2,3 tutapata ROI in 4 months na baadae tutaanza gawana faida utapata 50%".

Leoleo kuna mtu nimepewa deal ila sijui napataje kulifanikisha nikampigia jamaa yangu mmoja huwa ananisaidia akanipa details nikamaliza na kupata faida sio mbaya, nikamtoa ya soda. Juzi niliingiza hela kiasi na kuna jamaa nilimuelekeza kazi siku za nyuma Jmosi akapata hela akataka kunitumia kidogo kama shukrani nikakataa, najua nitamtumia nikiwa na shida aniboost.

Kufupisha story nasemaje: Kila mtu ana code ya kutoa hela yake, haitoshi tu kusema ni mtoaji. Na vilevile kila mtu ana tamaa na hela yake, kitendo cha kukupa hela ni risk hivyo kuna watu hawataki kuingia risk isiyo na return. Kikwete anasema kihuni kwamba ukila sharti na wewe ukubali kuliwa.
Sasa si ndio maana ameumia kwasababu yeye ameshaliwa sana, lakini yeye hajawala wenzie, ilipokuja muda wa yeye kuwala wenzie wakamtosa.

Anachokilalamikia huyu ndugu, kibinadamu muelewe tu. Ukweli ni kwamba nikipata shida lazima niwacheki wale ambao nao huwa wananicheki wakipata shida, ikienda tofauti lazima niquestion kama ni watu sahihi. Ndicho kilichompata huyu ndugu yetu.
 
Back
Top Bottom